Bin Hammam kukata rufaa ya Kufungiwa Maisha na FIFA

 

Na BBC Spoti

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika shughuli zozote za mchezo huo, aliyopewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.

Mohammed Bin Hammam

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohammed Bin Hammam

Bin Hammam ambaye anatoka Qatar, alipewa hukumu hiyo kufuatia tuhuma za kununua kura wakati wa uchaguzi wa urais wa FIFA ambao alikuwa mmoja wa wagombea wa kiti cha urais.

Katika mtandao wake, Bin Hammam, ametaja matukio ya hivi karibuni kama mapambano katika vita vinavyoendelea.

Vile vile amechapisha barua inayopongeza juhudi zake, katika shirikisho hilo iliyoandikwa mwaka wa 2008 na rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Chini ya barua hiyo kuna mstari unaosema “Hii ni mapambano na sio vita vyenyewe”.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: