Vodacom Shuffle Dance kuvunja rekodi ya Dunia?

 

Picha kwa Hisani ya Michuzi

 Pichani ni washiriki wa Vodacom Shuffle Dance, Tamasha lililofanyika kwenye ufukwe wa Sunrise Beach jana jumamosi.  likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea Duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.

Spoti Starehe ilishuhudia mamia kwa maelfu ya watu wakivuka kuelekea Kigamboni ambako kulikuwa na Tamasha hilo, hata hivyo uwezo wa Kivuko kubeba magari 60 tu kwa kivuko kikubwa na kidogo magari 16 kwa wakati mmoja kilikwaza watu wengine ambapo foleni ya kuvuka kwa jana ilifika hadi karibu na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

“Naimani kabisa kama wote wale wangefanikiwa kuvuka basi hapa watu wengi zaidi ya hawa wangekuwepo” alisema Mngoya mmoja wa washiriki kwenye Tamasha hilo.

Kwa mujibu wa Waandaaji na mtandao wao mpaka kufikia jana zaidi ya watu 500 walikuwa wamejiandikisha kwa ajili ya Tamasha hilo.

Video ya juu kabisa inaonyesha jinsi watu wakicheza Muziki wa Vulindela kwa style ya jana.

 

One Response to Vodacom Shuffle Dance kuvunja rekodi ya Dunia?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: