Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu “Mbeya Hatutaki Fiesta”

image

Katika hali isiyo ya kawaida tangu Tamasha la Fiesta lianze, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Mr Sugu amesema kuwa Mbeya hawahitaji tamasha la Fiesta na kusisitiza kuwa huo ni uamuzi na harakati za kupigana na maaduai wa sananaa ya Muziki.

Mbilinyi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook huku mamia ya wafuasi wake “wakipingana” kwa uamuzi huo, kwani wapo wanao uunga mkono na wengine kuukataa kwa hoja.

Maelekezo hayo ya Mheshimiwa Mbilinyi yanasema “…Mbeya hatuhitaji upuuzi unaoitwa FIESTA,kwahiyo isije na naapa…uamuzi huu ni sehemu ya mapambano yetu dhidi ya maadui hawa wa maendeleo ya sanaa,and we are very serious on this one!!!”.

Kiserikali Mbunge hawezi kuzuia Tamasha ila anaweza kuishauri Serikali au Jeshi la Polisi pale tu panapoonekana kuna dalili za uvunjifu wa amani au kama anahoja nyiongine ya msingi.

Wadau wa muziki walionyesha kupingana na wengine kukubaliana na wazo la mheshimiwa huku wengine wakihoji ni kwa nini Mh. Atumie nafasi yake kuwanyima raha mashabiki wa muziki na tamasha hilo “…Bifu lako na cloudz lisiwanyime wa2 starehe ya burudani…at least nao pia wapate nafasi ya kuwaona wasanii kwa ujumla wao…mtanzania hanyimwi maoni…” alisema mmoja wa mashabiki ambaye alichangia status ya Mh. Mbilinyi.

“Lakini Mheshimiwa Mbilinyi hakusema kama hayo ni maamuzi yake binafsi au anaongea kama Mbunge. Pia Sijajua kama huu ni muendelezo wa yaliyowahi kutokea huko nyuma kati ya Mh. Sugu na Kituo kimoja cha radio ambacho ni sehemu ya waandaaji wa Tamasha hilo lakini wadadisi wa mambo ya burudani wanasema ni vigumu kwa chama kama Chadema ambacho kinasimamia Demokrasia kufikia mahali kuwaamulia wananchi kutokana na sababu zao binafsi itakuwa ngumu…” alisema mchangiaji mwingine

Pia wapo waliomshauri Mheshimiwa kuhusiana na uamuzi huo kwa kusema “Mheshimiwa achana nao usije ukawekwa rumande 2kakosa mwakilishi..utakachotakiwa kufanya ni wanambea kusign patition against hiyo fiesta..ground zinaweza kuwa nyingi katika hilo kama maradhi and behaviour change in negative way otherwise utaonekana mkorofi na unachochea fujo then watakusulubisha..dont gv ur enemy chance to humiliate u coz they hv the ryt as well ni mtazamo tu..” alisema mdau mwingine aliyejitambulisha kama Aunt Manie.

“mimi kwa mtazamo wangu utakuwa unawanyima watu wa mbeya burudani jamani tusichanganye malumbano binfsi, siasa, umimi katika starehe we nani ambaye uazue watu wengine wasifanye starehee nazani sasa umefika wakati wa kuwapima akili nyie mnajifanya miungu watu” Alisema mdau mwingine Bw. Habib

Ila Habib alikutana na challenge toka kwa mdau Robert ambaye alisema “…”hakuna starehe bila maisha wewe! hata hao wasanii wanaowaleta hawalipwi ipasavyo njaa tupu…so hatuwezi kusapoti unyonyaji”

Tamasha la Fiesta hufanyika kila mwaka huku likiwa na kauli mbiu Fulani kwa ajili kuhamasishana huku likiambatana na burudani ya muziki. Kwa mtazamo wangu kuna njia mbadala za kupambana na haki za wanamuziki lakini inakuwaje kama hao wanaopiganiwa kwa haki zao wanakubaliana na hao wanyonyaji?

Hapo naona bado kazi ya watu kama Mheshimiwa Mbilinyi kuwa itakuwa ngumu, lakini kama kungekuwa na umoja wa hao wanamuziki na wao kupinga kile anachoongelea Mr Sugu basi wangefanikiwa.

Mi Naungana na Deejay Funga Flex kwa Kusema makubaliano kati ya msaniii na promota ni kwa pande hizo mbali tu, third party can’t do anythin even if msanii akubali kuperform bure! Hakuna ulinzi wala sheria itakayotengua hilo! Issue hapa na kubwa zaidi ya wasanii kunyonywa! Nilitegemea SUGU na waheshimiwa wengine wapiganie serikali kutunga policy za maana zitakazosimamia entertainment/music industry zaidi ya kuzuia FIESTA.

Binafsi ni mfuasi mzuri wa Mheshimiwa Mbilinyi lakini kwa hili naomba kutofautiana na we Mheshimiwa, acha kila matu atumie Uhuru wake, Tulifurahia umeingia Bungeni kama nilivyosema kuwa mstari wa Mbele kusimamia Policy nzuri ili hizo Policy ziwabane hawa wanyonyaji. Wakati tayari Tamasha lenyewe ndio limeeanza kwa uzinduzi kufanyika kanda ya ziwa huku wasanii wakiwa wamesha saini mikataba ikiwa ni pamoja na onyesho la Mbeya, kwangu mimi ingekuwa bora Mh. Sugu akatumia kiti chake na ukongwe kwenye medani hii ya sanaa kuwahamasisha wanamuziki wagomee tamasha hilo kwakuwaelimisha haki zao za msingi ikiwemo hili la unyonyaji ambalo anapingana nalo.

Ni Mtazamo tuu.

Advertisements

13 Responses to Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu “Mbeya Hatutaki Fiesta”

 1. Paesulta says:

  Kwani toka lini mbunge akaweza kuzuia kitu kama hiki?maana nnavyojua kibali kinatoka katika serikali ya jiji,na mbunge hana mamlaka yeyote kwa hilo.Nadhani tumerukia tu kumpinga Sugu,nadhani anachokampeni hapa ni kama alivyosema ni kuzuia ufisadi huu katika sanaa.Nadhani hata nae anajua kuwa hana mamlaka ya kuzuia kufanyika kwa tamasha hili,isipokuwa tu kama atatumia ”nguvu ya wananchi”,kitu amabacho naona ni kigumu kwani wananchi wana mambo ya maana kuwaumiza vichwa…..Tuhoji kama kweli ana maamla hii kisheria.

 2. Dada Ziada says:

  TUNALAAANI KWA NGUVU ZOTE KITENDO DHALILI KILICHOFANYWA NA VIONGOZI NA MASHABIKI WA DC MOTEMA PEMBE KWA KUMVUA NGUO DADA YETU MWANDISHI WA HABARI WA JAMBO LEO PALE ALOPOKUWA KAZINI , UWANJANI, KINSHASA ETI KWA MADAI YA KWAMBA ALIKUWA KAFICHA NDUMBA SEHEMU ZE SIRI.

  HIKI KITENDO HAKIKUBALIKI HATA KIDOGO KWA SISI WATANZANIA AMBAO TUMEKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA WAAFRIKA WENZETU NA HATA WACONGOMAN .

  WANAHARAKATI PLEASE TUSHIKIE BANGO UDHALILI HUU ULIOFANYWA NA MASHABIKI NA VIONGOZI WA MOTEMA PEMBE. HIKI KITENDO HAKIENDANI KABISA NA JINA LAO LA MOTEMA PEMBE KWA MAANA YA MOYO MWEUPE.

 3. Anonymous says:

  itakua ngumu

 4. Nshimbo says:

  Sugu una mengi ya maana ya kufanya kwa hilo sikuungi mkono kaka yangu.

  Mchangiaji wa kwanza kumbuka mbunge ni muwakilishi wa wananchi waliowengi hapa Sugu kaongea km mbunge ujue so tueleweje?

  Nakubali wanyonyaji wanatakiwa kukomeshwa. Ila sugu angetumia ushawishi wake kuwashawishi wasanii wakatae tangu mwanzo,angefanikiwa.

 5. Moses Kibaja says:

  Us@&£/:#%*e mtupu!!!

  Hao Clouds wanastahili hayo wehu na wezi, wasanii hawana pakukimbilia tu, wanatajirika kwa kazi za wasanii na wasanii wanabaki kuwa masikini tuu

 6. Anonymous says:

  Kuku kujipeleka kwenye banda lenye mchinjaji NANI alaumiwe Kuku au Mchinjaji?

 7. oppa 2nyi says:

  Mimi ninadhani dhana ya Mh.Mbilinyi (MB) Mbeya mjini ilikuwa ni sahihi kukataa the so called Fiesta kufanyika Jimboni kwake Mby. Miongoni mwa majukumu ya Mbunge ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao bila kudhulumiwa ,suala kwamba Mh.May
  anamajukumu mengi muhimu kuweza kulishughulikia suala la Tamasha la Fiesta Mbeya siyo sahihi, suala la dhuluma especially kwenye sanaa ya music ni eneo linalowasumbua wasanii wengi wa music Nchini lakini wamekosa mtu wa kuwasemea hivyo Mh.May anawajibu mkubwa yeye kama mdau kuhakikisha anapambana kuhakikisha dhuluma hii inakoma akumbuke naye ni mhanga kwenye hili sasa kwa kuwa amepata nafasi ya ubunge alipiganie ili kuwasaidia wasanii wengi nchini ambao wengi wao ni hohehahe wamenyonywa na wanaridhika na kimkwanja kidogo tu cha kubadilishia mboga huku wanaojiita mapromota wakineemeka na kuota vitambi vikubwa mithiri ya Hippopotumus.

  Mr May hakikisha kuwa unasimamia sheria na Sera kuhusiana jenga hoja mjengoni kwa kushirikiana na wabunge wenzako kuhakikisha kuwa wasanii hawadhulumiwiwa

 8. Mussa Khamsini says:

  Mbunge simama kidete hawa Clouds Wehu, ila fata ushauri wa Kaka Pius pambana nao kupitia Bungeni.

 9. Aloyce Massawe says:

  Ifike mahali we sugu uache wivu..ulifanya mziki ukakushinda ulishindwa hata kufika level ya mr nice.. sasa nakuomba heshim wadogo zako kazi wanafanya na tunawakubal fiesta tunaipenda ww ni nani uongelee mioyo yetu? Imoooooooooo

 10. Yen Halbur says:

  Extremely good site and exceptional and articles.useful style, as share great stuff with superior tips and concepts.

 11. Marlen Lube says:

  A few things i have continually told persons is that while searching for a good on-line electronics retail store, there are a few aspects that you have to take into account. First and foremost, you want to make sure to discover a reputable and reliable shop that has received great reviews and classification from other consumers and marketplace experts. This will make sure that you are dealing with a well-known store that gives good services and aid to its patrons. Thanks for sharing your notions on this weblog.

 12. We absolutely love your blog and find most of your post’s to be what precisely I’m looking for. Do you offer guest writers to write content for you personally? I wouldn’t mind writing a post or elaborating on most of the subjects you write regarding here. Again, awesome web log!

 13. It’s a shame you don’t have a donate button! I’d definitely donate to this excellent blog! I guess for now i’ll settle for bookmarking and adding your RSS feed to my Google account. I look forward to new updates and will share this blog with my Facebook group. Chat soon!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: