Husna atwaa taji la Miss Temeke.

GCG00001

Miss Temeke 2011 Husna Twalib (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Cynthia Kimasha (Kushoto) na mshindi wa tatu Mwajabu Juma mara baada ya kutangazwa matokeo.

MREMBO Husna Twalib ametwaa taji la Redd’s Miss Temeke 2011 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa TTC Chang’ombe usiku wa kuamkia jana.
Nafasi ya pili katika shindano hilo ilichukuliwa na Cinthia Kimasha aliyekuwa Miss Chang’ombe na ya tatu ilikwenda kwa Mwajabu Juma.

Husna anachukua nafasi ya Genevieve Mpangala aliyetwaa taji hilo mwaka jana na kufanya vizuri pia kwenye shindano la kitaifa, Miss Tanzania 2010. Shindano hilo lilisindikizwa na burudani kutoka bendi ya B Band ya msanii Banana Zorro na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa urembo.  Warembo 16 waliwania taji hilo katika shindano hilo la kwanza kufungua pazia kwa upande wa mashindano ya Kanda.

GCG00002

 

Warembo, walipita jukwaani na vazi la ubunifu, ufukweni na lile la jioni.

Husna ni mwanafunzi wa ngazi ya Cheti katika Chuo Cha Diplomasia jijini Dar Es Salaam akichukua Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa, awali alipoongea na Spoti Starehe Husna alisema nia yake ni kujiendelea kimasoma lakini bado ana mapenzi makubwa sana kwenye sekta ya ulimbwende na kusisitiza kuwa faraja anazopata kutoka kwenye familia hasa wazazi wake ndio zilizopelekea yeye kuingia kwenye shindano hilo.

Kabla ya kuanza kwa shindano hilo kulikuwa na tukio la ukataji keki ya kumpongeza muandaaji wa shindano hilo, Benny Kisaka aliyekuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Aidha mbali na hilo, kulikuwa na tuzo maalumu kwa wadau wa urembo waliochangia mafanikio ya Miss Temeke tangu kuanzishwa ambao ni kinywaji cha Redd’s, Vodacom, Times Radio na Clouds Fm ambapo tuzo hizo zilitolewa na wadau mbalimbali wa urembo.
Akizungumzia zaidi tuzo hizo siku hiyo Kisaka alisema kuwa zinalenga kuonesha ni kwa kiasi gani waandaaji wa shindano hilo wanatambua umuhimu wa wadhamini katika kuendeleza tasnia ya urembo.

One Response to Husna atwaa taji la Miss Temeke.

  1. You deserve a hug right now. You have brought up a very superb ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: