Werrason ana raha yake bwana…

 

Huwa natofautiana na Mashabiki wangu wakisema namchukia Werrason, la hasha namkubali sana Werrason ila mapenzi yangu kwa JB Mpiana ni kwenye kuimba na mpangilio wa muziki, anyway tuyaache hayo.

Angalia Sebene na jinsi wadada walivyotupa Mambo Muone Bibicia Mfwengi kabla hajaondoka pia muone The Crocodile anavyokupa mambo ni balaa…

Video ya leo ni zawadi kwa Ma Werasonike wote, Richard Malewa, Rashid na Muzee wa Muscut na wasomaji wangu wote Ma Werrasonique, Weekend njema.

5 Responses to Werrason ana raha yake bwana…

 1. Anonymous says:

  Brother pius huyo aliyevaa Track ya blue na top yake anaitwa nani jina lake limenitoka kidogo,

 2. Mussa Khamsini says:

  Angalao mara moja moja na we unakubali Werasson ni kiboko.
  Mi nashangaa Werasson wenzangu kila kikiwekwa kitu cha Werasson hamsemi kitu mnakaa kimya wakiweka cha JB wote tunakimbilia kumkataa sisi ndio tunafanya JB aonekane yuko njema bana. chambueni na zetu kama hii mi naikubali sana.
  Mdau Sao Paul

  • Hadj Le Jbnique says:

   wanajua hawana cha kusema kuhusu werra,ushahidi uko wazi bora wewe umekua werrasonique wa kwanza kulitambua hilo,ndio mfahamu jb ni maarufu kuliko member wote wa wenge musica 4×4 Tout Terrain kaka wape hi!wana wote huko pele.pata kitu hapo chini mambo ya mpunda style ndani ya paris

 3. Farid wa Muscat says:

  Tunashkuru sana Papaa Pius kwa kutupa burudani safi kama hii
  si utani Mzee upo kileleni na wengine wanajikongoja tu ,ukisikia mtu kakupa tuhuma kua humpendi Werra basi ujue huyo fahamu yake ni ndogo sana katika muziki na hasa katika WENGE FAMILY, maana sisi wote wana wenge tunapendana kama na tofauti yetu ipo kwenye kile kitu mioyo yetu inapenda yaani nakusudia haiwezekani watu wote wakawa na mapenzi sawa katika kitu kimoja .
  balobi ngai naboyaa JB Mpiana ……..Naboyaateeee

 4. Hadj Le Jbnique says:

  wenyewe mnaona jamani 5 comments only so far more than five days…ingekua habari ya Salvatory De La Patria Mukulumba a.k.a.papaa na daida,papaa na suraya,papaa na junior JB MPIANA ungeona comments zinavyomiminika hapa,yote hiyo ni kutokana na kwamba jb ana mvuto mpaka kwa haters wake……..wanajifanya hawamkubali hadharani lakini kimoyo moyo wanampenda sema tu wengi wana hasira kwa kuwa alijitoa wenge musica original akiwaachia waanzilishi wake waendelee yeye akaanzisha bendi kitendo kilichofuta ubabe wa wenge musica ndani ya kinshasa na dunia nzima,ndio wengine wanahasira nae mpaka leo japo wanampenda,lakini hakua na jinsi kwani waanzilishi walianza kumuandama baada ya kuona anapendwa zaidi na kuwafunika wao……akaamua kuwaachia bendi yao wenge musica lakini kuondoka kwake kuliitisa wenge zaidi katka historia ya maisha yake licha ya kuwa ilishawahi kukimbiwa na wanamuziki wake wengine hapo kabla tena si wakuja bali walikua wanzilishi kina Aime buanga na Jean Marie paul waliokwenda kuanzisha wenge el paris na wenge kumbela..hata sijui kama bado zipo hizi bendi.Huyo ndio mpiana tshituka mwana congo binadam.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: