Inch’ Allah ya Koffi Olomide, Balaaa!!

Rafiki yangu Mngoya Ahmed Juma Lukuta wa Kibanda Kicheba kwa Semkope yeye si mpenzi wa miziki ya Congo hata kidogo lakini alinunua CD kwa ajili ya wimbo huu wa Koffi zamani kidogo.

Baada ya kuisikiliza nilijua ni kwa nini aliupenda huu Wimbo. Kwa wanao mjua Koffi ana sauti sita ambazo anaweza kucheza nazo na kubadilisha kiasi akaimba kwenye wimbo na mtu usiyemjua ukadhani kuna watu sita tofauti wanaimba.

Kingine kikubwa ni jinsi Koffi alivyo na uwezo wa kutengeneza timu na anavyo waachia vijana wake watambe kwenye nyimbo zake, Ni ukweli anatumia pesa nyingi kuandaa Albamu ikiwa ni kwenye studio za hali ya juu lakini vipaji pia vina nafasi zake.

Msikilize Montana Kamenga (Mjombaake na General Defao), Msikilize Tibafola pia, Msikilize Geco Mpela enzi hizo na wengineo walivyonata na Beat kwenye wimbo huu, Pia chukua muda wako kumsikiliza Lora Mwana Digital mtoto wa marehemu Dindo Yogo.

Papaa Edgar Benson Kiiza nakati ya Kuala Lumpur ye huwa ananiambia Koffi ana amplifaya kwenye koo inayochuja sauti yake.

Binafsi namkubali sana Koffi na hiki kilikuwa kikosi chake cha ukweli kabla ya kuparaganyika.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: