Arsenal kukipiga na Malaysia All Stars mchana huu jijini Kuala Lumpur

image

Pichani Kocha wa Timu ya Taifa ya Malaysia alimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Malaysia kocha Arsene Wenger wa klabu ya Arsenal.

Klabu ya Arsenal ambayo iko ziarani huko Asia leo inacheza na timu ya Kombaini ya Malaysia ikijumuisha wachezaji wa timu ya Taifa na Ma Star wote wa Malaysia, mchezo ambao unatazamiwa kuanza saa mbili na dakika 45 usiku sana saa tisa alasili ya Afrika MAshariki.

Timu nyingi za Uingereza zimekuwa zikifanya ziara katika bara la Asia hasa kwenye zile nchi zilizoimarika kiuchumi katika kuhasasisha mchezo wa mpira wa miguu lakini pia kwa malengo ya kibiashara zaidi, mathalani Arsenal wamekuwa na na Training Camp mjini Malaysia ambapo wana academy ya kufundisha watoto wadogo sio hivyo tuu bali pia kujiongezea mashabiki ambapo wanauza sana vifaa vya michezo.

Tarehe 22 klabu nyingine toka Uingereza ya Chelsea wanatazamiwa kukipiga na Malaysia Kombaini katika uwanja wa Burkit Jaril ambao unauwezo wa kuchukua watazamani 100,000. Kwa mujibu wa waandaji wa mchezo huo Pro Events Management wanasema tiketi kwa ajili ya mchezo huo zinauzwa kati ya Malaysia Ringit RM58 (Tsh, 30,000), RM68 (Tsh.35,229),RM108 (Tsh 55,953.42) na RM388 (Tsh. 200,000). kwa VIP One.

Wakati huo huo mchezaji wa Arsenal Jack Wilshere amemtaka mchezaji mwenzake Cesc Fabregas kuonyesha ukomavu na kutoa maamuzi ya kubaki Arsenal ili kuufunga mjadala wa kuhama kwake timu ya Arsenal.

image

Wilshere

Kwa takriban wiki tatu sasa jina la Fabregas limekuwa likitawala vyombo vya habari kuhusiana na kutakiwa na klabu ya Klabu ya Barcelona, Awali kocha wa Arsenal Arsenal Wenger alisema kuwa Fabregas kwa sasa yuko njia panda na bado hajaamua kama atabaki ama kwenda kwenye klabu hiyo ambayo mwenyewe amekiri ni moja ya vilabu anavyovipenda.

Wilshere aliyasema hayo alipoongea na vyombo vya habari huko Malaysia ambako timu ya Arsenal iko Ziarani, “Fabregas lazima aonyeshe uaminifu/Utiifu kwa klabu ya Arsenal, hapo ndio ataonyesha uanamume wake na ukomavu wake pia…” alisema Wilshere.

One Response to Arsenal kukipiga na Malaysia All Stars mchana huu jijini Kuala Lumpur

  1. Relatively particular he will have a excellent study. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: