Etoile Du Berger “Nyota ya Jaha” ya JB Mpiana moto Pamba

July 26, 2011

Huwa ninasababu kwanini nampenda JB Mpiana aisee!! Ukiniuliza simply nitasema the guy can sing!! thats it. Papaa Jully Weston anasema JB Mpiana ana sauti zaidi ya sita na anaweza kuzitumia zote kwenye wimbo mmoja hicho kipaji wanacho wawili tuu JB Mpiana na Koffi Charles Olomide, pia ukimsikiliza Felix Wazekwa utakubali ana kipaji cha kipekee pia, hapa simlinganishi Wazekwa la hasha ila najaribu kusema tu kwa mtazamo wangu.

Sikiliza wimbo huu ambao hata Video Quality na Production yake iko bomba naweza kusema, sikiliza angalia then toa maoni yako usikurupuke ila sitokuzuia kusema chochote maana kuwa watu wanaushabiki wa Simba na Yanga hata kwa Muziki pia hahahahah, jumatatu Kareem.

Papaa Julie na Mamaa Punda Merci mingi sana!!

Advertisements

Atlanta Bana Ba Congoo Bouro Mpela huyooooo!!

July 26, 2011

image

Anaitwa Geco Bouro Mpela ni mdogo wake na Allain Mpella aliyekuwa Wenge BCBG. Gecco alifanya kazi na Koffi Olomide na kung’aa sana utamsikia vizuri kwenye wimbo wa Inshallah wa Koffi yeye pamoja na Fally Ipupa.

Baada ya hapo yeye na kaka yake walitoa Albam ya pamoja iliyoitwa Mortal Combat, sio kazi rahisi sana kwa Congo kukubalika hata kama ulikuwa mzuri ndani ya Kundi hiyo imewatokea wengi wa Wanamuziki wa Congo kama Blaise Bulla, Adolf Dominguez, na wengineo ambao walitoka kwenye makundi ila hali haikuwa hivo kwa watu kama Ferre Gola, Fally Ipupa na wengineo ambao wao kidogo wamepata show nyingi za kitaifa na kimataifa, pia wameuza CD nyingi kutokana na kukubaliaka ndani na nje ya Congo.


WERRASON PLANETE SONO BEACH MAYI A PEMBE

July 26, 2011

Fikiria ingekuwaje kama Wazaire wangekuwa na Beach kama ya Coco au South Ceach au Kijiji Beach Kigamboni bata lake lingekuwaje?

Hii ni show ya Werasson ya Planet Sono Beach nimepata DVD yake asante sana Papaa jully Weston Presidaa Bana Congoo Daresalaame, Nimeipenda sana hii Live ya WMMM kama kawaida ninapotaka kuangalia Sebene na si kusikiliza nyimbo huwa namuangalia Werrason.

Kilichonivutia zaidi ni ile Djodjo Ngonda live kwa kweli imekumbusha sana enzi zile za Wenge BCBG, pale Heritier, Capuccino na Miel walivyokuwa wakiimba na kunogesha shughuli nzima.

Vyombo humo vilipigwa vyema na kiufasaha kama walivyokuwa wataalamu wenyewe Allain Prince Makaba kwa Solo, Fi-carre na Bukina Faso Kasongo kwenye Rhythim na Bass.

Ukiangalia vizuri utaona hawa vijana wanambeba sana Werrason na kwa sasa wanawashika mashabiki si kwa kuimba tuu bali hata cheza yao si mchezo.


Zambia wampiga mkwara FERRE GOLA

July 26, 2011

Mwanamuziki anayekimbiza kwenye kile kinachosemwa kizazi cha tano cha Muziki wa Congo Ferre Gola anatarajiwa kutua Lusaka Zambia kwa ajili ya Show yake tarehe 31 Mwezi huu (Jumapili).

Mashabiki wa muziki wa jijini Lusaka wameiambia Vibes D’Afrique kwamba mara ya mwisho Ferre alipotumbuiza Zambia mashabiki wengi walichukizwa na kitendo chake cha kutumia zaidi ya asilimia 90% ya muda wake jukwaani kupiga nyimbo zake za taratibu jambo ambalo Wazambia wengi hawakulifurahia. “…We have better slows done by our Zambian artists and we know congolese music as sebenes hence when we get too many slows, it just gets boring coz we dont understand the language!!!!.

Wazambia wanasema kuwa wanaijua Congo kwa Sebene zaidi kama ni miziki ya taratibu wao wanao wanamuziki wanaopiga miziki hiyo zaidi ya Ferre mwenyewe.

Tunataka vitu kama Vita Imana, Sans killo na sebene baada ya  sebene…….Chikito njikata!!!!!!!! alimalizia shabiki mweingine aliyeongea na mdau wangu Yemima

Hiyo Live ni ya Kinshasa Sono Beach pata kitu. Angalia jamaa wanavokula bata ki beach beach si muchezoooo Hii ni maalumu kwa Shabiki yangu Ally Tandika Le Fimitive Presidaa najua unampenda sana Ferre haya Lusaka panakuhusu kitu gani kaka!!!?.


Bin Hammam kukata rufaa ya Kufungiwa Maisha na FIFA

July 26, 2011

 

Na BBC Spoti

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika shughuli zozote za mchezo huo, aliyopewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.

Mohammed Bin Hammam

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohammed Bin Hammam

Bin Hammam ambaye anatoka Qatar, alipewa hukumu hiyo kufuatia tuhuma za kununua kura wakati wa uchaguzi wa urais wa FIFA ambao alikuwa mmoja wa wagombea wa kiti cha urais.

Katika mtandao wake, Bin Hammam, ametaja matukio ya hivi karibuni kama mapambano katika vita vinavyoendelea.

Vile vile amechapisha barua inayopongeza juhudi zake, katika shirikisho hilo iliyoandikwa mwaka wa 2008 na rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Chini ya barua hiyo kuna mstari unaosema “Hii ni mapambano na sio vita vyenyewe”.


Mbwembwe za kufunga kwa Kisigino zamgharimu Balotelli.

July 26, 2011

Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika mechi yao dhidi ya LA Galaxy kwa kutoonyesha heshima kwa wapinzani wake.

Mshambulizi huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 20 alikuwa karibu kufunga goli,lakini hakufunga na badala yake akapiga mpira kwa kisigino na kukosa kufunga.

image

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja akajibizana na kocha wake.

Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki ilomalizika kwa sare ya 1-1.

Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia.


ona Cheche za Mbwana Samatta na TP Mazembe

July 26, 2011

%d bloggers like this: