TWIGA STARS YAPANGWA KUNDI B MICHEZO YA AFRIKA (ALL AFRICA GAMES)

 

Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars) imepangwa kundi B katika Michezo ya Afrika (All Africa Games). Michezo hiyo ya Kumi itafanyika kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu jijini Maputo, Msumbiji. Upangaji makundi kwa ajili ya michezo hiyo kwa upande wa wanawake na wanaume ulifanywa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Hicham El Amran. Rais wa CAF, Issa Hayatou pia alishuhudia upangaji huo wa makundi uliofanyika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri wakiwemo pia wawakilishi wa timu zilizofuzu kwa ajili ya michezo hiyo.

Twiga Stars imepangwa pamoja na timu za Afrika Kusini, Zimbabwe na Ghana. Kundi A lina wenyeji Msumbiji, Cameroon, Algeria na Guinea. Mabingwa wa mwaka 2007 Nigeria wameshindwa kufuzu kwa ajili ya michuano ya mwaka huu. Wiki iliyopita Twiga Stars ilikuwa Harare, Zimbabwe kwenye mashindano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA). Ilishika nafasi ya tatu ambapo ilicheza na Zimbabwe na Afrika Kusini.

Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ ndiyo walioibuka mabingwa wakati Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’ ilikuwa makamu bingwa. Twiga Stars inayofundishwa na Charles Mkwasa akisaidiwa na Nasra Mohamed inatarajia kuingia kambini mwezi mmoja kabla ya kuanza michuano hiyo inayoshirikisha timu nane. Kwa upande wa wanaume kundi A lina wenyeji Msumbiji, Afrika Kusini, Libya na Madagascar wakati kundi B ni Cameroon, Uganda, Ghana na Senegal.

Advertisements

One Response to TWIGA STARS YAPANGWA KUNDI B MICHEZO YA AFRIKA (ALL AFRICA GAMES)

  1. Appreciating the dedication you put into your blog and in depth information you present. It’s awesome to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Great read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: