Newcastle yamtimua meneja wao Hughton

December 7, 2010

Klabu ya Newcastle United Football imetangaza kuachana na meneja wake Chris Hughton. Pia kocha wa walinda mlango Paul Barron naye anaondoka katika klabu hiyo.

Chris HughtonChris Hughton

 

Bodi ya klabu hiyo imesema inamshukuru Chris kutokana na jitahada zake wakati wa kipindi cha mpito kutoka ligi ya Championship na kurejea katika Ligi Kuu ya England. Read the rest of this entry »

Advertisements

Vermaelen kurejea uwanjani mwakani

December 7, 2010

Mlinzi wa kati wa Arsenal Thomas Vermaelen, hawezi kurejea uwanjani hadi mwakani kutokana na maumivu yanayomkabili ya nyama za misuli ya mguu.

Thomas VermaelenThomas Vermaelen

 

Vermaelen mwenye umri wa miaka 24 hajacheza soka tangu alipoumia tarehe 7 mwezi wa Septemba, alipokuwa akiichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji, katika mchezo wa kuwania ubingwa wa Euro kwa mwaka 2012 nchini Uturuki. Read the rest of this entry »


Likama ya Wenge Musica Maison Merre

December 7, 2010

Niliipenda sana albam ya Solola Bien ya Werasson na Wenge Musica Maison Mere (WMMM) inawezekana labda kwa sababu bado hapa alikuwa na waimbaji wengi wa iliyokuwa BCBG wakati huo.

Huu wimbo wa Likama unanikumbusha rafiki yangu Big Prodyuz Maghambo  aka Muzee ya Pamba, huyu jamaa alikuwa anaupenda sna huu wimbo na siku kapata hii Albam kupitia kwa Patcho Mwamba wa FM Academia alinitumia Malaysia kwa DHL ili niusikilize huu Wimbo wa Likama.

Maghambo huo uliko kaka heshima kwako nimekukumbuka sana na huu wimbo ni kwa ajili yako papaa.

Merci mingi.


Kuimbwa gharama bwana!!

December 7, 2010

Hii ni Compilation ya mwanadada Sophia wa Kessy na ni jibu la mdau wangu Moris wa Mererani kama ulivyoniomba nikwambia nani ni nani kwenye nyimbo za Congo, nakujibu swali lako mkuu.

Sio jambo geni kusikia majina ya watu mabali mbali yakitajwa kwenye nyimbo, angalia hapa utajua

 

CHIEF DIDI KINUANI LE MILLIONAIRE

Didi Kinuani ni mfanyi biashara mkubwa sana huko paris na hata kongo katika nyimbo nyingi hata za hapa nyumbani pia unaweza kumsikia amiwa ameibwa amekuwa mfano wa kuigwa huko kongo kwa kuchangia si tu secta ya muziki lakini pia hata ma hospitali na hata kufikia hatua ya kununua vyo mbo vya muziki kwa kuwagaramia na wakati mwingine kuwasafirisha wanamuziki wa kongo barani ulaya na kuwatangaza kupitia kampuni yake ya group de kin.

 

ZADIO CONGOLE aka ZK aka ZADIO BEECEEBEEGEEQUE

Zadio Congole, huyu pia ni ‘mpigaji” ambaye alifaikiwa kupata pesa anaishi huko Ubelgiji (shengheni kwa ujumla) na ni mshabiki mkubwa wa JB Mpiana ambaye kwa kiasi kikubwa amejitolea pesa na muda katika bendi hii, Zadio ndiye mfadhili mkubwa wa show za JB Mpiana na amejizolea umaarufu kupitia muziki huku JB akiwa ameshamtungia nyimbo takribani tatu mpaka sasa huku wimbo wa Zadio au ZK ambao unapatikana kwenye album ya Quel Est Ton Probleme.

 

TABOU FATOU aka TABOU FATOU TOP MODELLE

Mwanamuziki Faustin Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa Di Caprio, Album yake ya “Droit Chemin” ndiyo Album bora ya Mwaka 2007/2008, Albamu hiyo  iliuza sana takribani miaka miwili mizima. katika Album hiyo kuna wimbo unaitwa “Liputa” kwenye huo wimbo amededicate kwa Taboo Fatou ” Mama na Compressor”(pichani), huyu ni Mfanyabiashara Mrembo anaishi Belgium, ana miliki maduka kadhaa ya Nguo huko Paris(France) na Beligium,na inasemekana zile Pamba zote za Fally, Taboo Fatou ndiyo anamvalisha, kwa wale wapenzi wa JB Mpiana watumbuka katika Album yake ya Kwanza(Solo) Feux D’Lamour,kuna wimbo unaitwa “Top Model” utampata humo Tabu Fatou.

MERE MALOU “MADAME YA POTO”

Marehemu Mama Mere Malou akiwa na Papa Wemba enzi hizo, Hawa waliwahi kuwa wapenzi.

Pichani juu ni Marehemu Mama Mere Malou “madame ya poto“ akiwa na Papa wemba enzi hizooo Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa, Pia Mere Malou ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mwanamuziki  Wemba.

 

 

Waombolezaji wakiwa na Papa Wemba siku Mama Mere Malou alipofariki

 

ZACHARIE BABABASWE

 

...

Zakari bababaswe mmoja wa ambao pia mie nawakubali waliochangia pia kutagaza vipindi vyao kutokana na interview za DVD ambazo amekuwa akitengeza na kuuza ulaya lakini pia kupitia kipindi cha lingala facile amekuwa akifanya mambo ma kubwa kwa sasa .
Tchacho Mbala
TCHACHO MBALA
Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo. Shukrani kwa Big Producer Maghambo.
WAPO WENGI SANA KAMA KINA KASHOGII, KINA YAKUZA DEBS,Boris Bondo, Bebee Ramadhani, Papito Mbala, Zamalenga, Cedric Okitundu, apokalips Bella na USA, na wengine wengi ambao sijataja majina yao i hope umewasikia sana na umekuwa ukijiuliza kwanini wanaibwa ingawa mwisho wa siku kwa namna moja ama nyingine nathubutu kusema jamaa hawa wanamchango mkubwa na wamesaidia sana kuutangaza muaiki wa Congo ulaya na kwingineko africa wamekuwa wakiwatunza wanamuziki na kuwapa suport .
Hapa nyumbani pia watu kama hawa wapo wengi sana nitakuletea picha zao na kile wanacho kifanya muda si mrefu na nikiwa na imani na wao pia bado wanayo nafasi ya wakishirikiana na wanamuziki kuutangaza muziki wetu wa Tanzania nje ya Tanzania tukishirikiana nao kama wadau wa sekta ya burudani kwakuwa miongoni mwao ni wafanya biashara wakubwa na maarufu na wana uwezo wa kusuport vijana wa kitanzania kwa kila namna.

%d bloggers like this: