Pole mdau….Hiyo ndio YANGA….ukiona manyoya jua mnyama kaliwa

July 11, 2011

image

Mdau na mnazi wa Simba Mudy Wandy akiwa uwanjani akishuhudia mnyama alivyochemka kuitafuna kandambili, Hii ilikuwa kipindi cha kwanza kabla ya matokeo na mashabiki wa Simba kama kawaida walikuwa na matumaini makubwa Simba ingeshinda.

Mpaka mwisho Yanga 1-0 Simba.

Poleni sana wadau wa Simba, Muddy Wandy, Mngoya, Alhaj Hakam, Robert Mwafrika, Uncle Dee, Dulla aka Asumani na wenzenu wooote ndio mpira na moto wa jangwani hauzimiki. teh teh teh teh!!

image

Picha hii ilipigwa na rafiki yangu Bakari Machumu ikionyesha uzalendo kwa watani wa jadi na kumaanisha kuwa mpira si ugomvi!!


Ni Yangaaaaa!!

July 11, 2011

Yanga ya Dsm jana ilifanikiwa kulitwaa kombe la Kagame ( Cecafa) baada ya kuifunga Simba Sports Club bao moja nila 1-0 katika Fainali ya kusisimua ilichezwa uwanja wa Taifa Dsm.
Mbele ya mashabiki 60,000 Yanga waliwapa raha mashsbiki wao huku timu zote zikionyesha mchezo wa hali ya juu.
Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye kusisimua kila aliyekwenda uwanjani alifurahi.
Mashabiki wa Yanga walimbeba juu kocha wao Timbe ambaye ameweka Rekodi ya kuchukua Kombe hilo mara nne akiwa na timu nne tofauti zikiwemo APR ya Rwanda, Polisi Uganda na Yanga.

20110711-073524.jpg


%d bloggers like this: