Proces Mambika utunzi wa Alain Mpela

 

Ingawa wengi wa mashabiki na wapinzani wa JB Mpiana wanasema kuwa tangu Album ya Feaux De La Mour JB Mpiana hajawahi kutoa album nyingine nzuri tena, pia wanadai JB Mpiana anawabana sana wanamuziki wake.

Kwangu mimi ukiniuliza ni album gani ambayo naweza isikiliza mwanzo mwisho nitakwambia Titanic chini ya Engineer Blaise Bulla, kiukweli niliipenda sana hii Album na jinsi jamaa walivuyojipanga na kama unafatilia utaona kila aliyekuwemo kwenye kundi alipata nafasi ya kutunda na kuimba.

Sikiliza jinsi Allain Mpela, Aimelia Liese Domingongo walivyokuwa wakijibizana humu, msikilize Aimelia mwenyewe alivyoingarisha kwa sauti yake nyororo (yuko wapi tangu aende kwa Werra?? umemsikia wapi?).

Kisha msikie Sele Bulla Engineer alivyochombeza na mwisho kabisa msikilize Tutu Caludji alivyoghani humu. Mnyonge tumnyonge lakini haki yake apewe arrangement ya muziki JB Mpiana yuko juuu baabake.

Hili ni ombi la Le Fimitive Julie Weston Baba Bee my die hard fun wa blog hii, na kwenu ma Beeceebeegeeque wooote.

Wiki ijayo nitawaletea historia na interview ya Le Phenomenon, The King of the Forest Werrason Ngiama Makanda so stay tuned kujua ni nani alizaliwa wapi, anaishije, nini msimamo wake kuhusu misuguano ya mashabiki, maono yake juu ya Muziki wa Congo.

13 Responses to Proces Mambika utunzi wa Alain Mpela

 1. Hadj Le Jbnique says:

  …..TANGO BANGO BAKOLOBAKA MUTO AKOKENDE……TANGO BANGO BAKOLOBAKA AFANDE AKONANA…….HAI NZAMBE….IGETE MBOMA BIBI NA MBOTO PRINCESSE,

  AAAH ACHENI JB AITWE MUKUBWA JAMANI MNYONGE ANYONGWE LAKINI HAKI YAKE AIPATE,HAPO CHINI NI VIDEO YA PROCES MAMBIKA LIVE ON STAGE NDANI YA OLYMPIA PARIS 1999 SIKU CHACHE BAADA YA KURELEASE ALBUM YA TITANIC,HUMU UTAWAONA WALE WAMAMA WA NGUVU WAMAMA WA KILO WENYE PESA CHAFU AMBAO TUMEKUWA TUKIWASIKIA WAKITAJWATAJWA KWENYE NYIMBO ZA WATOTO WA CONGO,HAPO MWANZO MTAMUONA JB ANAMTAJA IGETE MBOMA,NAE ANAPANDA JUKWAANI NA KUMKUMBATIA JB,PIA MTAMUONA MAREHEMU MAMAA MERE MALOU MADAME YA POTO AKIPANDA STEJINI AKIWA AMEVAA NGUO YA KIJANI NA KOFIA YAKE,MAMAA MEREVEE BEBE AKUJI NAE PIA ANAONEKANA HUMU PAMOJA NA WAMAMA WENGINE WENGI TU
  MWISHO WA VIDEO NDIO KWENYE UTAMU ZAIDI,KUNA WATOTO WATAPANDA JUKWAANI,WATAMWAGA NDOMBOLO LA KUFA MTU NA KUWATOA NISHAI BANA BCBG WOTE AKIWEMO JB,PATA VIDEO,UKIWA NA SPEAKER UTAENJOY ZAIDI.MERCI

 2. Juma BCBG says:

  Wakati mwingine naumia sana nikiwazaga hawa jamaa waliparanganyika, simlaumu JB Mpiana wala werason lakini inaweza ikawa wao ndio wamesababisha matatizo yote haya. leo hii sisi humu tunabishana na kutupiana maneno wao wanaingiza fwedha tuvumiliane tu jamani.
  Kaka Pius naipenda Blog yako kwa habari hizi za Congo unanikunaga sana kakaka

 3. Farid wa Muscat says:

  wazimu ulinipata baada ya kushuka album hii na hasa Tutu Caludji ndie alieifanya hasa nyimbo zote zikawa bomba sana mpaka leo mimi hua sichoki kabisa kuisikiliza .
  asante sana Mzee Pius kwa kutukumbusha starehe kama hii

 4. flower says:

  Kaka Pius,naomba nitoke nje ya mada kidogo.Mie nilikuwa napenda na bado nazipenda nyimbo za Defao ingawa cjui zina maana gani.Hivi huyu Bwana yupo wapi?na je bado anajishughulisha na muziki?wimbo wake ambayo nlikuwa naupenda sana ni :Papa Pona nini okimi ndako”hata ukicheck profile ya fb yangu leo nimeuweka naomba unitafsirie walau kidogo nijue una maana gani.Natanguliza shukrani.Weekend njema

  • Farid wa Muscat says:

   mimi mwenzako umenikumbusha aliekua anaipendezesha band ya defao sana na esi mwingine ni THEO MBALA sijui kwa sasa yupo wapi? napenda pale alipokua akiimba (nalingi nakende na nga na mbuyimai eeeh mbuyimai kananga maamaa.

   • Hadj Le Jbnique says:

    THEO MBALA ALIPOTOKA BIG STARS YA GENERAL DEFAO ALIPUMZIKA KIDOGO,AKAMSAIDIA AIMELIA KATIKA SOLO PROJECT YAKE “CONSTANT” AMBAYO WENGINE WANAIITA GENERATION WENGEE,THEO ALIFANYA ATALAKU HUMO NI ALBUM NZURI TU,THEN BAADA YA HAPO THEO MBALA AKAJIUNGA LES ANTI CHOC YA MZEE BOZI BOZIANA,WALIKUA YEYE PAMOJA NA KABOSE AMBAE SASA YUKO NA BENDI YAKE,TAFUTA CD ZA BOZI BOZIANA UTAMUONA THEO MBALA AKIENDELEZA VURUGU ZAKE

  • Shaibu Thabit Mwambungu from Tanzania,Mbinga-Ruvuma says:

   Defao kwa sasa anaishi Nairobi. Papa ye Po nini okimi ndako ye = Baba e kwanini unaikimbia nyumba Okimi ndako nayo= unakimbia nyumba ,Zonga ndako tobongisa malembe= Rudi nyumbani tumalize taratibu kuna hako kaujumbe baba ametelekeza familia kutekeleza majukumu yake kwa watoto chakula ,shule kwa watoto. Mdau mwambungu mbinga

 5. Hadj Le Jbnique says:

  Defao kwa sasa anaishi nairobi kenya.

 6. le shakespear du tanzanie says:

  jb mpiana yuko juuuuu… TSHA MUNTU TSHA MUNTU??? VIDEO NZURI SANA HIIII INANIKUMBUSHA MBALI SANA

 7. Hadj Le Jbnique says:

  THEO MBALA AKIWA NA BOZI BOZIANA HUYU HAPA

 8. joseph lembo says:

  Jb Mpiana yuko juu hata mm nisikilizapo nyimbo zake napata burudani kubya kama wimbo wake wa essau da mkuu kachana kinoma na anaonyesha ni jinsi gani ambavyo hana kinyongo moyoni mwake na ninaupenda sana

 9. Cora Downy says:

  Quite good weblog and exceptional and articles.beneficial style and design, as share superior stuff with good concepts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: