Dis Moi Amour; “Niambie Mpenzi wangu toka kwake JB Mpiana

December 15, 2010

Wimbo huu unapatikana kwenye album ya TH ambayo JB Mpiana aliitoa akisema yeye ni Mnyenyekevu Daima, akisema kuwa wanatakiwa kuwapa burudani washabiki na si maneno, ikiwa ni kijembe kwa mkongwe Werrason ambaye kwa wakati huo alionyesha kujibu kila Albam ambayo JB Mpiana alikuwa akiitoa, na hapa lilikuwa ni jibu kwa albamu ya Solola Bien.

Advertisements

Kambi Ya Giraffe Unique Model Yazinduliwa Rasmi

December 15, 2010

Washiriki wa shindano la Giraffe Unique Model 2010 wakiwa pamoja na mratibu wao, Bw. Magese (katikati) wakikata keki kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa kambi yao katika afla fupi iliyofanyika jana katika hotel ya Giraffe Ocean View jijini Dar es salaam.Shindano hilo linatazamiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu katika hoteli hiyo ya Giraffe.


Makhirikhiri kutumbuiza Land Mark Hotel ijumaa hii.

December 15, 2010

...

Wanamuziki maarufu wa Makhirikhiri chini ya kinara wao Shumba Ratshega ‘Tajiri Mtoto’ watafanya maonyesho matatu mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ujio uliowezeshwa na Klabu ya Lufita ya Tabata.

Siku ya Ijumaa Makhirikhiri watatumbuiza katika ukumbi wa Land Mark Ubungo. Kwa mujibu wa taarifa ya waandazi kiingilio kitakuwa Tsh. 20,000/- huku kukiwa na maonyesho mengine mawili zaidi tarehe 18 na 19.

Makhirikhiri waliwahi kuja TAnzania kwenye ziara ambayo iliwachukua zaidi ya miezi miwili, ziara ambayo haikuwa na mafanikio sana kama ilivyotazamiwa labda kutokana na matangazo machache kipindi walipokuja.

Wakifanya vitu vyao huko Iringa walipokuja hapo awali.


%d bloggers like this: