Pengo la Ferre WMMM kuzibwa na kijana huyu?

Tutazame video hii werra pamoja,utamuona dogo mmoja anaitwa Merlin Bouton,huyu naamini ataziba pengo la Ferre Gola Hapo WMMM Japo mawerasonique wamekua wagumu kulikubali pengo la Ferre lakini ukweli ni kwamba Ferre aliacha pengo wmmm,sasa pengo nadhani huyu bwana mdogo kaliziba

27 Responses to Pengo la Ferre WMMM kuzibwa na kijana huyu?

 1. Hadj le Jbnique says:

  HAYA SASA NDIO MAMBO YANGU,KITU HIKI MAALUM KWA AJILI YA KUPROMOTE PRODUCT YA BRALIMA YAANI PRIMUS BEER TOKA KWA WENGE MUSICA YA NGIAMA MAKANDA PHENOMENA IGWE KIMETULIA ILE MBAYA,DOGO BOUTON YUKO JUU NAMTABIRIA MAKUBWA KUFIKA MBALI KIMUZIKI,NA WENGINE WOTE WALIOIMBA WAMEFANYA KAZI NZURI,SAUTI NZURI,WERRA HAJAWEKA ILE YA KWAKE MAMBO YAMEKUA BURDAN,MZEE MZIMA NAONA ANAUZA SURA TU HAPA HUKU VIJANA WAKIPIGA KAZI,KUMBE ASIPOWEKA SAUTI YAKE MUZIKI WA WMMM UNAPENDEZA,UMEHARIBIKA MWISHONI ALIPOAANZA KULIA LIA

 2. Stivin says:

  Wewe, Sauti ya Wera iko Unique congo nzima hakuna! ukitaka kuamini chukua wa Dadet wa album ya Pentagon walioimba kwa kupokezana na Mpiana! tafuta mtu asiwajua halafu muulize sauti ipi tamu atakujibu! acha ushabiki!

 3. Hadj le Jbnique says:

  ya sele bulla tutaiitaje kama hiyo ya phenomena unaiita unique?ok bwana pengine ndivyo unavyoona wewe ila kuweka tu kumbukumbu sawa katika wenge musica 4×4 tout terrain watu ambao inasemekana hawakua na sauti nzuri ingawa walikua na vipaji ni werra,tata mobitch adolphe dominguez na sele,ila sele alikua anajua sana kuitumia hiyo hiyo sauti yake na mambo mengine ya arrangement jamaa alikua juu,werra kama ulikua unaifuatilia wenge na kujua majukumu ya kila mmoja ni wazi unajua kwamba jamaa upande wa muziki kama muziki hakua na nafasi yeyote ya uongozi unaoendana na muziki,hakuwahi kuwa chef d’orchestre (sijui kama unajua maana yake)licha ya kuukaa wenge muda mrefu kama muanzilishi,wala pia hakuwahi kuwa president wa bendi,unajua alikua na cheo gani?alikua mtunza fedha!cheo ambacho sidhani kama kina uhusiano wowote na mambo ya muziki,pia jamani mjue kihistria werra si muimbaji,uimbaji aliforce tu,yeye kipaji chake ni kupiga ngoma za tumba!

 4. Stivin says:

  Hahaha! unanichekesha sana weye! Kuwa mtunza fedha haimaanishi kuwa hakuwa na sauti, Angalia video za zamani za wenge Jukwaani, ndo utajua nani walikuwa viongozi wakuu wa Wenge! Jaribu kutafuta video ya Shoo ya Mwaka 1996 waliofanya na Bozi Boziana na nyingine waliofanya na Papa Wemba. Nani alitunga nyimbo nyingi kwenye albam ya Pentagon? Nani alitunga Kinebouge? Sikiliza Hi Ho Ha New Image, halafu uniambie nani walikuwa lead sing’ers? Ndugu yangu Werra kama Werra hakuwa na kipaji basi Mpiana angeondoka na Utamu wote wa Wenge! Baada ya Wenge Kuvunjika na Mpiana kubaki na karibu Cream yote nani amevuma? Mpiana ameongeza nini katika CV yake! Be realistic pubguza mapenzi kwa Mpiana!

 5. Stivin says:

  Samahani nilimaanisha Kala yi Boeng! wimbo bora zaidi kuwahi kupigwa na Wenge!

 6. Hadj le Jbnique says:

  bora umegundua mapema na kurekebisha mwenyewe kuhusu kinebouge,lakini bandugu wapendwa hebu tujaribu kujiuliza wenge musica ilikuwapo zamani hata kabla ya JB MPIANA kujiunga,lakini mmewahi kujiuliza ni kwanini haikupata mafanikio huko nyuma mpaka JB alipokuja kujiunga nayo?hili swali nawaachia mawerasonique wote sio wewe tu,wote msaidiane kulijibu.kuhusu mpiana angeondoka na utamu baada ya bendi kutengana,hili kila wakati nawaambia hebu tufuatilia album moja baada ya nyingine baada ya werra na genge lake kuzama kwenye ajali ya titanic,tuanze na album zao za kwanza,ni wimbo gani labda hata mmoja katika FORCE D’INTERVENTION RAPIDE unaoweza kuulinganisha na wimbo wowote wa TITANIC?tuzichambua na kuzilinganisha hizi album mbili kama hatukugundua itakua ni sawasawa na kulinganisha kifo na usingizi na kusema viko sawa!

 7. Stivin says:

  Wakati hizo albam mbili zinatoka, Titanic and Force FORCE D’INTERVENTION RAPIDE, wimbo bora wa Kongo ulikuwa Chantal Switzerland, na mwanamuziki bora alikuwa Werrason. Unalijua hilo?

 8. Hadj le Jbnique says:

  Ha ha haaa kaka hizo record zako mmmm!zinatia shaka,kwanza kala yi boeing wimbo bora zaidi kuwahi kupigwa na wenge…!hapa Unakwepa kuitaja KIN E BOUGE na MULOLO,Kwanini…sababu unazijua mwenyewe.Pili Chantal Swittzerland wimbo bora congo 1999!!!hapa hukutuwekea hata waliotoa hiyo tuzo,kwanini?…bila shaka huwafahamu na wala hawapo,may be hii wazee wa HEAD OFFICE OF WENGE MUSICA kama wanavyojiita wenyewe mkiingereza(mkifaransa ndio wenge musica maison mere)walijipa wenyewe,maana mzee mzima kipindi kile alikua anatafuta kila njia ili amfikie mpiana.Kiufupi kaka hiyo award haikuwahi kuwepo.Award ambayo waliipata miaka ile GOLDEN RECORD kupitia album lao la solola bien ambayo haitolewi congo,inatolewa FRANCE,ndio iliyomtoa mpaka kufikia mawerasonique kumwita Le Phonomenon kutokana na shows zake kujaza watu(wahuni)wengi,na hili limechangiwa zaidi na ujanja wake wa kutoa misaada kwa watoto wa mitaani,kutoa vyakula kwa wafungwa na kupeleka madawa mahospitalini kinsasha,ndio ameweza kuwin heart and mind ya watu wa kawaida wa mitaani ndani ya congo ambao ndio wamekua chanzo cha vurugu maana huwa ukimkosoa jamaa ndani ya congo wanaanzisha vurugu.Hii nadhani inatokana na aina ya muziki wanaosikiliza toka kwa mzee mzima-vurugu tupu.

 9. Stivin says:

  Kweli nimeamini kuwa humpendi Werrason, Hiyo tuzo ipo na inatolewa congo na Repa Bora mwaka huo alikuwa Bill Clinton, Vp kuhusu Kora? JB kashinda ngapi? Vipi kuhusu Mpunda, mbona kimya? Halafu unasema eti WEnge ilikuwa haijulikani kabla JB kujiunga, JB alikuwa najulikana kabla ya kujiunga Wenge? Hata kama Hutaki De la Foret ndo mwanamuziki bora Congo Kwa sasa! We unasema Werra Hakuwa na Sauti Ukamtaja Adoldh and Bula, Maana yake wewe sauti ni Emelia, Mpiana na Mpela, Mbona wamefulia? Muziki sio sauti nyembamba amabazo unazipenda wewe, ingekuwa ni Hivyo Franco, Pepe, Kale na Madilu wasingevuma, Manda Chant angekuwa Maarufu kuliko JB(Kwa sababu ana sauti nzuri kuliko JB) Mpiana katoa Albam gani yenye viwango vya solola Bien toka wamegawanyika?

 10. Richard Malewa says:

  Nimechungulia hapa ni siku mingi sijapta pole sana mdogo wangu Stivi nitapita baadaye tuje tuwazoboe hao WATAPIKAO KUKU MZIMA! MZIMA! MZIMA! nitakuja tena tuwatoe MAPEPO YA JB! Exorcise the Ghosts! Mambo ni LE LE LE LE LEEEE LEEEEE LEEEEEE LEEEEE LEEEEEE WERASSON ANALETA MAAAAAMBO ANALETA MAAAAMBO EEEEEEHHH! LEEEE LEEEEE LEEEEE LEEEEE MTABANA MTAAACHIA WENYEWE!!!!!!!!! INAZINDULIWA RASMI MWEZI HUU TECHNO MALEWA 2 UKISIKIA LEEEEE LEEEE LEEEEE HAPA BONGO UJUE NI KWA MFALME ASIYEPINGIKA THE ONLY AND ONLY ONE LE PHONEMENA LE ROI DE FORRET. NAKUJA STIVI MDOGO WANGU USIWE NA HOFU WATU WADOGO SANA HAWA!

 11. Richard Malewa says:

  Wewe unasema eti anagawa zawadi kwa watoto wa mitaani na mayatima ili apate umaarufu wewe! wewe! Mwogope Mungu wewe! Yaani unataka kusema ubalozi wa heshima kapewa na taasisi ya kimataifa kwa sababu ya kutoa zawadi? toa basi na wewe uone kama UNICEF watakupatia huo ubalozi wa heshima.

  Werrason ana mchango mkubwa sana kwa kutumia karama au kipawa chake cha Muziki katika dunia hii lakini amekuwa mkarimu mno kwa kurudisha kile anachokipata kwa makundi ya watu, watoto, mayatima na watoto wa mitaani kile anachokipata! siyo kwenda kutoa kwa mashetani kama mnavyofanya na JB Mpiana wenu!

  Yaani pamoja na ku-Exorcise ma-Ghost yenu bado mnataka mtolewe Kuku wazima wazima tena!

  Uchoyo wa JB Mpiana unadhihirika mpaka jinsi anavyowabania vijana wasiimbe tofauti na Le Roy De Forret . Ndiyo maana mpaka leo hana kijana yeyote wa kujivunia aliyetoka Solo. Ovyooo! na kastaili kenu kamoja ka-mpunda, JB Kachemka vibaya mno kuingilia anga za sebene za Le Roy Forret, sasa tutawaangamiza moja kwa moja na Techno Malewa 2.

  Werrason Analeta mambooo Analeeeta maaaambo yoooooo

  Werrason Analeta mambooo Analeeeta maaaambo yoooooo

  Leleleeeeeeeeee Leeeee leeeeee leeeee leeeeeee

  Torekaaaaaaaaaaaaaaa

 12. Jordan says:

  Huwezi kusema JB anawabania vijana hebu sikiliza nyimbo nyingi zimetamba ni za vijana wametunga.
  Sikiliza kitu cha Sunda Bass cha Liberez kabanwa yule?

 13. Stivin says:

  Mzee Malewa! JB alikuwa nasaidiwa sana na Makaba katika kupanga nyimbo zake! Jamaa walikuwa marafiki walioingia wote Wenge, na alimsaidia sana kuipanga Feux De l’mour, Baada ya hapo Jamaa kapotea! Muziki wake ni mwepesi sana! afadhali angemtafuta hata Boukinafaso Mboka Liya amsaidie! Mboka liya ndo alietunga solo la TH japo kwenye recording hakuwepo! Tatizo la JB roho Kwatu.

 14. Hadj le Jbnique says:

  Nilikua nawafuatilia mawerasonique nione mnavyofunguka na kutema nyongo,ni hivi bandugu,nilitaka mnitajie award iliyoshinda chantal kama wimbo bora wa congo 1999 ilitolewa na nani,nasikitika mpango naingia mtamboni muda huu hakuna werrasonique yeyote aliyethubutu kufanya hivyo,mmoja kakimbilia kora award!naomba nimuulize swali,hivi kati ya WERRA,DEFAO na AWILO nani kashinda tuzo nyingi za kora?je kati ya AWILO na WERRA nani yuko juu kwa kigezo cha kora music award?mi nadhani kuhusu kora jb hakuwahi kupata hiyo award kwa kuwa may be hapigi muziki wa aina ya awilo na werra,nadhani ndio maana hata mwalimu wembadio shungu a.k.a.PAPA WEMBA hakuwahi kushinda kora award ambayo hata sifahamu iliishiaga wapi.

  Kuhusu JB kutotoa kijana hata mmoja,hapa sijiu ulikua una maanisha nini,lakini kama ulikua una maanisha kutoka na album nadhani umesahau au hukuanza muda mrefu kukifuatilia kizazi cha wenge,pengine malewa ndio iliyokufanya uijue wenge na werrason,lakini mtu wa kwanza kabisa kutoa solo album alikua ni Aimelia Lyase Demingongo,Alitoa album iliyokwenda kwa jina la GENERATION WENGEE,Ilikua album kali sana hata leo itafute uisikilize utaelewa nasema nini sema bahati mbaya haikufanyiwa promo ya kutosha labda ndio maana haukupata kuisikia wala kuijua lakini ilipigwa congo nzima na katika ulimwengu mzima wa wazungumza lingala.

  Kuhusu JB kuwabania watoto JB utalipata ukimsikiliza kijana ERIC MENTE hapa chini,

  Je huyu nae kabaniwa?naomba jibu kwa mawerrasonique wote mshirikiane kulijibu hili.

 15. Richard Malewa says:

  Hiiiii hata aibu hamna eti alimtoa Aimelia? Aimelia alitoa hiyo ALBUM lini? Aimelia amekaa kwa Werra miaka mingapi? mpaka ameenda kuanzisha Bendi yake? Halafu tafsiri ya kijana nini ? Hivi utasema watu ambao walikuwepo kabla Wenge Kuvunjika ni Vijana wa JB Mpiana? Kwa hiyo Mzee Le Roy Naye ni Kijana wa JB MPiana. Kuhusiana na Aimelia toa kwenye Hesabu.

  Labda useme Mzee Werra amemfanya Aimelia ajitambue uwezo wake mpaka ameenda kuanzisha Bendi Yake. Tuseme Vijana ambao wametolewa na JB MPiana na Werrason baada ya Wenge Kutengana.

  Werrason Analeta Mambooooooo

  Analeta mamboooooooo hooooooooo MSICHOKEEEEEE!!!!!!!

 16. Hadj le Jbnique says:

  Mzee wa malewa kwani kwa ufahamu wako wewe Lyase anazo album ngapi?hiyo bendi unayoizungumzia kama kweli anayo maana mimi hata jina lake silifahamu ameianzisha mwaka gani?kama kitu hukifahamu ni bora ukauliza kwanza kwani hakuna mtu anaejua kila kitu pia mimi.Kiufupi mzee AIMELIA LYASE DEMINGONGO alitoka na solo album yake ya kwanza mwaka 2000 akiwa bado ndani ya BCBG,Na hii kumbuka ilikua ni mwaka mmoja baada ya album ya TITANIC kutoka 1999!….upo mpaka hapo au nimekuacha!
  Katika album hiyo AIMELIA alipata support kubwa sana kutoka kwa members wengine wa BCBG wakati huo,kasoro kwenye upande wa animation mnazoita “rap” au Atalaku alifanya THEO MBALA wa Big Stars ya LE GENERAL DEFAO MATUMONA enzi hizo,hata sijui yuko wapi huyu mtu last time alikua na mzee Benz Boozi Boziana.
  ALBUM hiyo ilienda kwa jina la CONSTAT,japo wengi waliifahamu kwa jina la GENERATION WENGEE kutokana na Kibao cha Generation wengee kilichomo humo kuzifunika nyimbo zote.Nyimbo nyingine humo ni:

  1:Constat
  2:Reve
  3:Juse et Bien
  4:Piece Rare
  5:Pathetique
  6:Bakake
  7:Lumiere
  8:La cle De L’an 2000
  9:Affection Kitchindja

  Halafu membership ya mtu kama AIMELIA,MPELLA,KALUDJI ndani wenge musica 4×4 inaweza kulingana na ya mtu kama JB,WERRA,PRINCE,MASELA n.k.hao kina Lyase walikuja hiyo wenge baadae sana mzee tena wakiwa ni vijana wa kina jb so hao ni vijana wao tu mpaka kufa.Una lingine?vipi kuhusu MENTE Mbona hujamzungumzia hata mstari mmoja?

 17. Richard Malewa says:

  Wewe acha urongo huwezi kumlinganisha Aimelia na Vijana kama akina Ferre hata kama alikuja baadae sana Wenge lakini ni ukweli Aimelia alishajenga jina ndani ya Wenge Origino. Ilikuwa na yeye aanzishe bendi yake baada ya kutengana kama walivyofanya wengine. Hata Mpela alikuwa na yeye awe na bendi yake.

  Kwa hiyo ondoa kabisa hilo wazo la Aimelia alitolewa na JB Mpiana. Na kama ulivosema wewe mwenyewe siyo lazima ujue kila kitu kwamba nani anafanya nini ila kwa taarifa yako habari ndiyo hiyo Aimelia baada ya kufundwa ujasiriamali na kujiamini mbele ya majukwaa naye ana bendi yake. Siyo na wewe ujue kila kitu. Siyo yeye hata Kabose yule aliyekuwa anatumika kwa Defao naye baada ya kupewa tutition ya ujasiriamali na kujiamini naye ana Bendi yake.

  Siyo wanamuziki wa JB Mpiana kutumika tu kama misukule yake!

 18. Stivin says:

  Nani kakudanganya kuwa JB alimtoa Aimelia? Aimelia ni kipaji lilichopelekwa Wenge na Werra, ndio maana baada ya kuona Werra kaondoka na maendeleo yake yako shakani akakimbilia Maison Mere! labda utaje mwingine kwa kweli, Huyo kijana uliemweka hapo sana sana anaiga sauti ya Ferre hana chochote kipya!

 19. Hadj le Jbnique says:

  Hebu kwanza mngeitafuta CONSTAT a.k.a. GENERATION WENGEE muisikilize vizuri ndio mtanielewa ninachozungumza,then twende sawa,maana hata kuisikia hamjawahi,so hatuwezi elewana,ila ukweli utabaki palepale Lyase alianza kutoka solo akia bcbg,lakini sisi kwa kua sio watu wa mayowe hatupigi kelele juu ya hilo na wala hatuhesabu,nilitaka tu kuwakumbusha kwamba hakuanza kutoka solo baada ya kutoka head office.Aimelia lyase sio kijana wa jb ila kabose kijana wa werra! kupenda kubaya,acha tu,Sasa hapo bwana malewa ndio unapochanganya taarifa,Aimelia Lyase unasema sio kijana wa Jb ila KABOSE BULEMBI eti ni mwanafunzi wa DE LA FORRET WERRASON! hivi unamjua Vizuri KABOSE kweli au ulifamfahamu baada ya kumuona hapo maison mere(head office) kwenu?ana tofauti gani na Alain Mpela ama Lyase Demingongo?yule mtu ana vipaji lukuki toka enzi za BIG STARS,yeye montana,theo mbala,unaweza mcheck hapo chini kwenye video akiwa katika matayarisho ya album yake “ELECTION” ambayo amemshirikisha pia ALAIN MPELA,steve nae anasema MENTE anaiga sauti ya FERRE,Steve unajua walikotoka MENTE na FERRE?nani anamuiga mwenzake?hii inanikumbusha hadithi ya Le Rambow Du Zaire Koffi na Felix Wazekwa ambao watu wa East Africa wengi mpaka leo wanaamini wazekwa anamuiga koffi!sitaki kuzama huko bwana ngoja niache muone mnavyoamini na si kuamini mnavyoona

  Msikie tena hapa uone kama kuna chocchote toka kwa de la forret hapo

 20. Hadj le Jbnique says:

  AFANDE MPELA + KABOSE BULEMBI,FIREEEEEEEEEEEEEEE!

 21. Anonymous says:

  Huo wimbo Generation WENGE uliupenda wewe, haukuhit kabisa! ndo maana akakimbilia kwa Werra baada ya kugundua kuwa bado hajaiva!

 22. Anonymous says:

  Unataka kunimbaia Ferre anamuiga Mente, acha utani, Fere ameingia Wenge 1997, na hiyo ndo sauti yake toka wakati huo! huyo Mente alikwina?

 23. Richard Malewa says:

  Sijaingia hapa muda kidogo lakini na wewe Hadji Le Jbnique uwe unatulizana na kusoma vizuri vilivyoandikwa siyo kukurupuka kama Anti -Terro! nimeandika vizuri kabisa alichopewa Kabose baada ya kutumika kwa Defao ni skills za Ujasiriamali na Kujiamini ndiyo maana naye anatoka kivyake. Sijasema kwamba ni zao la kulelewa na Mzee Werra Werra.lol.

  Ahaaaaa baada ya hii timu ya Motema Pembe kuja nimekumbuka rapping anayoimba mmoja wa Atalaku wa Werrason. Sikia hiii ninyi MaBCBGQUES

  Nani Motema Pembe ? Werrason Motema Pembe!
  Nani Motema Pembe? Werrason Motema Pembe!

  Motema Pembe ( Moyo Mweupe)

  Leeee leeeee leeeeee leeeeee leeeeeeeee!

  MALIZIENI WENYEWE NA CHUPI ZITAWABANA MWAKA HUUU NA KAMPUNDA KENU NINYI MaBCBGQUES!

 24. Anonymous says:

  Mpunda Imefulia mbaya! haina lolote, Mpiana kwishnehi! Mganga wae aliyekuwa anamsadia kashakufa!

 25. Hadj Le Jbnique says:

  OKEY BWANA MALEWA KAMA NDIVYO ULIANDIKA HIVYO KUHUSU KABOSE NI VEMA,PENGINE SIKUELEWA SAWASAWA NIKADHANI HIZO SKILLS U MEAN ALIZITOA HAPO HEAD OFFICE,NILISHINDWA KUSHANGAA MAANA KWA TAARIFA TU NI KWAMBA KABOSE BAADA YA BIG STARS YA G DEFAO KUPOTEZA MUELEKEO ALIMFUATA THEO MBALA ALIYETANGULIA KWENDA LE ANTI CHOC YA MZEE BOZI BOZIANA AMBAKO KABOSE ALISHIRIKI KUANDAA ALBUM MOJA YA BOZI,BAADA YA ALBUM HIYO NDIPO AKATIMKIA KWA WERRA THEN AKAANZISHA BENDI YAKE,JAMAA ANA VIPAJI LUKUKI IKIWEMO KUIMBA PIA NI MWEPESI SANA KATIKA KUCHEZA BILA KUSAHAU ANA KIPAJI CHA KUCHEKESHA(COMEDIAN)KAMA SUZUKII 4X4 JAPO HAJAPRACTICE RASMI AS SUZUKII ALIWAHI FANYA KWENYE TV SHOWS…NI HAYO TU NILIPENDA KUSHARE KATIKA TOPIC HII.

 26. werra ni mkali sana kuliko jb tukiangalia walipo gawanyika hadi leo werra ana sifa nyingi saaaaaaaaaaana kudhidi jb. concerts zao ni werra pekee aliye wahi kujaza maukumbi zote za ufaransa: zenith, bercy lakini jb hajawahi kujaza kumbi hizo pia album zao ni za werra tu ndio zinazopata sifa sana.kwa hiyo ukimlinganisha werra na jb utakuwa uja tenda haki linganisha jb na awilo,ferre,deplic sio werra. Werra huko juu saaaaaaaana kwa jb.

 27. Wonderful information and facts, excellent and useful style and design, as share excellent stuff with good ideas and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: