Essien aamua atahudhuria vyote Mechi ya heshima ya Kanu na Harusi ya Drogba Ufaransa.

image

Pichani ni Drogba na Mchumbaake Lalla Diakite.

Kutumbuizwa na Fally Ipupa na Jay Martin

Mchezaji wa Chelsea na Ghana Michael Essien ameamua kuhudhuria shughuli zote mbili za marafiki zake ambazo zitafanyika kesho jumamosi.

Essien ameamua kuhudhuria mechi ya mwisho ya Kanu na pia atahudhuria ndoa ya mshkaji wake wa karibu Didier Drogba ambayo itafanyika huko Nice Ufaransa masaa 24 baadaye.

Kanu ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kwa Essien kukubali ofa ya kusaini na Chelsea mwaka 2006 akitokea Lyon ya Ufaransa.

Hata hivyo Essien atakosa bachelor party ambayo itafanyika muda yeye akiwa Nigeria kwa mchezo wa kumuaga Kanu kisoka, lakini pindi akimaliza mchezo huo atawahi Airport ili aiwahi Harusi ya mshkaji wake Drogba.

“Uzuri ni kuwa kuna lisaa zima baada ya mechi kuisha hivyo ataiwahi Air France inayotokea Lagos” alisema mmoja wa maofisa walioandaa mechi hiyo.

Miongoni mwa ma star wengine kwenye mechi hiyo ni pamoja na El Hadji Diouf,  Asamoah Gyan na Sulley Muntari, Samuel Eto na Emmanuel Adebayor.
Bafana Bafana watawakilishwa na kipa wao nambari moja Itumeleng Khune, Aaron Mokoena na Siphiwe Tshabalala, mchezaji ambaye ameweka historia ya kufunga goli la kwanza wakati kombe la dunia lilipochezwa kwa mara ya kwanza barani Africa.

Awali ilisemwa kuwa Essien ataikosa ndoa ya Drogba kwa ajili ya mechi hii.

Aidha mwanamuziki J Martin na Fally Ipupa ndiyo watatumbuiza kwenye sherehe hiyo, Inasemwa kuwa Drogba anaupenda sana wimbo wa Jupa Remix ambao Jay Martin na Fally Ipupa wameshirikiana na hivyo alipendekeza wawepo. Tutawaletea picha na habari zaidi juu ya harusi hiyo.

Advertisements

2 Responses to Essien aamua atahudhuria vyote Mechi ya heshima ya Kanu na Harusi ya Drogba Ufaransa.

  1. Isa Kitka says:

    I think this really is an informative publish and it is actually experienced and really handy. I would like to thank you for that efforts you might have manufactured in creating this post.

  2. Julio Lorr says:

    Extremely good web site and great and content articles.worthwhile style, as share great things with fantastic tips and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: