Kwa hili Simba na Yanga mmechemka.

April 5, 2011
Mkereketwa wa Simba Mudy Wandy akijifariji kupiga picha baada ya kushuhudia timu yake imelala 3-2.

Mkereketwa wa Simba Mudy Wandy akijifariji kupiga picha baada ya kushuhudia timu yake imelala 3-2.

Shabiki akiwa amevalia bango lenye maandishi TP Mazembe 6-0 Simba.

Shabiki akiwa amevalia bango lenye maandishi TP Mazembe 6-0 Simba.

Majuzi tulishuhudia mchezo baina ya Simba na TP Mazembe, Mchezo ulikuwa muhimu sana kwa Simba kushinda ili iweze kwenda mbele mwa michuano hii.

Kuna vitu vingi vinavyoiwezesha timu kushinda mbali na uwezo wa wachezaji, ujumla wa timu ( team spirit), maelekezo ya Kocha na kuusoma mchezo kwa kuiangalia timu husika, pia utayari wa kisaikolojia unahitajika ili kuweza kushinda.

Hapa naomba niyaache yooote ila nataka niongelee nafasi ya mashabiki katika saikolojia ya wachezaji. Ni wazi kuwa mashabiki wanachangia sana kuwapa hari wachezaji. Kwa kulitambua hilo ndio maana kwenye michezo muhimu inafikiaga hata mashabiki wanaruhusiwa kuingia bure ili mradi walete chachu ya usindi.

Hali haiko hivyo kwa vilabu pinzani na watani wa jadi vya simba na yanga. Kwani utani na upinzani wao umeenda hadi kufikia hawana uzalendo wala utaifa kabisa. Majuzi wakati Yanga wanakabiliana na Dedebit ya Ethiopia mashabiki wa Simba walivaa jezi za Dedebit na kuishangilia Dedebit dhidi ya Yanga.

Masikini Simba hawakujua au walisahau kuwa wangewahitaji mashabiki wa Yanga kwenye mchezo wao muhimu takribani siku kadhaa baada ya mchezo wa Yanga na Dedebit. Jambo ambalo kweli Yanga wamelipiza kwa kuzinunua kwa wingi Jezi za TP Mazembe na kuishangilia kwenye mchezo wa Juzi Jumapili uwanja wa Taifa.

Huu ulikuwa mchezo muhimu sana kwa Simba kushinda ili iweze kusonga mbele. Washabiki wa Yanga tangu mitaani walikuwa wakiwazodoa wenzao wa simba kuwa wasingeweza kushinda. Kisaoikolojia Simba ilianza kushindwa kuanzia mitaani kwani mashabiki wa Yanga walichokuwa wakifanya ni kukusanya data za TP Mazembe na kuwatishia mashabiki wa Simba ambao wengine walikata tamaa hata kabla ya mchezo.

Kuna wakati timu hizi zilikubaliana kushangiliana hasa kwenye mechi za Kimataifa, lakini mkataba huu umekuwa wa viongozi zaidi bila kushuka kwa mashabiki. Ambao kwangu mimi naona inabidi wahamasishwe juu ya uzalendo huu. Tulihitaji kuziona timu zetu zikishiriki kwenye mechi za kimataifa ndio fahari yetu, haya zote zimetolewa kwa faida ya nani sasa?

Badilikeni washabiki, mwisho wa siku soka letu halitakuwa.

Posted with WordPress for BlackBerry.