Roga Roga Uso kwa Uso na Werrason

image

Kwa wafatiliaji wa Muziki wanaikumbuka Bendi ya Extra Musica hii ilitamba sana ikitokea huko Congo ya Brazaville lakini tambo zake hazikudumu sana, Bendi hii ilianzishwa mwaka 1993 huko Brazaville chini ya Kiongozi wake Roga Roga akishirikiana na Espe Bass ambao kwa pamoja wawili hao ndio walioanzisha Bendi hiyo kwa ajili ya kutoa burudani na kufariji waombolezaji wakati za misiba mjini Ouenze huko huko Brazaville.

Baadaye Kundi likaanza kukua baada ya nyimbo zao kukubalika na walianza kwa kukodisha vyombo mpaka ikawa bendi kamili.

Mwaka 95 kundi hili lilirekodi nyimbo sita katika albamu iliyojulikana kama Les Nouvelles Missiles yaani Kombora jipya. Takwimu zinasema kwamba mpaka kufikia mwaka 1996 jumla ya kopi 50,000 zilikuwa zimeshanunuliwa mbali na nyingine makumi kwa mamia ya kopi zilizosambazwa mitaani na walanguzi kwa njia za panya.

Kwa sasa Roga Roga bado anapiga muziki huko huko Brazaville na wiki hii ijumaa watatumbuiza jukwaa moja na Werrason Ngiama na Bendi yake ya Wenge Musica Maison Merre ambayo inamashabiki lukuki huko Brazaville.  Washabiki wa muziki wanasema Roga Roga ni mmoja wa wapiga Solo mahairi ambaye hajapata kutokea Brazavile huku wakimlinganisha na Allain Prince Makaba wa Wenge BCBG enzi hizo.

2 Responses to Roga Roga Uso kwa Uso na Werrason

  1. Farid wa Muscat says:

    Roga roga azaa asala bien haya ndio yalikua maneno ya Kila mbongo si uongo ni kweli kabisa pamoja na Alain Prince hawa wawili ndio wafalme wa SOLO GUITAR haijawahi kutokea na wala hakuna atakaewafikia kiwango chao aaaaaaaaaaaah mokili mobimba toyoka extra

  2. Hadj Le Jbnique says:

    Kweli kabisa kaka hakuna chembe ya shaka juu ya wasifu huo wa Le fondeteur Roga roga,yuko juu pia anajua sana kucheza miongoni mwa wapiga guitar,tena kwa kuongezea tu hata Le Rambow du zaire koffi olomide aliwahi kumnyatia sana amtie kundini QL,Sema aligonga mwamba kwa kuwa Roga roga asingeweza kuiacha Extra Musica yake,Espe Bass pia ni mkali ana vipaji vingi,anapiga bass,anatunga,anaimba,kiufupi hawa watoto walikua wamekamilika,karibu kila mtu alikua ana kipaji zaidi ya kimoja,kumbuka Roga roga pia anatunga,anapiga solo,anaimba na anacheza sana.Lakini tusisahau asili ya hii bendi ni vijana waliokua wanaipenda na kuifuatilia wenge na mwanzoni walianza kupiga kwa kukopi nyimbo za wenge na kuzipiga kwenye shows zao,ukifuatilia mwanzo walipotoa album ya kwanza utazikia sauti za werrason ikiimbwa na Guy guy,blaize bulla ikiimbwa na Espe Bass,solo key ya Alain Makaba ikipigwa na Roga roga e.t.c

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: