Ndoa ya Drogba yafungwa kimya kimya.

image

 

image

 

Waalikwa wakijivinjari.

Hatimaye jana jumapili mchezaji maarufu wa Ivory Coast na Chelsea Didie Drogba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Lalla Diakite huko the Marie de Monaco, Monaco.

Inasemwa kuwa sherehe hii ilifanikishwa na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich na ye alikuwa ndiye Chairman wa Shughuli nzima, huku wachezaji wenzake kama Solomon Kalou na Florent Malouda wakiwa ni wapambe wa Bwana Harusi. Mbali na hao mwanamuziki nyota wa R n B Akon pia alikuwa ni mmoja wa waalikwa ambapo Fally Ipupa alikuwa mmoja wa walitumbuiza.

Habari zinasema kwamba Drogba aliupenda sana wimbo wa Jupa Remix ambao Fally alishirikishwa na J Martin na ndipo alipomualika kuja kutumbuiza binafsi lakini Fally alipowasiliana na Drogba alimwambia kuwa wimbo ule ni wa J. Martin hivyo akitaka aupige ni lazima mwenye wimbo pia awepo ndipo mwanamuziki J. MArtin alipopewa mualiko rasmi.

Drogba na mpenzi wake walikutana awali mwaka 1999 huko Paris Ufaransa ambapo Drogba alikuwa katika harakati zake za mwanzo za soka, na tangu hapo wamekuwa wapenzi na walifanikiwa kupata watoto watatu lakini walikuwa bado hawajafunga ndoa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza toleo la leo, Tofauti na watu wengine Drogba alikataa wazo la kufanya harusi ya kifahari na kusema kuwa anataka kitu cha kawaida kabisa.

“Anataka kufanya ndoa ya kawaida kabisa ikishuhudiwa na marafiki wa karibu pamoja na ndugu wa karibu tuu, anataka kumpa mpenzi wake Lala harusi ambayo aliiwaza kwani hawakuwa na uwezo wakati wanakutana” kilisema chanzo cha habari cha The Sun.

Weekend ya jana pia ilishuhudia mchezaji wa Manchester City Vincent Kompany na mwingine wa Luka Modric pia wakifunga ndoa.

image

Dogba na MkeweLalla Diakite wanatoka dini tofauti huku mkewe akiwa Muislamu na Drogba ni Mkristu wa madhehebu ya Roman Katoliki lakini wote wanaheshimu dini zao.

Wachunguzi wa maisha ya Ma Star wanasema Drogba na Mkewe Lalla Diakite hawa ni version ya kiafrica mpya ya David and Victoria Bekham huku mitandao ikimsifia kuwa ni mtu aliyemheshimu sana mkewe na kutokuwa nakashfa za ngono kama wachezaji wengine.

Advertisements

3 Responses to Ndoa ya Drogba yafungwa kimya kimya.

  1. Jordan says:

    Kaka nakupendea hapo tuu nimeiy=tafuta sana hii story.
    Big Up Drogba umeonyesha mfano harusi za kitajiri hazina mpango.

  2. Hadj Le Jbnique says:

    Nampenda Didi,siku zote amekuwa na msimamo tofauti na wachezaji wengi weusi wenye mafanikio ambao wengi wao wamekua wakikimbilia kuoa wazungu,so didi na sam eto’o fils wametutoa mkosi sisi weusi kwa kuoa weusi wenzao…….thanx a lot u guys,we proud of u.

  3. Hadj Le Jbnique says:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: