Bonne Anniversaire mukulu, A Toi Souverain bin Adam, Papa Cheri, Moto Pamba,el matador,mukulu ke le christ t garde….

Anatimiza Miaka 44 Leo!!

19436_100192180015309_100000735813655_2578_4372194_n

Mwanamuziki kiongozi wa kundi la Wenge BCBG Jean Bedel Tshituka Mpiana leo anatimiza miaka 44 tangu kuzaliwa kwake.

Mdau wangu Mandago na Pendo Mamaa Internet wa A Town alinitumia email kuniuliza picha hii ambayo niliwahi kuiona je JB amembeba nani?

Kwa wasiojua JB MPIANA MUKULU WA BAKULU LE GRA LIDEE GENERASIO DE LA MUSIC CONGOLESE SUVEREIGH TSHITUKA A.K.A PAPA NA DAIDA ana watoto wanne akiwemo huyu aliyembeba ambaye anaitwa Daida, huyu ni kipenzi cha JB Mpiana na alizaa na mwanamke anaitwa Amida Shatur, kama umesikia nyimbo nyingi za album ya Internet na TH amemtaja sana humo.

JB Mpiana alizaliwa huko Jimbo la Katanga mwaka 1967 tarehe kama ya leo June 2. JB ni mtoto wa Mpiana na Agnes Lusambo walipohojiwa kuhusu mwana wao wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa akiwa na miaka 25, Mama yake mzazi alisema JB Mpiana ni mpenzi wa Wali Maharage na Samaki, anasema Mpiana hata akibadili chakula lakini maharage lazima yawepo.

Alichowahi kusema Baba yake ni kuhusu kugombana na mwanaye alipokuwa anakataa shule na kuzama kwenye muziki, kwani JB Mpiana ana Diploma (State diploma of humanities commercial and Administration.) nimetohoa kutoka Kifaransa na hiyo ndio maana nzuri niliyoipata, tangu hapo Mpiana hakutaka kuendelea na masomo zaidi ingawa wazazi wake waikuwa na Uwezo wa kumsomesha.

Mpiana hakuwa muanzilishi wa kundi la Wenge kwani wakati anajiunga nalo wanamuziki wengine kama Didie Masela aliyekuwa akipiga gitaa la bass na Werasson walikuwa tayari wamo kundini ila Kujiunga kwake na kundi hili pamoja na vinara wengine kuliling’arisha na kuongeza umaarufu wake.

Aliliongoza vyema kundi la Wenge BCBG ingawaje kulikuwa na watu kuondoka hapa na pale, akilizungumzia hilo alipokuwa ziarani hapa Dar Es Salaam Mpiana alisema BCBG ni kama Dream Team akiondoka mmoja mzuri ujue kuna wazuri kumi wako njiani wanakuja.

Birthday hii ya JB Mpiana imekuja huku albamu yao mpya ya Soyouns Serieuxe ikiwa sokoni na inasemwa kufanya vizuri pia. BAdo sijajua leo JB anapiga wapi huku akisherehekea siku yake hii muhimu lakini mara nipatapo nitawajuza.

Happy Birthday JB Mpiana

Naomba Nikuache na Mpunda Style, ambayo kwa sasa inashika toka kwenye albam mpya ya Bana Wenge wa Ukweli.

5 Responses to Bonne Anniversaire mukulu, A Toi Souverain bin Adam, Papa Cheri, Moto Pamba,el matador,mukulu ke le christ t garde….

 1. PDGTony says:

  Happy Birthday JB Mpiana Leader Charismatique!!!

 2. Hadj le Jbnique says:

  Watoto wa JB wanaojulikana official ni watatu,Wakwanza ni DAIDA ambao ndio huyo aliembeba,wa pili pia ni msichana anaita Soraya na watatu ni kidume chake ambae anaitwa Junior Mpiana,ila Mamaa Amida yeye jumla ana watoto wanne kwa sasa,ambao ni Daida,Soraya,Junior na Diam Kinuani ambae ni mtoto aliezaa na Dikin(Didi kinuani)na hilo jina la Mtoto wa AMIDA aliemzaa na DIKIN kirefu chake ni Didi and Amida,yani DIDI + AMIDA=DIAM

 3. imani says:

  Kweli wewe una weza kuriport habari, nilidhani utakosea kwasababu mimi namjua JB mwanzo mwisho ni roll model wangu na band yangu nimei form kama ya kwake nimekua na album zake nyingi sana japo watu kama kina Alain Mpela (Afande) Titina Alcapone, Tutucaluji nawengine wengi walipoondoka ilinifanya niyumbe sana kununua record za JB baada ya kuimiss sauti yake Album ya mwisho kununua ni Quel es Problem? zingine nazipata kupiti TV na Redion stations nikikuta zita pigwa hapohapo nasikiliza.
  Lakini ume nikuna sa una weza kazi Hongera sana!

 4. FAN FAN says:

  Salut papa chérie j’aime ta musique depuis mes 6ans

 5. Patrick ramazani says:

  Papa cheri naza moto naho! Naza mwana wa sud-kivu east. Courage ya danzeee!!… Vieux nangaee….

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: