“Wapenzi wangu naweni mikono, chakula tayari” Solo Thang

Travellah Kazini

Mwanamuziki Msafiri kondo aka Solo Thang aka Travellah aka Msafiri amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani albamu yake itakuwa tayari hivi kkaribuni.

Solo Thang aliyasema hayo alipooongea nami leo hii kuhusiana na albamu yake ya Traveller ambayo iko kwenye hatua za mwisho za umaliziaji.

Aidha Solo amesema kuwa Albam hiyo yenye nyimbo 14 itakuwa sokoni kuanzia February.

Travellah Mwenyewe

Solothang alisema kuwa ameshirikisha wanamuziki kadhaa kwenye Albamu yake hiyo ikiwa ni mchanganyiko wa vichwa vya zamani kama Chidy, Jay Moe na Mfalme wa Wasukuma Fid Q, ” Kuna kazi nimefanya na CHIDY inaitwa VIINIMACHO..kuna nyingine na FID..Inaitwa AIRBUSS na moja nimefanya na JAYMOE inaitwa Family” alisema Solo Thang.

Nyimbo zote hizi  zitakua kwenye album…Video moja nimefanya ..nyimbo inaitwa ALL I NEED,ndio nipo kwenye mipango ya kufanya nyingi zaidi..nadhani baada ya mwezi nitakua na Video mpya hewani na album itakua inapatikana Online” Aliongeza Solo Thang.

Msafiri Kondo aka Traveller aka Msafiri aka Solo Thang ni mmoja wa wanamuziki ambao walijizolea umaarufu sana enzi za mwanzo za muziki wa Bongo Flava na pia ni kati ya wanamuziki wachache wa kizazi kipya mwenye elimu ya kutosha akiwa na Diploma ya Diplomasia toka Chuo cha Diplomasia na Kisha kuendelea na Degree nchini Uingereza na pia ameshasoma kozi mbalimbali.

Advertisements

2 Responses to “Wapenzi wangu naweni mikono, chakula tayari” Solo Thang

  1. Anonymous says:

    Lamaaa nakufeel sana mkurumba

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: