JB Mpiana Chiboko bwana, hii ni show ya Jumamosi majuzi!!

Na The Romantic

Bila ubishi JB Mpiana kwa sasa ndio mwanamuziki anaeongoza kwa kujaza watu kwenye show zake za kulipia (sio za bure)ndani ya Congo.Hilo limedhihirika juzi jumamosi iliyopita huko kisangani ambako kama mtakumbuka werrason alipeleka mambo yake huko.Sasa basi hiyo jumamosi JB alivamia anga hizo si kwa nia ya kupeleka mambo kama werrason bali yeye alikwenda huko kisangani na ujumbe mzito,aliwaambia maneno haya “BANA CONGO MOBIMBA TOLINGANAAAAA..JB MPIANA ET WERRASON TOLINGANAAA…DIDIER MASELA ALAIN MAKABA……Sikiliza 7:13 Alipoimba JB Mpiana 7:37 alipomtaja Werasson mashabiki walishangilia sana na wanamuziki wote waliondoka Wenge akiwahimiza wapendane na washabiki wote walikuwa wakiimba naye wimbo ule mtamu wa Essau.

Hapa JB anawahimiza watoto wote wa congo kupendana na kuacha kuchukiana bila sababu,anatoa mfano wa yeye na wanabendi wenzake wa zamani wawe na upendo kwani bado wako wa ndugu ila kikazi tu ndio wanatofautiana,watu walifurahi sana hasa alipomtaja werrason,wachambuzi wa mambo wanamuona JB licha ya kuwa ni mdogo kiumri ukimlinganisha na Werra kichwa chake kimejaaa akili na busara nyingi.Angalia mwenyewe video ya show hiyo iliyodhaminiwa na PRIMUS ilivyokua…..

54 Responses to JB Mpiana Chiboko bwana, hii ni show ya Jumamosi majuzi!!

 1. Stivin says:

  JB na Werra wamepishana mwaka mmoja! kichwa cha JB kingekuwa kimejaa busara asingekuwa na ubinafsi, ubinafsi wake uliuwa Wenge!

  • POLEPOLE NDIO MWENDO says:

   Werrason alizaliwa 1965,Jb Mpiana alizaliwa 1967.

  • jully weston ilunga says:

   kaka jb hana ubinafsi unakosea sana naomba fwatilia sana story kwa ukaribu,kama jb aliuwa wenge sasa n’giama waliomsaidia kuinua wenge maison mere waka wapi?naongelea DIDIE MASELA,ADOLPH DOMINGUEZ,FERRE GOLA,BILL CLITON,DIDIER LA COSTE,J DE T MULOPWE wako wapi hawa watu na wali chukua muda gani karibu naye????nakumbuka tena AIMELIA LIAS alikimbia kwa jb kwenda kwa N’GIAMA alikiona cha moto.

 2. Stivin says:

  Umejiuliza kwa nini alipomtaja Werra uwanja mzima ulizizima?

 3. Richard Malewa says:

  Tolingana huu msamiati ulifutika kwenye kichwa cha Panzi cha JB MPiana moto umemchoma miaka kumi Sifuri tupu leo eti Tolingana Tolingana. Mbona hakutaka kushiriki kwenye ile show ya Wenge Re Union. Manguli wote walikuwapo kasoro yeye!

  kama ni Tolingana ni heri yule ambaye ni Balozi wa Amani anayetambuliwa na UNICEF Le Roy De Forret, Le Phenomena, Le le le lee leeee leeeeee leeeeeeeeeeeeee! Dunia inajua hata Afrika inajua.

  • Hadj Le Jbnique says:

   hii ndio show anayoizungumzia Rich,je ilifana bila jb

   • Hadj Le Jbnique says:

    Haya ndio yalikua mazoezi waliyokuwa wakiyafanya kabla ya show hiyo,hapa nimefurahishwa na Alain Prince Makaba jinsi alivyokuwa kibonge siku hizi,adolphe big tata yeye kama kawa full tumbo

   • Anonymous says:

    Kama wewe ni mnazi wa JB utaona haikufana!

  • jully weston ilunga says:

   kaka werra anaongoza sasa hivi congo kwa kuto helewana na wana mziki wenzake mfano,yeye na koffi anasema foffi mbaya ok ye na papa wemba hivyo hivyo ye na ferre yale yale,ye adolph yale yale,yena chala mwana yale yale,ye na bill cliton ndo usi seme kabisa sitaki kumtaji jb,mtu peke yake wana elewana naye ni felix wazekwa upo?

   • piusmickys says:

    Haya watu wa Werason hawayaoni kila siku wanamsema JB tuu, Huyu Papaa Julie Weston Ilunga anatoka Congo na ni Mcongoman ambaye anapenda mzuki sana si mshabiki wa JB lakini anasema ukweli Papa Julie ni mshabiki mkubwa wa Koffi na akina Ferre na Fally lakini anaupenda muziki wa Wenge kwa ujumla.
    Tuendeleee

   • Hadj Le Jbnique says:

    umesema vizuri sana,chukua zawadi hii,najua wewe ni mtu wa muziki hivyo hata kama haina video utaifurahia,msikilize kila mtu hapo alivyofanya kazi yake,kuanzia jb ambae ndio alitunga hiki kitu willy mutu,werra de la forret then usikilize vidole vinavyozungumza vya prince makaba

    watch?v=CHkX9GmMdRc&playnext=1&list=PLDBF2CFE1F31ED109

   • Hadj Le Jbnique says:

    umesema vizuri sana kaka chukua zawadi hii toka kwangu,hapa kwa kuwa wewe unaonekana ni mtu wa muziki naamini utafurahia japo hamna video,nataka uwasikilize kwa makini wote kuanzia jb ambae ndio mwenye wimbo,werra de la forret na mwisho usikie vidole vya alain prince makaba,i luv this song

 4. Sissy HKM says:

  Huyu si ndiyo yule alikuwa anajifanya nguli eti “Tsha Muntu Tsha Muntu” leo eti anataka apendwe kwa kipi alicho nacho heeee Kafulia Babuuu! na jasho la pual litakutoka mwaka huu! Tolingana?!

  • jully weston ilunga says:

   kaka unaelewa vibaya tsha muntu cha muntu tsha nzambi tsha nzambi,akisema tolinga ni sawa kwa nini kuchukiana?werra mpaka sasa hivi anatafuta staili ya kuingiza album yake kona zote mpunda imeshika kaka soyon serieux, uezi kua na wakwe zako ukafuraia wacheze mziki kama leleleeeeeee hiyo inafaa ma chokora na ma chege pole.

 5. Stivin says:

  Halafu watu wenyewe kiduchu! Hivi unaangaliaga show za Werra lakini? Mpiana saizi yake ni Dominguez na Blaise Bula, Mshindani wa Werra labda Koffi!

  • mukulumba says:

   Werra na koffi si washindani kaka wale ni wapinzani……..watu hata kushikana mikono wanaogopana….ule ni upinzani wa kitoto wa werra

  • jully weston ilunga says:

   hahahaaaaaaa kaka pole pole tena sana geuza maneno yako soit serieux.

 6. Farid wa Muscat says:

  JB nampenda na Werrasone nampenda zaidi lakini nahisi kama Mpiana ndie sababu kubwa ya kuvunjika kwa starehe yetu ya 4×4 na sababu ni kujali manufaa yake zaidi ya wenzake , na kila siku anazidi kupoteza washabiki na khasara kubwa aliipata ni pale alivyonipoteza mimi yaani nimebaki nasikiliza sauti yake katika nyimbo za zamani tu ila kwa siku hizi sina time nae maana hana kivutio chochote, ila kwa Werra nahisi anakwenda na wakati na anatoa ile kitu watu wanataka (miziki tolingi na motema) .

  • POLEPOLE NDIO MWENDO says:

   Sasa jamani tuwe wakweli tuache kumchukia tu mtu kwa kufuata mkumbo…Farid ni mashabiki wepi hasa unaowataka wewe zaidi ya hao hapo kisangani?yani unamchukia mtu mpaka kila mtu anajua,chuki binafsi haifai tuwe washabiki wa muziki wakweli zaidi kuliko kuwa washabiki wa werrason tuuuu basi

  • jully weston ilunga says:

   farid mi nazani ni kwa sababu auna habari kamili za huyo papa cherie,akuna mwana mziki ana uwezo wa kukaa myaka yote aliokaa bila kutoa album lakini anajaza watu, mfano mwaka juzi alikuja dar ulizia shoo ilikua je?mimi naona bora upungue wewe usio jua mziki waongezeka wanao jua mziki

 7. piusmickys says:

  Aaah jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Bado JB anabaki kuwa mwanamuziki nambari One kwangu, sitakiwi kuwa na uapande lakini kuna mahalla dah inauma kumuona The Charismatique Leader akizodolewa kiasi hiki!! Bravooo JB uko juu Papa Cheriii

 8. POLEPOLE NDIO MWENDO says:

  Wachambuzi wa mambo ya muziki wanasema Le Roi De La Forret werrason sio muimbaji mzuri ukimlinganisha na JB,KOFFI,MZEE PAPA WEMBA,WAZEKWA,FERRE,FALLY na Hata Blaize Bulla.Katika kulitetea hilo wamekuwa wakijenga hoja kwamba muimbaji mzuri huwezi kumjudge kwa kuzisikiliza C.D. za album zilizokwisha pikwa studio kwa kuwa hiyo inakuwa ni kazi iliyotayarishwa kwa miezi kadhaa studio kabla ya kuletwa sokoni,inakuwa imechujwa.Wanadai muimbaji mzuri anapimwa kwa jinsi anavyoperform anapoimba live on stage kwenye concerts au kwenye interview.Ili kujiridhiridhisha si vibaya na sisi humu kila mmoja at your own time jaribu kutafuta cds za concert live au interviews za JB,WERRA,WEMBA,KOFFI,AWILO n.k tuzitazame kwa makini jinsi wanavyoimba live,Then tu judge.

  Pia wachambuzi hao wamekua wakimchallenge werra kwamba amekua akiforce kuimba sauti isiyo yake,hapo wanadai ndio amekua akiharibu mambo kabisa,wanasema yeye sauti yake ni natural bass lakini sometimes amekua akiforce kuimba kwenye high notes,na hii imekuwa ikiwakumba wanamuziki wengi wenye sauti nzito wanapokuwa viongozi au wamiliki wa bendi mfano King Kester au mzee Bozii Boziana nao wamekuwa na tatizo la kuforce kuimba kwenye high tones wakati hawana uwezo huo,hivyo wamekua wakipunguza radha ama kuharibu kabisa muziki wao.Hawa wanatakiwa kustick kwenye natural bass kwa kuwa ndipo uwezo wao unapoishia.

  MAWERASONIQUE MNALIZUNGUMZIAJE HILI MUWE FAIR KATIKA KUTOA MAONI MSISUKUMWE NA JAZBA NA USHABIKI KUPITA KIASI.

  • Farid wa Muscat says:

   Polepole mimi nahisi huo ni mtazamo wako zaidi maana unawatuhumu watu kua wanamchukia JB kumbe wewe ndio mwenye chuki nambari one dhidi ya Werrasone, hio sio fair kabisa hebu punguza mwendo ili uendane na jina lako usije ukajikwaa bure, sasa mimi nakwambia katika family ya wenge 4×4 kila mmoja ana sauti yake ya pekee na wako wengine wenye uwezo wa kuimba sauti tofauti zaidi ya 1 au 2 au 3 na wengine zaidi kwa hio huwezi kusema kua fulani sauti yake ni nzuri kushinda fulani hapo utakua unaleta ubaguzi wa hali ya juu ilimradi umlet down mwimbaji usiempenda , sasa mimi nakwambia sisi tunawapenda wote kwa sauti zao , hebu chukua zawadi hii ya suprisse kapangala http://www.youtube.com/watch?v=DP8NPqA9Abc
   na ukipenda nyongeza sikiliza chantal swizerland nina uhakika utafurahi.

   • Hadj Le Jbnique says:

    Ungekuwa unawapenda wote usingethubutu kusema show hiyo ya jb kisangani iliukua na watu kiduchu…..ni hilo tu nilitaka kuliweka sawa,otherwise fuatilieni sawasawa alichotukumbusha mdau polepole hapo juu,ni vema watu wakaimba kwa sauti zao,kama huwezi kuimba sauti ya kwanza dont force,unaharibu kazi wakati kipaji unacho….salamu kwa werra na mzee bozi boziana hizi huo ni ujumbe wao

  • jully weston ilunga says:

   hiyo ni kweli kabisa sijaona werra kuimba wimbo kwanzia mwanzo mpaka mwisho bila msada wa heritier au mtu mwingini lakini souverain leader jb mpiana papa cheri moto pamba anaweza kuna kitu kama omba,jeannette feu de l’amour,ezau………., mopao mokonzi le quadra kora man pap na didi stone naye ndo zake anakuja na kitu kama aspirine,ninele,coucou,alia………… mwanzo hadi mwisho wanaimba wenyeu

 9. POLEPOLE NDIO MWENDO says:

  BORA MIMI SIJASEMA……..

 10. Hadj Le Jbnique says:

  Pole Pole umenigusa sana umenifanya nikose cha kusema

 11. Anonymous says:

  mata na mpunda, jb mpiana ni mwisho wa matatizo na ni mwimbaji mzuri sana kuliko wera son ila lazima wote tukubali kwamba ana tatizo la ubinafsi na yeye ndiye aliyesababisha wenge bcbg igawanyike lile kundi lilikuwa mwisho wa matatizo, mimi nawapenda wote na nawasikiliza wote ila lingala sifahamu kama kuna sehemu hapa dar wanafundisha naomba mnielekeze nikajifunze ninatalipia pia kwa hilo.

  • Farid wa Muscat says:

   sijui kama uliwahi kusikiliza album ya ndombolo ya solo ? na kama uliwahi kusikiliza je unaweza ukatambua majina ya waimbaji wote walioshiriki kwenye nyimbo zote pamoja na wapigaji? halafu nenda katizame cover ya cassete ili uweze ujue maana ya ubinafsi ni nini.

   • Hadj Le Jbnique says:

    Naona sasa unachanganya mambo,album ya Feux d’amour unayoiita ndombolo ya solo haikua album ya kundi kama vile ilivyokua pentagon ambayo kila mtu alicompose song mle ndani,hii ilikua ni project binafsi ya JB hivyo alikua na uhuru wa kupanga nani aimbe nini kwenye nyimbo zote zilizokuwemo mle ndani ambazo alizitunga peke yake,ndio maana ukaona kulikua na vocal za papa wemba hakuwahi kupigia wenge,huyo werra pia nae alitia vocal kwenye wimbo mmoja na wengine wote alijaribu kuwapa shavu angalau kwenye nyimbo moja mle ndani,kasoro tutu kaludji ndio alifanya animation katika nyimbo zote hata le grand chibuta roberto ekokota alipata nafasi kwenye wimbo mmoja tu nadhani,so ile album msiililie sana kwa kuwa ilikua ni solo album ya jb kama ilivyokuwa new image ya prince makaba ambayo hatuwasikii mawerasonique mkiililia kwanini Feux d’amour ambayo werra alipewa mistari miwili tu kuimba ambayo ilitungwa na jb pia?Kilichoiua wenge ni wivu wa kike wa werra na genge lake baada ya kuona jb katengeneza album nzuri nyimbo zote katunga yeye na imeuza kupita album zote za kundi,ndio wakaanzisha chokochoko eti za kumpindua jb kwenye uongozi,ndio jb akaona upuuzi akasema mi najitoa wenge musica head office naanzisha tawi langu kuwapisha mpate uongozi,anaetaka kuja kwangu ruksa asiyetaka abaki head office lakini wote tutabaki kuwa wenge,cha ajabu sasa wanamuziki wengi hawakutaka kubaki head office wakamfuata jb,ndipo ikawa ianaonekana kama vile werra na genge lake ndio waliojiondoa….lakini ukweli ni jb ndio aliamua kuwapisha waanzilishi wa wenge maana walikua wakimsimanga kwamba yeye si muanzilishi bali alikuja tu….habari ndio hiyo kwa msioijua
    kwanini kwanini Werra anaiita hiyo yenu ni Wenge MMM

   • jully weston ilunga says:

    hahaha farid sizani kama unaelewa unacho sema kwanza jb ajawai kutoa album inaitwa ndombolo inaitwa feu de l’amou hilo ni la kwanza pili ni album yake binafsi siyo ya band awezi kuweka kila aliemba kwenye cover itajaa nakumbuka ameshirikisha hadi papa wemba kwenye hiyo album angalia kwenye cd orginal kuna ma dina ya kila alieshiriki na ana wa shukuru hote walieimba naye,mbona sijawai kuona mwana mziki ameweka picha ya watu wingini kwenye cover ya album yake binafsi labda hiwe ya band,najua uezi kuelewa kwa sababu una fwatilia sana werra jua ajawai kutoa album yake mwenyewe.

  • Hadj Le Jbnique says:

   to leave, to go -kende
   to go rotten -polo
   to go up by car -komata na motuka
   I want to go to the market – Nalingi kokende na zando

  • jully weston ilunga says:

   jamani aliesababisha wenge bcbg igawanike ni papa wemba sio jb,kwanza ilikua jb asimamishwa kazi,werra na wenzake waliitisha kikao cha band ilikua kwenye kikao wamusimasha kazi, jb kwa kua alikua ametoka kutoa album yake ya feu de la mour alikua na hela akawambia kama mna n simamisha bila sababu mimi naenda kwanzisha band yangu najitoa,hapo hapo alisimama kwenye kikao nakuondoka blaise bula akasema mimi namfwata souverain,aimelia ,tutu kaluji alain mpela na wingini ndo wakamfwata akuwaita walifwata moto.kosa lake liko wapi jamani mwacheni mtoto wa mama marie lusambo, kama amuelewi vizuri fwateni wimbo wake wa ezau anaeleza kila kitu.

 12. le shakespear du tanzanie says:

  JB mpiana yupo juu kwa kweli tuu kama wadau mnaposema kuwa anao ubinafsi.. akijirekebisha atakuwa bien.. love u papa cheriiii

  • Farid wa Muscat says:

   yes 100% atakua bien na arudishe majeshi ya zamani wenge

  • jully weston ilunga says:

   farid majeshi ya zamani ni matapishi yake kama wewe unaweza kurudisha matapishi yako mdomoni poa na yeye ata rudiana na werra anayomtakia mabaya kila siku.

 13. Hadj Le Jbnique says:

  Hapa tuna video mbili,moja ni ya wenge musica 4×4 TT ya mpiana na ya chini yake ni ile ambayo walikuwapo wote wanaoitwa manguli kasoro Jb Mpiana tu ndio hakuwepo,tuzitazame zote kwa makini kisha tutoe tathmini ipi ilipwaya na kwanini ilipwaya?Richard Malewa,Stevin,Pius na wengine nasubiri jibu,namalizia kwa kusema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mu mpe.Kwenye video ya pili mtamsikia werra nae akisema Tolingana JB mpiana,tolingana zaiko na wenge,chock star,Tp Ok,japo Sikusikia tu akisema tolingana Koffi Olomide…sijui kwanini….anajua mwenyewe bwana,

  • Pius says:

   Hadj kaka hapo hakuna kuuliza mtu anayebisha huyo ni mchawi JB Mpiana ni kiboko na ana heshima na sehemu yake kwenye kundi la Wenge mtake msitake.

   Kama mtu anapenda mziki lazima amkubali Mpiana

 14. Hadj Le Jbnique says:

  Sikia maneno ya Aimelia akimkaribisha mdogo wake Flam Kapaya ndani ya Paris…….kweli sasa dunia muzima TOLINGANAA,Nimependa sana hii video nikaona nishee na nyie humu ndani.melesi mingi

 15. Farid wa Muscat says:

  Mzee Polepole hapo nakuona umekwenda kasi sana kwa tuhuma ulizonipa ambazo hazifanani na maneno niliyosema , mimi sijatoa kauli yoyote ile ambayo inaashiria chuki kwa JB Mpiana hilo nakataa kabisa, tena laiti ungejua jinsi vipi nimeiweka family ya WENGE 4X4 moyoni mwangu nadhani usingenituhumu kwa chuki, na ikiwa unaikumbuka list yote ya wenge kabla ya 1997 mpaka walipoanza basi ujue hao wote ni watu nawapenda sana na ninazo record zao zote na mpaka leo hii ndio starehe yangu kubwa nyimbo zao, point niliozungumza mimi ni kua JB Mpiana miziki yake mipya kwa sasa haivutii na huu ni mtazamo wangu nikiwa kama mpenzi wa muziki na hasa wa wenge kwa ujumla,

  • Anonymous says:

   JB Mpiana kushneh! albam yake ya mwisho ilikuwa Feux d l amour! albam hiyo alipigwa tafu na wana wenge wote! baada ya hapo kwishneh! nani anitajie albam ya JB inayoweza kushindana na Solola Bien? lelelelelele!

   • piusmickys says:

    Unataka kuniambia Internet ilikuwa mbaya? Je Titanic ilikuwa mbaya pia? Umesikiliza Serge Palmi wewe? Umesikiliza hizo nyimbo ndani yake au tunaongelea ushabiki jamani?

 16. Richard Malewa says:

  Hamna chochote kile ambacho mnaweza kujivunia kwa Mzee wa Makafara JB Mpiana. Mnahitaji maombi mengine muweze kutoa kuku hai waliobakia matumboni mwenu. Sisi wabongo tunajua nani ni BEST na wala haihitaji akili za Panzi kama za JB Mpiana. Tunajua hilo kwa jinsi wanamuziki wote wa Afrika jinsi wanavyoigilizia nyimbo za Werrason. Kuanzia kwenye Kuimba mpaka, kughani na kucheza ndiyo kabisaaa usiseme. Lini hivi watu waliwahi kumwigilizia JB Mpiana zaidi ya yeye kumwigiza Malou Stoch na Samaki ana Vipande vingapi kama Faly Ipupa alivyoingiza Zombo na Matembele kwenye Album yake ya Pili ambayo imekuwa ni Failure! Nitawatia vidokezo vichache tu.

  Takeu – Ile style ya Mr. Nice aliitoa wapi?

  Mjinga mpenda majivuno – Banza kanakili kwa nani?

  Kamera, kamera, kamera – Diouf Katoa wapi

  Mathematicque Mechanics = WMM Mecanique?

  Malewa! Malewa! Malewa – Sykes Katoa kwa nani?

  Siku hizi kuna vionjo vya lee lee leeee – Wazee wa Kizigo wamechomoa wapi

  Sebene Live za nani zimeshika chati kwenye Mwongo huuu?

  Nani kila Mwaka anakwenda Zenith Kila mara kwenda kufanya Maonyesho ya Kufa Mtu?!!!!!

  Juzi hawa Mapacha Watatu ule wimbo wao unaanza imba! imba ! imba! wamachomoa wapi?

  Umeangalia juzi Live Zenith YA WERASSON 2010 Clouds TV na kwanini watu wanataka TENA NA TENA TENA IRUDIWE!

  KWENDENI ZENU HUKO NA MUZIKI WA KIZAMANI NA TAAARABU ZENU ASILIA ! MAANA HATA TAARABU ZA SIKU HIZI MANENO KIDOGO SEBENE NA VICHOMBEZO KIBAO! NANI ANATAKA KUMSIKILIZA MTU MMOJA DK. 15 KWANI MMESIKIA NI SOAP OPERA!

  MMPENDE MSIPENDE! MTAKE MSITAKE! TANZANIA NZIMA INAJUA NA CONGO INAJUA! AFRIKA INAJUA NA DUNIA INAJUA! WERASSON NI MATAWI YA JUU! YUPO KWENYE KIWANGO KINGINE KABISA!

  MUZIKI WENU MKASHINDANE NA PAPA WEMBA ( aka kisauti kama JB Mpiana) MAANA NDIYO MENTOR WENU! MAANA HATA KOFI OLOMIDE ANACHEKEA PEMBENI MAANA ANAMFAHAMU!

  KWA NINI WERASSON? WERASSON? AU SABABU MTI WENYE EMBE MBIVU NDIYO UNATUPIWA MAWE!

  MMEJARIBU KILA MBINU KUMWANGAMIZA WERRASON! LAKINI KILE NI CHUMA CHA RELI! HATA LEO AKICHUKUA SKWADI YOTE YA TWANGA AU WAZEE WA KIZIGO BILA YA AKINA KAKOL, HERITIER, MIEL, CAPUCINO, BRIGADE, EBO LOTIE, OLIVIER BADO ATACHANA MAWINGU! NA ROHO ZENU MBAYA NA NYEUSI TIIII!!!

  MPAKA MTAPISHWE KUKU MWINGINE? lol

  • Hadj Le Jbnique says:

   JB HAWEZI KUMUIGA HUYO MBONGO STONCH,LABDA WEWE ULIANZA KUMSIKIA STONCH KWA MARA YA KWANZA KWA KUWA HUKO BONGO NYIMBO ZINACHELEWA KUFIKA,LOPELEE ILIKUWA IMESHACHEZWA NA JB KITAMBO KABLA YA HUYO SAMAKI WENU,STONCH ALICHOFANYA NI KUITIA MKISWAHILI ILI MUELEWE NDIO MANA SIDHANI KAMA AMEWAHI KUJISIFU KUIANZISHA YEYE

 17. Sister HKM says:

  Jamani hivi kuna mtu ana uwezo wa Kunyosha nyosha vikopo vya watu kama Werrason na Blaise Bula? Ahaaaa!

  Eti walikuwa wanamwonea wivu JB Mpiana, ma**ko yenu.

  Si ilipangwa aanza Makaba atoke Solo, Akaja JB Mpiana, sasa nini kilimfanya nin JB Mpiana amkatalie Roi De Forret naye asitoke Solo?

  Lakini majibu yake si Mliisikia Kwenye Kibuisa Mpipa! Maana mlikuwa kama Manchester United vile Mkishangaa shangaaa Uwanjani na Anti – Terro Yenu. Ahaaaaa! Ahaaaaa! Ahaaaa! Mlizoea vya Kunyonga eeeeh!

  Yule, Kaka ndiye LE-PHENOMENON!

 18. jully weston ilunga says:

  tunapo ongelea album tuangalieni kazi, kwenye solola bien werra amefanya kazi gani? sana sana ni bill cliton ambae ni rap ndo amefanya kazi sana pamoja na ferre gola kutoa wimbo wa vita imana ambao ulivuma kwenye hiyo album na bill cliton alikuja na kitu kinaitwa elicopteur.

 19. Richard Malewa says:

  Wewe ulishawahi kusikia ALBUM ya WERRASON ime-flop kama za JB Mpiana ? Kwani ukipewa nafasi ya Kuimba kwani ndiyo lazima wewe uwe umetunga? una mtindio nini? mfano wimbo kama KAMA wa Wenge alitunga nani? na nani waliimba ule wimbo? lol Una akili za Kutapika Kuku kama Mjomba wenu JB Mpiana?.

  Mara ngapi Werrason AMEENDA ZENITH? JB Mpiana mara ya Mwisho ni lini?

  Halafu wewe toka huko nje ya Congo ndiyo umjue Werrason nin ni nani? Ama sivyo mwambie momba wako Pius aweke ile post niliyoonyesha jinsi nyimbo za Werrason zimekuwa zikinakiliwa hapa Tanzania na zinavyowapatia UJIKO wanamuziki wa KITANZANIA.

  • Hadj Le Jbnique says:

   Richard sio kila mtu humu anaishi Tanzania kaka…..werra may mnampenda hapo mtaani kwenu lakini kuna sehemu nyingine hakuna anaejua anachoimba werra,usi generalise mambo na kujaribu kufanya eti tanzania ndio sampling nzuri kwamba wanamuziki wa huko wakiiga wimbo basi ndio bora duniani

  • piusmickys says:

   Salama ndugu yangu Richard Malewa.
   Tafadhali naomba tujaribu kutumia lugha ambayo haiwezi kuwakwaza wengine.
   Tuepuke maneno makali ambayo yanaweza kuwafanya wengine wajisikie vibaya.

   Asante.
   Editor – Spoti Starehe

 20. papaa lovee says:

  Hivi watu mnashindwa kuelewa toka wenge ivunjike angalia albam alizotoa Jb na werason ndio utajua nani zaidi.Titanic vs sijui albam gani ya werason ambayo nyimbo nzuri ni moja tu Koffi aina angalia sasa Titanic unakuta liberation, likalamoto , Th vs solola bien

 21. papaa lovee says:

  Jb aka binadam aka baba la daida yuko juu ile mbaya gwiji la muziki papa wemba mwenyewe anamkubali ile mbaya!!

 22. I certainly enjoy each very little little bit of it and I have you bookmarked to check out out new things of your site a ought to read site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: