Tumkumbuke Defao

Leo tunakwenda angle tofauti kidogo,tunamzungumzia Genaral Defao Matumona na bendi yake ya Big Stars ambayo ilitesa sana katika ulimwengu wa muziki wa congo kwenye miaka ya tisini.Defao alianza kuimba mwanzoni mwa mwaka 1976 katika bendi za mitaani ndani ya kinshasa kama orchestre soka movema,fogo stars,korotoro n.k.Inasemekana alishawishika kupenda kuimba kutokana na uimbaji wa wakali wa zaiko langa langa wakati huo Papa wemba na Nyoka Longo,lakini mwenyewe amekuwa akikiri kwamba TABU LEY amekuwa main inspiration kwake.

Defao alianza kujulikana zaidi nje congo mwaka 1991alipoanzisha bendi yake ya BIG STARS Iliyokuja kuitijisa miji mikubwa ya africa kama Abidjan,Dar es salaam,Kinshasa,Oagadougou n.k.Hapa chini kwa mfano mtaweza kuiona video ya live concert Abidjan enzi hizo likiwa jiji la maraha kwelikweli kabla ya kukumbwa na machafuko ya kisiasa.

Hapo mwanzo ni THEO MBALA enzi hizo akiwa ndio yuko kwenye kiwango cha juu kabisa anamchezesha Chocholi chocholaa mcheza show mahiri wa big stars.Pia anawachezesha Defao na Kina Kabose anaeimba na kushikwa kichwa na defao,ilikua safi sana.
Hapa THEO MBALA anaendeleza vurugu zake

 

Hapa chini hizi ndio enzi defao hakamatiki

Shukrani za kipekee kwa Msomaji wangu Mwambungu wa Tunduma, Merci Mingi Papaa kwa habari zako tam tam, na wapenzi wote waomaji wa Blog ya Spoti Starehe nawatakia Weekend Njema.

7 Responses to Tumkumbuke Defao

 1. flower says:

  Asante sana kaka Pius,Kwa kutuwekea historia ya Defao.nawe tunakutakia weekend njema

 2. Farid wa Muscat says:

  Asante sana Papaa Pius na Mzee Mwambungu ,
  kabla ya miaka mitano nilimkuta Theo Mbala akiimba katika african club moja pale Dubai inaitwa (vendom plaza) ila hali yake ilikua taabani alikua anaonesha kua ameathirika na ulevi wa kupindukia ila alikua akichangamka tu pale anaponiona maana alikua anajua kua napenda sana pale anapoimba nalingi nakende na ngaa na mbuyimai,,,,mbuyimai kananga mamaaaaa mbuyimai kanangaa na na sijuii kwa sasa yupo wapi masikini, pale dubai alikuja kwa mwaliko wa Tino chaijaba

 3. Hadj Le Jbnique says:

  Defao & Les Big Stars at their very best 1990’s,aaah!those were the days bwana nayakumbuka sana maisha ya darisalama wakati huo TAZARA CLUB iko mbele,mlioko pande hizo msalimieni sana rafiki yangu HUSSEIN MACHENI,Alimpenda sana DEFAO.

  Hapo Defao alikua na watu wa kazi,kwenye uimbaji alikua na kina MONTANA KAMENGA,KABOSE na wakali wengine,BURKINAFASO MBOKA LIYA alipiga solo guitar,drums alikuwepo juju music,atalaku ndio Theo mbala,

  Album ya mwisho ya defao kufanya vizuri ilikua TREMBLEMENT DE TERRE 1999 ambayo ndio unapatikana huo wimbo diogene hapo juu tumeona video yake akimtaja Rambow Koffi Olomide na pia ndio album ya mwisho Theo Mbala kushirikiana na Defao ndio maana hata kwenye video hiyo haonekani Theo japo ndio aliefanya atalaku,alikuwa keshaachana na Defao wakati wa kufanya video.

  THEO MBALA alipotoka Big Stars alikaa kwa muda,ndipo baadae akajiunga na Les Anti Choc ya mzee Bozi Boziana,alieuliza yuko wapi basi anaweza kumpata hapa chini kwenye hii video hapo

  Melesi Mingi.

 4. Hadj Le Jbnique says:

  Hapa chini ndio GENERAL DEFAO wa NAIROBI,Sio wa KIN tena,kishakuwa mswahili,msikie mwenyewe anasema nini

 5. kazamoyo says:

  nimewakubali kweli

 6. inserzioni says:

  inserzioni…

  […]Tumkumbuke Defao « Spoti na Starehe[…]…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: