Etoile Du Berger “Nyota ya Jaha” ya JB Mpiana moto Pamba

Huwa ninasababu kwanini nampenda JB Mpiana aisee!! Ukiniuliza simply nitasema the guy can sing!! thats it. Papaa Jully Weston anasema JB Mpiana ana sauti zaidi ya sita na anaweza kuzitumia zote kwenye wimbo mmoja hicho kipaji wanacho wawili tuu JB Mpiana na Koffi Charles Olomide, pia ukimsikiliza Felix Wazekwa utakubali ana kipaji cha kipekee pia, hapa simlinganishi Wazekwa la hasha ila najaribu kusema tu kwa mtazamo wangu.

Sikiliza wimbo huu ambao hata Video Quality na Production yake iko bomba naweza kusema, sikiliza angalia then toa maoni yako usikurupuke ila sitokuzuia kusema chochote maana kuwa watu wanaushabiki wa Simba na Yanga hata kwa Muziki pia hahahahah, jumatatu Kareem.

Papaa Julie na Mamaa Punda Merci mingi sana!!

One Response to Etoile Du Berger “Nyota ya Jaha” ya JB Mpiana moto Pamba

  1. Hadj Le Jbnique says:

    Ama hakika JB ni King Of Congo Rhumba,wimbo mkali video bomba,ujumbe unaeleweka,nadhani kwa aliyeimbwa ni raha tupu kwake kuyasikia maneno anayoambiwa na jb hapa.

    Wimbo huu Jb amemtungia maalum binti wa rais wa Congo Brazzavile mzee Denis Sassou Nguesso aitwae Claudia,ndio maana wimbo huu huko Brazaa na sehemu nyingine wanauita Claudia,Hapo chini unaweza kumuona mwenyewe binti mrembo huyo mrembo ambae kama mtakumbuka dada yake ndio yule Edita Sassou Nguesso au Mamaa Bongo aliyekuwa first lady wa Gabon baada ya kuolewa na Rais wa Gabon marehemu mzee Omari Bongo,EDITA nae pia ni marehemu kwa sasa.Pia JB naona humo ndani amempa shavu kwa kumtaja pia mamaa WIVINE MOLEKA yule mwanamama mwanasiasa kijana wa congo tuliyewahi kumuona huko nyuma akimtebelea Footballer Tressor Mputu kwenye makazi yake.

    CLAUDIA SOSSOU huyu hapa

    http://www.claudia-sassou-nguesso.com/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: