Ferre Gola ft Heritier Watanabe – Nostalgie

January 16, 2011

Kiukweli namkubali sana Ferre Gola mi nilimsikia kwa mara ya kwanza kwenye live ya Wenge BCBG aliimba kipande cha Mpela kule Belgium siku nyingi baadaye alipotea hadi pale Werasson alipoanza kumpa nafasi tena.

Sikiliza hii kitu inaitwa Nostalgie aliyoipiga akiwa na WMMM akiwa na kifaa kingine kinatwa Heritier Watanabe, hawa vijana ni balaa. kiukweli Werasson alikuwa na haki ya kumlilia Ferre Gola ambaye kwa sasa anafanya vizuri sana kwenye ulimwengu wa muziki wa Congo.

Ferre na vijana hawa wanaokuja juu kwa sasa inasemwa ndio kizazi cha nne cha mageuzi ya muziki wa Congo. Baada ya kizazi cha nne kilichotamba cha akina JB mpiana, Werasson na wengineo.

Jumatatu njema wadau

Advertisements

Sulley Muntari kachoshwa na Inter Milan

January 16, 2011

Mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Ghana, Sulley Muntari, anajiandaa kuihama klabu ya Italia ya Inter Milan.

Sulley MuntariSulley Muntari


Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Italia, Marco Branca, ameeleza kupitia televisheni ya nchi hiyo, kwamba Muntari mwenye umri wa miaka 26, amekwishawasilisha maombi ya uhamisho.

Enzi za Jose Mourinho, Muntari alikuwa anakaribia kupewa nafasi ya moja kwa moja ya chaguo la kwanza, katika msimu wake wa kwanza na Inter.

Hata hivyo, Muntari alipoteza nafasi yake katika timu hiyo msimu uliopita na msimu huu amecheza mara chache.

Mchezaji huyo wa zamani wa Portsmouth, amecheza mara 12 katika mashindano yote na zaidi akiwa mchezaji wa akiba.


%d bloggers like this: