Waoooooo baba!!

February 17, 2011
Advertisements

Kila Kinyozi ana Kinyozi wake; Arsenal yainyoa Barca

February 17, 2011

Nakupa Dozi ya “Aspirine” yakwake Koffi Olomide

February 17, 2011

Kuna wanamuziki wachache sana wenye uwezo wa kuimba wimbo mmoja mwanzo hadi mwisho na bado wakakuacha unatamani kuendelea kuusikiliza. Kama unakubaliana na mimi basi Koffi ni mmoja wapo, Wataalamu wa muziki wanasema Koffi anazaidi ya sauti saba ambazo anaweza kucheza nazo akiaanzia kuimba sauti ya chini sana ama ya bass sana.

Hii ni strength kubwa ya Koffi na ndio maana amekuwa akifanikiwa sana kwenye nyimbo zake kwani pale ambapo anataka uimbe kama ye anavyotaka ukishindwa basi anapanda mwenyewe.

Huu ni mmoja ya nyimbo zake za Rhumba ambazo zilitokea kupendwa na kila unapopigwa mwili wangu husisimuka sana. Vijana wengi ambao walitoka kwa mwamba huyu walifanikiwa kimuziki na wamekuwa moto wa kuotea mbali kwenye game nzima ya Muziki.


Nahodha wa AC Milan Gattuso aomba radhi

February 17, 2011

Nahodha wa AC Milan Gennaro Gattuso ameomba radhi kwa kumpiga kichwa kocha wa Tottenham Joe Jordan, baada ya timu yake kulazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa timu 16 kuwania ubingwa wa Ulaya.

Gattuso akimkaba koo Joe JordanGattuso akimkaba koo Joe Jordan

Gattuso anayechezea pia timu ya taifa ya Italia, alizozana na Jordan mwenye umri wa miaka 59 na baadae akamsukuma kichwani.

Nahodha huyo wa AC Milaa mwenye umri wa miaka 33 ambaye siku za nyuma aliwahi kuichezea klabu ya Rangers ya Scotland, anasubiri kuadhibiwa kutokana na vitendo vyake vya utovu wa alivyoonesha uwanjani.

“Nilishindwa kujizuia,” alisema Gattuso, ambaye awali alimsukuma Jordan usoni. “Hakuna kisingizo kwa niliyoyafanya. Nabeba lawama zote kwa yote hayo.” Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: