Arsenal yagawana pointi na Wigan 2-2, Chelsea yaona mwezi

December 30, 2010

Arsenal imelazimishwa kwenda sare na Wigan ya magoli 2-2.

Wigan wakicheza nyumbani ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Arsenal kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Ben Watson katika dakika ya 18.

WatsonBen Watson

 

Arsenal walikuja juu ya kulisakama lango la Wigan na kuppata mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 39 na 44, kupitia Andrey Arshavin na Niklas Bendtner.

Wakiwa wanaelekea kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuizaba Chelsea, Arsenal walijikuta wakienda sare baada la mlinzi wa Arsenal Sebastian Squillaci kujifunga, zikiwa zimesalia dakika tisa mpira kumalizika.

SquilacciSebastian Squilacci alijifunga

 

Kwingineko Chelsea ilizinduka na kupata ushindi wake wa kwanza baada ya michezo saba, kwa kuifunga Bolton bao 1-0.

Bao hilo pekee lilifungwa na Flourent Malouda katika dakika ya 61.

MaloudaFlourent Malouda

 

Liverpool nayo ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Wolves ambao wako mkiani.

Bao hilo pekee lilifungwa na Stephen Ward katika dakika ya 56.

Liverpool ilishindwa kuonesha cheche zake licha ya nahodha Steven Gerrard kurejea uwanjani.

Wolves wamepata ushindi huo kwenye uwanja wa Anfiled ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 26.

LiverpoolLiverpool wamefungwa kwao

 

Ushindi wa Chelsea umeipeleka timu hiyo hadi na fasi ya nne, juu ya Tottenham. Arsenal imesalia katika nafasi ya tatu, huku Manchester City ikiwa nafasi ya pili na Manchester United katika nafasi ya kwanza, licha ya kuwa pointi sawa na City.

 

Advertisements

Jela kwa kushambulia wachezaji wa Togo

December 30, 2010

Na BBC Michezo

Mahakama moja nchini Angola imemhukumu kwenda jela miaka 24 mtuhumiwa wa shambulio la timu ya taifa ya soka ta Togo, mwezi Januari.

Cabinda

Cabinda, Eneo ambalo mauaji yalitokea

 

Mtuhumiwa huyo ni Joao Antonio Puati. Wakili wa mtuhumiwa huyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa alikutwa na hatia ya kufanya “uasi kwa kutumia silaha”.

Basi lililokuwa limebeba timu hiyo, lilishambuliwa katika jimbo la Cabinda, wakati wachezaji hao wakielekea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

JenezaJeneza la mmoja wa maafisa waliouawa wa Togo

 

Bw Puati alikana mashitaka hayo, na amekanusha kuhusiana na kundi la waasi ambalo lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Mtu mwingine, Daniel Simbai, alifutiwa mashitaka kama hayo, yaliyokuwa yakimkabili.

Alikuwepo

Maafisa wawili wa Togo waliuawa, katika shambulio hilo lililodumu kwa nusu saa, ambalo kundi la waasi la Flec linadai kuhusika nalo.

“Joao Antonio Puati alikuwepo katika eneo la tukio, na uhusiano wake na Flec umeonekana wakati wa kesi,” amesema mwendesha mashitaka mkuu wa Cabinda, Antonio Nito, wakati akizungumza na AFP.

Mwandishi wa zamani wa BBC nchini Angola Louise Redvers amesema mawakili wa upande wa utetezi wamekata rufaa katika mahakama kuu.

CabindaEmmanuel Adebayor akipozwa na mchezaji mwenzake

 

Wamesema ushahidi wa uhusiano na kundi la Flec haukuoneshwa wakati kesi ikiendeshwa, bali ulitokana na taarifa za polisi zilizochukuliwa kutoka kwa Puati wakati akiwa kizuizini.

Wakili wa utetezi Arao Tempo ameiambia BBC kuwa mteja wake aliteswa wakati akiwa jela la kulazimishwa kukiri kuwa anahusiana na Flec.

Kisiasa

Amesema uamuzi wa kumhukumu Bw Puati ambaye ni raia wa Kongo-Brazzaville, na kumuachilia huru mtuhumiwa mwenzake ambaye ni raia wa Angola, ni wa kisiasa.

Amesema hukumu hiyo ni kupeleka ujumbe Kongo-Brazzaville, ambako waasi wengi na wafuasi wa Flec wanaishi na kufanya shughuli zao.

Gerezani

Wiki iliyopita, wanaharakati wanne wa haki za binaadam waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo la mwezi Januari, waliachiliwa huru kutoka gerezani.

Makundi ya haki za binnadam yameituhumu Angola kwa kutumia shambulio dhidi ya timu ya Togo, ili kuhalalisha msako dhidi ya wakosoaji wa serikali katika jimbo la Cabinda.

Flec imekuwa ikipigana kwa miongo mitatu kudai uhuru wa Cabinda, eneo ambalo linatenganishwa na Angola kwa kipande kidogo cha ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Licha ya eneo hilo kuwa na utajiri wa mafuta, ni moja ya maeneo masikini zaidi nchini Angola.

 


%d bloggers like this: