TIC na Bodi ya Utalii watumieni Ma Celebrities wanaokuja nchini

image

Ni Miaka 10 Sasa tangu Tamasha la Fiesta limeanza likiwa na majina tofauti tangu enzi za Dar Carnival mpaka sasa Fiesta. Ni Tamasha ambalo linakutanisha wanamuziki na mashabiki wao huku likiwa na kauli mbiu ila kikubwa ni kufikisha burudani na kuwakutanisha watanzania bila kujali umri kwani wengi wa washiriki ni vijanalakini pia wapo watu wa makamu na hata watu wazima pia. Lazima tukubali Prime Time na Clouds ni baba wa Burudani si tu kwa Tanzania bali Afrika ya Mashariki kwa ujumla.

Shukrani na hongera kwa timu nzima ya waandaaji wa Tamasha hili kubwa kwani kupitia wao tumeweza kuwaona wanamuziki wengi wakubwa wakiletwa hapa nchini katika kuchangiza na kunogesha Tamasha hilo.

Wengi wa wanamuziki hawa ni Macebrity wakubwa si tu kwa nchi wanazotoka yaani USA au Jamaica peke yake la hasha ni Dunia nzima kama si Africa Nzima.

Habari za safari zao huwa ziko kwenye mitandao yote ya burudani na picha za matukio yao huwa zinatupwa kwenye mitandao kila kona. Ikumbukwe pia hawa wanamuziki wa kipato kikubwa sana ama kwa mauzo ya kazi zao, matamasha wanayoyafanya, mikataba ya matangazo na mengineyo hii inawafanya wawe katika rank za juu kwenye orodha ya matajiri duniani. Kwa mujibu wa taarifa za mitandao Ludacris alikuwa anaongoza kwa mauzo kwa wanamuziki wanaotoka pande za kusini akiwa na zaidi za copy 19.5 millioni ambazo zimeshauzwa. (Gomba hapa upate takwimu zake)

Dhumuni la makala yangu hii ni kutaka kuwakumbusha Bodi ya Utalii na Kituo cha Uwekezaji hapa Tanzania TIC, nahisi hii ilikuwa ni nafasi kubwa kwa wao kila mmoja wao kutupa shilingi yake wani si rahisi kuwapata hawa watu na mpaka mwanamuziki wa Marekani anakubali  na kusaini mkataba wa kuja kufanya Show hapa Tanzania atakuwa ameshatafuta habari za kujua hiyo Tanzania iko wapi na vitu kama hivyo.

Kwa TIC wanatakiwa waonyeshe ushirikiano na kubaini maeneo ambayo wanaweza kuwavutia hawa wanamuziki wanaokuja kuona ni katika upande upi wanaweza kuwekeza na sisi tukafaidika. Hata kwa upande huo huo wa Burudani kwa utajiri walionao wao hata wakiamua kuwekeza asilimia 10 tu ya pato lake hii itakuwa ni neema kubwa sana Taifa letu na watu watapata ajira. Kwani hawa watu hawaji peke yao mara nyingi wanakuja na menejiment nzima ikiwemo ma Meneja wao je hawaoni haja ya kufanya vitu kama hivyo?.

image

Umati wa mashabiki wakifurahia Serengeti Fiesta huko Moshi, Picha na Michuzi Jr.

Kwa Bodi ya Utalii, hii ni nafasi kwenye ya kuwafanya hawa watu wawe mabalozi wa hizi rasilimali zetu tulizonazo, kwa mtu kama Ludacris kwa nini asipewe ofa ya kutembelea mbuga za wanyama, tukamuonyeshe Simba kisha tumpige picha si kwa matangazo ila zisambazwe kama habari tu huyu ana mashabiki wangapi ambao hawajamuona Simba?  inawezekana kamuona lakini si kwenye mazingira asili, Kama tunajivunia Ngorongoro Crater ni moja ya maajabu ya dunia kwa nini tusimpeleke aende akayaone hayo maajabu? . Gharama ya kumpeleka Ludacris au mwanamuziki kama huyo Ngorongoro sio issue ya kuumiza kichwa kwa serikali kwani kwa gharama hizo hizo wapo maofisa ambao wanakwendaga huko ama na familia zao au na nyumba ndogo zao kupumzika kwa kutumia gharama za serikali … unabisha?….

Tunahitaji kuongeza idadi ya watalii na watalii tunaotaka waje sio hawa watalii uchwara ambao wanakula elfu kumi kwa siku, tunataka watalii ambao watakuja na umati wa watu na pesa zao kuja kupumzika na kutumia pesa zao. Sio kila siku viongozi wa Bodi ya utalii au TIC wanasafiri wao tu kuzunguza huku na kule ipo siku tutaomba kuona mafanikio ya ziara hizi we ngoja tuu.

Wanamuziki wanaongoza kwa “starehe” maana burudani ndio biashara yao, ni tofauti na wafanyabiashara au wafanyakazi ambao wao wanapata mapumziko mara chache, mfano kwa mfanya kazi mapumziko ni mara moja kwa mwaka ndio anapata likizo, lakini kwa wanamuziki au wacheza sinema anajipinda kwa kazi moja kisha anatulia kula matunda, hawa tungewalenga hawa wangeongeza pato la taifa na hata la watanzania baadhi yetu tiungefaidika pia.

Wakati kwa nchi kama Malaysia kwa mwaka 2009 iliingiza watalii 24 Millioni kwetu sisi tuliingiza watalii milioni 2 na kwetu tulijisifu kuwa tumeingiza watalii wengi zaidi, Malaysia kuna nini cha kutushinda sisi kwenye utalii?

Wizara na idara husika kaeni na hawa waandaaji muangalie mnawezaje kufanikisha hili.

Shime kwa bodi ya Utaliii watumieni hawa waandalizi angalieni jinsi gani mnaweza kushirikiana nao kwenye hili, nawasifu sana Clouds (Prime Times Promotion) ni wabunifu sana naimani mkikaa nao lazima watatoka na kitu hapo.

Mi nimesema tuu na nimtazamo wangu, na wengine walonge!!

Happy Birthday to Me!!

Advertisements

4 Responses to TIC na Bodi ya Utalii watumieni Ma Celebrities wanaokuja nchini

 1. Mgosi says:

  Kaka nimeipenda sana hii makala yako sana tu
  natamani wangekuwa wanapita humu na kusoma vitu kama hivi au kuwe na column ambayo itakuwa ikichambua yanayoongelewa kwenye blogs inaandikwa kwenye gazeti kama daily news au Guardian.

 2. Mwimba says:

  Hii ni changamoto kwa Serikali yetu kwakweli.

 3. Mdau UK says:

  Sio rahisi kihivyo mikataba inawabana lakini kama
  ulivosema labda iende kama offer kwake, Wazo zuri kaka.

 4. Its my fantastic pleasure to visit your web site and to take pleasure in your terrific posts right here. I like it a good deal. I can really feel that you just paid much interest for all those articles, as all of them make sense and are extremely beneficial.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: