Wafah Dufour Bin Laden, Mtoto wa kaka yake Osama Bin Laden anayeng’ara kwenye Ulimbwende

Wafa Dufour Bin Laden

Huku Dunia ikiwa inatawaliwa na habari pamoja na matukio yaliyoambatana na kupatikana na hatimaye kuuwawa kwa gaidi nambari moja Dunianiani (kwa mujibu wa CIA), Basi sisi Spoti na Starehe tunajaribu kuiangalia familia hii ya Osama Bin Laden katika kona nyingine ya kiburudani zaidi.

Pichani juu anaitwa Wafah Dufour ila jina lake kamili ni Wafah Dufour Binladin akiwa ni binti wa kaka yake Osama Bin Laden ambaye yeye na wazazi wake walikuwa wakiishi huko Calfornia-Marekani ambako walilowea.

Wafah ni mtoto wa kaka yake Osama anayeitwa Yeslam bin Ladin, Osama na Yeslam ni baadhi ya watoto 54 wa Mohammed bin Laden raia wa Yemen aliyeamia Saudi Arabia na kulowea huko ambapo alijiendeleza na kufikia kuwa ni mmoja wa makandarasi wakubwa. Mama yake anaitwa  Carmen bin Ladin ambaye ni raia wa Iran amechanganyika na Mswiss.
 
Wafah Dufour aliishi Los Angeles Calfornia katika utoto wake na baadaye Jeddah, Saud Arabia lakini baadaye alihamia Geneve Switzerland akiambatana na wazazi wake na wadogo zake wawili wa kike Nadjia na Noor. Mnamo mwaka 1988, wazazi wake walitengana na baadaye waliachana (divorced) mwaka 2006. Inasemwa kuwa Wafah hajawahi kuongea na baba yake wala wadogo zake tangu akiwa na miaka 15.

Kabla ya September 11 alikuwa ni mtoto wa kawaida na ambaye alitumia jina lake bila ya wasiwasi kama mtu mwingine, hali ilibadilika ghafla baada ya Sep 11 ambapo jina la Bin Laden likawa ni kama nuksi kwake ndipo alipoamua kubadili jina na kutumia ubini wa mama yake na kujiita Wafah Dufour.  “Siwezi kubadili ukweli kuwa ni hawa ni ndugu zangu na yule ni ndugu wa baba yangu, lakini pale inapokuja jina linahusishwa na ugaidi tena ambao umeua Wamarekani wenzangu, hapo ndio naliona jina mzigo” Alisema Wafah alipofanya mahojiano na jarida la GQ.

...

Kama watoto wengine Wafah naye alijifunza kutunza Koran akiwa na miaka 10 hukohuko CAlfornia Marekani, Wazazi wake walihamia Switzerland yeye akiwa binti mdogo.

Alipokuwa akaanza kuwa na mapenzi ya kufanya uanamitindo na muziki jambo ambalo alilifanikisha, mwenyewe anasema zamani aliishi vizuri sana na kwa uhuru ila baada ya tukio la September 11 la kigaidi jina la baba yake liliona chungu kwani alinyoshewa kidole kila anapopita.

“Nimezaliwa Amerika, nataka watu wajue mimi ni mmarekani, pia wajue mimi ni kama raia wengine wa Marekani, kwangu mimi Amerika ndio nyumbani” alisema Wafah alipoongea na jarida la GQ.
 

...

 
Baada ya tukio lile la Word Trade Centre kupigwa mabomu Wafah alikuwa America na anasema ilibidi ajifungie ndani kwa miezi 6 bila kuongea na watu, “nilipatwa na msongo wa mawazo (depression} na wakati mwingine kutamani hata nipotee kabisa”.  Wakati wa tukio la September 11 Wafah alikuwa na mkataba mzuri wa kazi lakini kila kitu kilifutika, pamoja na kuwa na MAster Degree ya Sheria lakini bado kwa ubini wa BinLAden asingeweza kuajirika, ingawa bado alikuwa ni mwanafunzi wa  New York’s Columbia Law School.
HApo ndipo idea ya kubadili jina ilipokuja na kuamua kubadili fani na kujikita kwenye Ulimbwende na Muziki ndipo alipokutana na jarida la GQ ambalo anasema lilimtoa.
 
Picha zile zilileta mtafaruku na kufanya aandamwe sana na vyombo vya habari kwani kwa kuzingatia anatoka kwenye familia yenye msimamo mkali wa kidini na yeye kupiga picha za nusu utupu. Kwa upande mmoja hii ilimbeba na kumpandisha chati sana kwenye fani yake.
Binafsi anasema anapenda kufanya kitu ambacho moyo wake unapenda na kamwe kisihusishwe na dini yake, bado imani yake ipo pale pale ila ni yeye anajua anachokifanya.
 

...

 
Kwa sasa Wafah ni mwanamitindo na mwanamuziki ambaye tayari amesharekodi nyimbo zake kadhaa zilizo kwenye mahadhi ya Pop!. Amejizolea umaarufu huku akifananishwa na Angeline Jolie kwa midomo yake. Kwa sasa Wafah anaishi London Uingereza na yuko kwenye mipango ya kujiunga na Bendi maarufu ya Rock Black Lips.
 
Habari hii ni kwa mujibu wa mitandao na jarida la GQ, Picha na GQ
 

2 Responses to Wafah Dufour Bin Laden, Mtoto wa kaka yake Osama Bin Laden anayeng’ara kwenye Ulimbwende

  1. hermosa seo says:

    I have added your page to my Google Plus bookmarks I was reading your posts while walking my dog.

  2. Reasonably sure he’ll possess a fantastic study. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: