Mitumba : Kipindi kwenye “Al jazeera” kilichoibua ufisadi nyuma ya Pazia ya Misaada.

December 6, 2010

 

Ni Hadithi ya ukweli ambayo inahadithiwa na muandishi wa Aljazeera ambaye aliamua kufuatilia uongo na ukweli kuhusu michango inayotolewa na wazungu kwa nchi zinazoendelea na kwa safari hii aliamua kufuatilia misaada ya Nguo ambayo baadaye hugeuka kuwa biashara ambayo sio tu inanufaisha wazungu, la hasha bali pia waafrika wenyewe kwa njia moja ama nyingine.

Kwenye Video ambayo inaonyesha Fulana iliyochangwa na kijana huko Ulaya na kupitia mikono mingi kabla ya kumfikia muuza mitumba huko Iringa na hatimaye kutua kwa kijana mdogo ambaye ana ndoto ya kuja kuwa mchezaji mpira maarufu.

Safari ya Fulana hii ni ndefu zaidi ya Kilomita 10,000 huku ikikata  mbuka kwa kutumia usafiri wa aina tofauti tofauti.

Kwa wapenzi wa vipindi vya Al Jazeera watakuwa wakikijua kipindi hiki cha Witness ambacho kinaambatana na habari za kiuchunguzi ambapo mwandishi hupewa au kuamua kufuatilia kitu ambacho ama kina utata au ni kwa faida ya watazamaji kwa ujumla.

Unapoongelea nguvu na uwezo wa Mtu anayeitwa Muandishi wa habari ni kwa tukio kama hili, yapo mengi ya kujifunza lakini huenda basi ukabakiwa na maswali mengi kuliko majibu, kwani kama ulidhani mafisadi ni sisi tu la hasha.

Advertisements

Mganda ashinda Tusker Project Fame 2010, Msechu wa Pili

December 6, 2010

Washiriki wakiwa wamejipanga kwenye Nusu Fainali wiki iliyopita

Muwakilishi pekee wa Tanzania Peter Msechu ameibuka mshindi wa Pili baada ya kupambana vilivyo mpaka fainali.

Msechu ambaye alipewa nafasi kubwa kushinda alikuwa akishangiliwa kila alipopanda jukwaani na kwa siku ya jana alitumbuiza na Kidumu ambaye walirandana vilivyo.

KAtika kutumbuiza mmoja mmoja Msechu aliimba wimbo wa “Nipate Nafasi” sina hakika na jina la wimbo ambao uliimbwa na Kilwa Jazz ambapo aliuongeza vionjo vyake na kumsifia mtoto Juliana ambaye anasema tangu aende Kenya alitokea kumpenda lakini alishindwa kusema na ameamua kumwambia mbele za watu, “…Juliana naumiaaaaa” ndio ilikuwa chorus ya wimbo huo na mashabiki wote waliibuka kwa furaha na mayowe.

Baada ya kumaliza Msechu aliulizwa na Jaji Juliana “…Msechu ni Juliana yupi huyo unayemzungumzia?” aliuliza Juliana huku akiwa ameweka shingo upande na kuonyesha kuguswa na ujumbe wa Msechu, kwa kijiamini Msechu alijibu ni Wewe jibu lililofanya Jaji Ian alipuke kwa kicheko.

Zitto amtumia Salamu za pongezi

Mwanasiasa kijana Zitto Zubeir Kabwe alikuwa mmoja wa watu walionyesha furaha zao kwa hatua ambayo MSechu amefikia na kumpongeza. “Hongera sana MSECHU” ilisema statement ya Facebook ya mwanasiasa huyo jana usiku huku ikifuatiwa na watu mbali mbali chini yake kutoa salamu za Pongezi, huku wengine wakitupia lawama zao kwa Watanzania wakisema kuwa hawakupiga kura. ” Tuna watumiaji wa simu zaidi ya Milioni 15, kama nusu ya hawa wangepiga kura Msechu angepata ushindi wa Kishindo, infact angepata kura nyingi kuliko CCM” ilisema moja ya status ya mdau wa burudani.

“Msechu kwangu mimi we ni mshindi, your entertainer, unajua jinsi ya kutawala jukwaa na kuwaburudisha washabiki wako, hiko nikipaji, tofauti na mshindi Davis ambaye anajua kuimba lakini hawezi kuteka nyoyo za mashabiki” alisema Paul Msanga kwenye status yake ya Facebook.

Kwa ushindi huu Mganda Davis atajinyakulia zaidi ya Tsh. 30,000,000/- huku akijipatia mkataba wa kurekodi Album na kampuni kubwa huko Afrika ya Kusini.

MSechu karibu nyumbani, we ni mshindi na

Angalia Video hii umuone Msechu

 


DROGBA DINNER BOOST FOR HOSPITAL PROJECT

December 6, 2010

 

..

Mualikwa akichana sebene huku FAlly akighani na jamaa wakimkodolea macho.

...

Toka Kushoto ni mmoja wa waalikwa, Ashley Cole, Mamaa Yasmin na Essien.

Yasmini ni mtanzania na ni mke wa “Le Grand Yakuza” Debs De Mukelinga wa Congo, alionekana sana kwenye Show ya JB Mpiana na Fally Ipupa ya hapa Dar Es Salaam.

…………..

Mchezaji wa Chelsea Mu-Ivory Coast Didier Drogba jumamosi alifanya Dinner ya nguvu kwa ajili ya kuchangia na kutunisha mfuko wake wa kijamii.

Huku ikihudhuriwa na mamia ya mashabiki na wanamichezo pamoja na wanamuziki maarufu, Chakula hicho cha usiku kiliweza kukusanya zaidi ya Paundi za Uingereza  £300,000 ikiwa ni jitihada zake za kujenga Hospitali kubwa huko jijini Abidjan, Mji mkuu wa Ivory Coast mahali ambapo ndio amezaliwa.

Waalikwa waliburudishwa na Nicole Scherzinger, The Saturdays, Mwanamuziki nguli toka Congo Fally Ipupa na DJ Spoony.

Halikadhalika mwanamuziki toka kundi a U2 ajulikanaye kwa jina la Bono alitoa ujumbe wake kwa njia ya Video akiunga mkono jitihada hizo na kusema kuwa yeye binafsi atasaidia, Bono ni mwanamuziki ambaye amesaidia sana nchi za Africa ikiwemo Tanzania ambapo aliwahi kuja mara kadhaa na kuwasaidia waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI.

PAmpja na vitu vilivyopigwa mnada ni Gitaa la mwanamuziki Bono ambalo lilikuwa na Saini yake na lilinunuliwa na Mchezaji wa Chelsea Michael Essien, Jezi ya mwanasoka Lionel Messi abayo ilinunuliwa na mchezaji mwenzie  Frank Lampard, naye mwanasoka nguli Salomon Kalou alinunua jezi ya Kobi Bryant, pia kulikuwa na Shati ambalo lilikuwa limesainiwa na mwanasoka nhguli wa Uingereza DAvid Bekham pamoja na zawadi nyingine kadha wa kadhaa ikiwa ni pamoja na mapumziko kwenye hoteli za kifahari sehemu mbalimbali ulimwenguni.

Chakula hicho cha jioni kilihudhuriwa naMichael Essien, Solomon Kalou, wengine ni  Ashley ColeFlorent Malouda,John Mikel ObiJohn Terry na Frank Lampard, pamoja na wachezaji wa Arsenal Theo Walcott, Emmanuel Eboue na Bacary Sagna, huku klabu ya Tottenham ikiwakilishwa na William Gallas na Carlo Cudicini na Fulham walikuwepo Diomansy Kamara na Dickson Etuhu.

Kati ya waalikwa 400 waliohudhuria pia walikuwepo Christine Bleakley, Professor Green na mwanamuziki Akon.

Pia wapo walichangia kupitia Tweeter za watu maarufu kama Russel Brand, Shakira na @FondationDrogba.

Na Jordan Kitima nakati ya UK,

Big up kaka

 


%d bloggers like this: