MBWANA SAMATTA AIFUNGIA TP MAZEMBE BAO LA USHINDI.

July 16, 2011
Na Aidan Leonce


MBWANA SAMATTA JEZI NAMBA 29 AKIFUNGA BAO PEKEE KWA KICHWA.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta juzi aliikoa timu yake ya Tp Mazembe na kuipa ushindi wa bao moja bila katika mchezo wa ligi . Samatta aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Serge Lofo alifunga bao hilo katika dakika ya 89 ya mchezo huo ambao kwake ulikuwa wa kwanza tangu ajiunge toka Simba Sports Club .
Sammatta aliingia kwenye mchezo huo sambamba na mwenzie waliyejiunga naye toka Simba Patrick Ochan ambaye naye alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza ambapo alichukua nafasi ya Rainford Kalaba aliyeumia dakika 15 baada ya mchezo kuanza . Tp Mazembe pia ilimkaribisha kiungo wake Guy Lusadisu aliyecheza mchezo wake wa kwanza tangu atoke kwenye adhabu ya kifungo cha FIFA baada ya kufanya fujo kwenye michuano ya kombe la Kagame huko Rwanda mwaka jana.
Hii ni mara ya tata kwa Samatta kufunga bao kwenye mchezo wake wa kwanza rasmi ambapo aliifungia Simba mabao mawili dhidi ya African Lyon ambayo ni timu yake ya zamani katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Simba kwenye ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita , pia aliifungia timu ya taifa ya wakubwa katika mchezo wake wa kwanza akitokea benchi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati na sasa ameifungia klabu yake mpya kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi.


Taifa Stars kukipiga Palestina, Jordan.

July 16, 2011

image

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) itakuwa na ziara ya mechi mbili nje ya nchi. Stars itacheza mechi ya kwanza Agosti 10 mwaka huu mjini Ramallah, Palestina dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo. Stars ambayo inatarajia kuondoka Agosti 7 mwaka huu kwa ajili ya ziara ya mechi hizo mbili, itacheza mechi ya pili Agosti 13 mwaka huu dhidi ya Jordan katika Jiji la Aman. Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen ambaye hivi sasa yuko likizo kwao Denmark anatarajia kutangaza kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya mechi hizo mara baada ya kurejea nchini mapema mwezi ujao.


%d bloggers like this: