Sean Kingston Apata Ajali Mbaya, Aendelea Vizuri

image

Mwanamuziki machachari katika sekta ya Raga, Sean Kingston wa Jamaica, ambaye alipata ajali mbaya siku ya Jumapili, anaripotiwa kuwa anaendelea vizuri. Kingston alipata ajali hiyo akiendesha pikipiki ya kwenye maji, Jet Ski, katika ufukwe wa bahari huko Miami, Florida.

Kingston alikuwa akiendesha pikipiki hiyo ya mwendo kasi huku akiwa amepakia abiria wa kike, majira ya jioni ya Jumapili. Inasemekana Kingston alishindwa kukimiliki vyema chombo hicho na hatimae kwenda kujibamiza katika ukingo wa daraja.

Kingston na abiria wake waliokolewa na boti moja ndogo iliyokuwa ikipita karibu yao na baadae kuwahishwa hospitali na kikosi cha zima moyo cha Miami. Awali, hospitali ya Jackson Memorial ilitoa taarifa kwamba mwanamuziki huyo alikuwa hoi bin taaban, lakini sasa habari zinasema kwamba jamaa anajitambua.

Abiria wa Kingstona yuko buheri wa afya na anaisaidia polisi kwa uchunguzi, kwa mujibu wa wavuti ya Local10.com

Kingston alianza kuwika katika tasnia ya muziki mapema 2007 akiwa na singo yake ya Beautiful Girls. Singo hiyo ilikamata chati za nchini Marekani na Uingereza. Ameshafayatua vibao vingine matata akishirikiana na wakali kama Justin Bieber na Natasha Bedingfield.

Albamu yake ya tatu inategemewa kuachiwa baadae mwaka huu.

http://www.guardian.co.uk/music/2011/may/31/sean-kingston-jet-ski-c…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: