Shamim ndani ya Silver Boutique…

July 6, 2011

IMG_0436

IMG_0438

IMG_0446

IMG_0447

Dadaa Shamim Mwasha wa 8020 Blog akiwa ndani ya duka la Silver Boutique akichagua mazagazaga.

Silver Boutique wanaopatikana Jamhuri Street nyuma ya Jengo la Benjamin Mkapa wameshusha mzigo mpya kwa ajili ya kina dada na akina kaka wanaojali umaridadi…. Watembelee kwa kubofya hapa.

http://silverboutique.blogspot.com/


On the Making of Speak with Your Body, AY Ft. LA’MYIA GOOD & LIL ROMEO "BEHIND THE SCENE"

July 6, 2011

264142_10150229525643359_592028358_7532117_4988906_n

Shooting hii ni ya wimbo mpya wa AY unaitwa Speak with your Body ambao ni wimbo mpya wa AY akimshirikisha Romeo na La’Myia, Shooting ambayo ilifanyika Hollywood huko Calfornia. Video hii imekuwa Directed na William Tikki na Shai Kedem na Sauti imefanywa na Riley, Waalikwa ni No Limit Soldiers, Actress Megan Good & Actor Sam Jones III kwa mujibu wa AY video inatarajiwa kutoka baada ya wiki mbili kuanzia sasa. 

 

 

260231_10150229524458359_592028358_7532096_7068296_n

Mwanadada  La’Myia akiandaliwa kwa ajili ya Shooting

264579_10150229526728359_592028358_7532138_7484241_n

Wataalamu wako kazini

260288_10150229524338359_592028358_7532094_6239371_n

AY akiangalia moja ya scene kwenye session hiyo.

260462_10150229525463359_592028358_7532114_6142061_n

AY na Lil Romeo wakishow love

260472_10150229524573359_592028358_7532098_530902_n

La’Myia

261232_10150229524388359_592028358_7532095_2549368_n

Kila mtu yuko Busy…

 

261883_10150229524523359_592028358_7532097_2887577_n

 

263493_10150229526058359_592028358_7532124_47887_n

Kazi inaendelea….


CHERIE ENVELEE, Utunzi wa Djino wa BCBG ndani ya SOYONS SERIEUX na Dadaamtu akaufanyia Remix..!

July 6, 2011

Nani zaidi Hapa?

Hapa leo tuna nyimbo ambayo ukiisikiliza vizuri utagundua ni moja iitwayo CHERIE ENVELEE lakini imeimbwa mara mbili na watu wawili tofauti tena wa familia moja yaani kaka na dada,vijana wenyeji wa kisangani,hawa ni mwanamuziki wa Wenge Bcbg Djino na dadake.

Wimbo huu mara ya kwanza Djino aliurekodi na bcbg ukiwa ni moja ya nyimbo zilizomo kwenye album lao jipya la Sayons Serieux,dada yake Djino anaekwenda kwa jina la Claudia Bakisa amekuja kuurekodi upya Kama remix,je upi umetoka bomba?

Hii sasa ndio original version iliyoimbwa na Djino mwenyewe,mwana kisangani,huyu ndio anaongea kiswahili kwenye ile video ya jb tolingana kisangani kama mlisikia akisema sema pole pole ndio mwendo na watu wakalipuka, watu wa kisangani wanaongea zaidi kiswahili.

 

 

Na huu ni wa Dada mtu Claudia Bakisa

 

Sikiliza hizi sauti kisha uniambie version ipi ni bomba kwako, The Romantic wa Mapenzi Club mercy mingi papaa kwa hii, Papaa Julie Elystone Le Charismatique Leader, Presidaa wa Congolee ya Darisalama, Uko juu Papaa Salute!!! , hebu sema kidogo hapa.


JB Mpiana Chiboko bwana, hii ni show ya Jumamosi majuzi!!

July 6, 2011

Na The Romantic

Bila ubishi JB Mpiana kwa sasa ndio mwanamuziki anaeongoza kwa kujaza watu kwenye show zake za kulipia (sio za bure)ndani ya Congo.Hilo limedhihirika juzi jumamosi iliyopita huko kisangani ambako kama mtakumbuka werrason alipeleka mambo yake huko.Sasa basi hiyo jumamosi JB alivamia anga hizo si kwa nia ya kupeleka mambo kama werrason bali yeye alikwenda huko kisangani na ujumbe mzito,aliwaambia maneno haya “BANA CONGO MOBIMBA TOLINGANAAAAA..JB MPIANA ET WERRASON TOLINGANAAA…DIDIER MASELA ALAIN MAKABA……Sikiliza 7:13 Alipoimba JB Mpiana 7:37 alipomtaja Werasson mashabiki walishangilia sana na wanamuziki wote waliondoka Wenge akiwahimiza wapendane na washabiki wote walikuwa wakiimba naye wimbo ule mtamu wa Essau.

Hapa JB anawahimiza watoto wote wa congo kupendana na kuacha kuchukiana bila sababu,anatoa mfano wa yeye na wanabendi wenzake wa zamani wawe na upendo kwani bado wako wa ndugu ila kikazi tu ndio wanatofautiana,watu walifurahi sana hasa alipomtaja werrason,wachambuzi wa mambo wanamuona JB licha ya kuwa ni mdogo kiumri ukimlinganisha na Werra kichwa chake kimejaaa akili na busara nyingi.Angalia mwenyewe video ya show hiyo iliyodhaminiwa na PRIMUS ilivyokua…..


Sizai tena toka kwa Mash Guitar

July 6, 2011

Wimbo huu unamtambulisha Kasim aka Mash Guitar unaongelea matatizo yaliyoko kwenye jamaii, Mash Guitar ndio mtunzi akiwashirikisha Nyani mtu toka kundi la Manyani Unit, jamaa ametumia mtindo wa asili wa Modern Mchiriki na kiduku kwa sana, Ndani ya wimbo huu jamaa anajaribu kuelezea wanawe wanne kila mmoja na na tatizo lake, huku akijenga hoja kwa nini hataki kuzaa tena.

Jamaa anawapa moyo wale wasio na kizazi (wagumba) kwani anasema wapo waliozaa kama yeye na wanaona bora wasingezaa kamwe kwani jamaa anawatoto wanne wakwanza ni Mlevi, Wa Pili Kibaka, wa tatu jamaa anadai ni Shoga na wanne ni Chadudoa asiyependa shule.

Haya ni matatizo yaliyoko kwenye jamii na hii ni changamoto kwa malezi ya vijana wetu na maisha ya sasa, Nakupa hongera kaka kwa wimbo huu natumai nyingine zinakuja.Kwa wanaopenda viduku huku kuna viduku na mambo yetu ya khanga moko hahaha!!.

Kasim ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Mwalimu Nyerere akisomea mambo ya Gender. Pamoja kaka!!


%d bloggers like this: