Kwa hili Simba mmechemka!!

Alipokuwa akiongea na wasaidizi wake katika semina elekezi Mh. Rais Dr. Jakaya alilaani kitendo cha kukalia habari na viongozi kukaa kimya pasi kuwatumia wasemaji wa wizara na idara za Serikali kujibu hoja au kutoa habari, Rais alijaribu kuonyesha umuhimu wa watu hawa katika dunia ya sasa ambayo upashanaji habari umebadilika kwa kasi.

Majuzi akikaririwa na vyombo vya habari mwenyekiti wa  Simba, Aden Rage ambaye alikaliliwa juzi na vyombo vya habari akieleza kuwa Ndimbo alikuwa sawa na karani, mtu wa chini, ni kauli ya kutotambua kile ambacho klabu hiyo iliridhia na kutekeleza kama agizo la Fifa, hivyo anapaswa kumwomba radhi msemaji huyo hata kama amejiuzulu.

Akiongea na wanahabari juu ya uamuzi wake wa kujiuzulu, Clifford Ndimbo alisema kuwa ameamua kujiuzulu rasmi wadhifa wake huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutopata ushirikiano wa kutosha baina yake na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.
Ndimbo amesema kwamba kama msemaji wa klabu hiyo ameshindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo kutokana na ‘siasa’ za klabu hiyo hivyo ameona ajiweke kando na kuendelea na mambo mengine.

Ndipo majuzi Mwenyekiti Rahe naye alijibu mapigo kwa kuongea na wanahabari na kukaririwa akisema Ndimbo alikuwa sawa na karani, mtu wa chini.

Inawezekana Rage asiyajue maazimio ya Fifa yaliyofikiwa mwaka 2006 huko Bagamoyo yakielekezwa kwa FAT kusiamamia vilabu kuwa na maofisa Habari, Katibu na Mhasibu wa kuajiriwa. Nachelea kusema hivi labda kipindi hicho Mh. Rage alikuwa akitumikia kifungo chake kabla ya kutenguliwa mwaka 2008 na Majaji Damian Lubuva, John Mroso na Mbarouk S. Mbarouk baada ya Mh. Rage Kukata rufaa ya hukumu hiyo ya miaka mitatu.

Inashangaza kidogo kwa kiongozi mkubwa kama Rage kutotambua umuhimu wala nafasi ya mtu kama Ndimbo, haiingii akilini hata kidogo.

Ndio maana kumekuwepo na mkanganyiko siku za karibuni katika habari toka vilabu hasa hivi vikubwa vya Simba na Yanga kwani kila mtu amekuwa msemaji na anasema lolote, Kwa mtindo huu ni kweli nafasi ya watu kama Ndimbo haiwezi kuonekana uhitaji wake.

Lazima Simba watambue umuhimu na uhalali wa nafasi ile au kama anaona ile anaiweza Zaidi aiache nafasi ya Uenyekiti na kuomba ya Afisa Habari. Na kabla hamjatangaza au kumsaili afisa habari mpya mpange nini mipaka yake na kumpa Job Descriptions ili kuondoa mambo ya aibu na kudhalilishana kama ilivyotokea.

11 Responses to Kwa hili Simba mmechemka!!

 1. Huyo rage inabidi amuombe radhi ndimbo na pia awaombe radhi makalani kwa kudharau kazi zao says:

  Spoti na starehe

 2. Jordan says:

  Mi nakwambia kila siku uwe unaandika Makala, napenda sana ukichambua kitu, acha uvivu Piua andika.
  Soma email yako nimekuandikia kitu.
  Jordan

 3. mukulumba says:

  Huyo aliyekua afisa habari yeye mwenyewe kashindwa kazi,hakuyajua majukumu yake sawasawa,yeye alidhani afisa habari kazi yake ni kuongea na waandishi wa habari tu basi,hakujua kwamba yeye ndio aliekua responsible kuishughulikia web site ya club na kuweka update matokeo yake kazi hiyo imekua ikifanya na mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya simba bwana ibrahim masoud maestro mtangazaji wa clouds redio and tv station.Halafu kitu kingine jamaa alionyesha upeo mdogo ile mbaya pale alipotoa press release ya kuacha kazi simba kabla ya kuandika barua rasmi ya kufanya hivyo kwa uongozi!!hii sijawahi kuona popote,ndio maana akampa nguvu isiyo na sababu ADEN kumtoa akili,halafu kingine alichochemsha mchizi ni kuandika barua ya kuacha kazi kwa njia ya e mail!hii nayo mimi sijapata kumuona mtu yeyote zaidi yake akifanya hivyo..nani amewahi kuona ama kusikia hii kabla ya huyu bwana kufanya hivyo?kiufupi dogo alichemka mbaya akubali tu yaishe kwa maslahi ya simba,hii inanikumbusha habari ya kaijage wa tff yule msemaji alieshindwa kutimiza wajibu wake na kusababisha mh.rais ahadhirike pale national stadium kisa eti alienda kutoa photocopy na kuacha kusimamia majukumu yake,leo nae analalamika na wandishi wenzake nao kwa kumpenda kupita kiasi wanaandika makala ndeeeefu kumtetea kama tunavyoona kwa huyu aliyekua msemaji wa mnyama.

 4. Nice information, outstanding and important style, as share great stuff with fantastic thoughts and concepts.

 5. A few things i have constantly told men and women is that when you are evaluating a good on the net electronics retail outlet, there are a few issues that you have to take into account. First and foremost, you should really make sure to locate a reputable plus reliable store that has enjoyed great evaluations and classification from other consumers and industry leaders. This will make certain you are getting along with a well-known store to provide good services and aid to the patrons. Many thanks for sharing your thinking on this website.

 6. Appreciating the hard work you put into your blog and detailed information you provide. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed information. Wonderful read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

 7. Thanks for the marvelous posting! I seriously enjoyed reading it, you will be a great author.I will make sure to bookmark your blog and definitely will come back someday. I want to encourage yourself to continue your great posts, have a nice morning!

 8. At this time it appears like Movable Type is the preferred blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

 9. Appreciating the time and energy you put into your blog and detailed information you present. It’s nice to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed information. Wonderful read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: