KANUMBA AELEZEA SABABU ZA KWENDA KUIZINDULIA FILAMU YA OFF SIDE NCHINI DRC

December 2, 2010

Hivi karibuni,kupitia vyombo mbalimbali vya habari,ilitangazwa kwamba filamu inayokwenda kwa jina la Off-Side,ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa filamu nchini Tanzania,itazinduliwa rasmi nchini Congo(DRC-Democratic Republic of Congo).Filamu hiyo imechezwa na baadhi ya vinara wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kama vile Steven Kanumba,Ray Kigosi na mwanadada Irene Uwoya.

Mara tu baada ya habari hizo kutoka,baadhi ya mashabiki wa filamu walituandikia kutaka kujua sababu za filamu hiyo kwenda kuzinduliwa rasmi nchini Congo badala ya nyumbani Tanzania ambapo ndipo penye mashabiki wengi zaidi na isitoshe ndio uwanja wa nyumbani.

Ili kupata jibu la swali hilo na mengine Bongo Celebrity ilimtafuta Kanumba na kufanya naye mahojiano, Gonga hapa kujua zaidi

 

Advertisements

Issa Hayatou akanusha madai ya rushwa

December 2, 2010

Afisa mkuu wa mcheza wa soka Issa Hayatou amekanusha vikali madai alihusika na ufisadi kwenye kipindi kilichorushwa na BBC cha Panorama.

Issa HayatouIssa Hayatou

 

Hayatou ambaye ni Makamu Rais wa shirikisho la FIFA amesema anatafakari kuichukulia BBC hatua za kisheria.

Kwenye kipindi cha PANORAMA kilichopeperushwa hewani siku ya Jumatatu, inadaiwa Hayatou alichukua hongo ya pesa za Kifaransa 100,000 sawa na paundi za Uingereza 12,900 mwaka wa 1995, kutoka kwa kampuni moja ya Uswizi ili kampuni hiyo ipewe mkataba mnono wa matangazo na FIFA.

Bwana Hayatou amesema pesa hizo zilikuwa zinatumika kufadhili Shirikisho la soka barani Afrika Caf.

” Pesa hizi hazikuwa zangu ila zilikuwa zitumike kwa maadhimisho ya miaka arobaini ya shirikisho la soka barani Afrika Caf.” Alisema raia huyo wa Cameroon ambaye pia anaiongoza Caf.

“Wakati huo ISL ndio waliokuwa wafadhili wa Caf na walitoa pesa hizo kwa shirikisho hilo wala sio kwangu na kamati kuu ya Caf ilikubali na kuidhinisha”

”Nitakutana na mawakili wangu. Nitazungumza nao kisha nione hatua za kuchukua.”

Kipindi hicho cha Panorama kilimshutumu Bwana Hayatou kwa kuhusika kwenye ufisadi pamoja na viongozi wengine wa FIFA, Nicolas Leoz wa Paraguay na Ricardo Teixeira kutoka Brazil.

Viongozi hao watatu wamo kwenye jopo litakaloamua ni nani atakayekuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2018 na 2022.

Kamati ya Kimataifa inayosimamia ya Olimpiki ilisema itafanya uchunguzi wake kuhusiana na madai hayo ya ufisadi kwa kuwa bw Hayatou ni mwanachama wa kamati hiyo.

Kundi lilalotetea Uingereza kupata nafasi ya kuwa wenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia wameishutumu BBC kwa kutoa ripoti hiyo ikiwa imesalia siku mbili tu kuamua nani atakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

 


Mourinho akataa timu yake kufedheheshwa

December 2, 2010

Na BBC

Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho amekanusha kwamba timu yake ilifedheheshwa na Barcelona baada ya kushindiliwa mabao 5-0 katika uwanja wa Camp Nou.

 

Mabingwa wa Hispania Barca walicheza katika kiwango cha juu walipoisambaratisha Madrid katika mchezo wa kwanza wa El Clasico kwa Mourinho tangu aanze kuifundisha Madrid.

Alisema:”Timu moja ilicheza katika kiwango chake na nyingine haikucheza vizuri. “Kupoteza sawa tumepoteza, lakini kufedheheshwa hapana. Ilikuwa sahihi kupoteza mchezo ule, kwa sababu hatukucheza vizuri.

“Nimezungumza na wachezaji wangu na nimewaambia msimu haujamalizika. Aliuliza: “Nani ajuaye kitakachotokea mwaka huu?”

Mourinho, ambaye katika ufundishaji wake wa soka ya kulipwa hajawahi kuongoza timu iliyowahi kufungwa hata mabao manne kwa bila, amesema dakika 90 za mchezo na Barcelona hazikuonesha makali ya kweli ya Madrid.

Aliongeza:”Sidhani kama matokeo ya mechi ile yanaonesha tofauti ya wazi baina ya timu hizi mbili. “Na pia mbio za ubingwa hazijamalizika leo.

“Tupo nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara wa ligi hii, lakini kuna michezo mingi imesalia. Hatuna budi kuonesha uwezo wetu wa kusakata kandanda na kushinda. Natamani hata tungekuwa na mchezo kesho.

Kwa Pep Guardiola, ambaye ameshinda kwa mara ya tano El Clasico tangu awe meneja wa Barcelona, amesema amefurahishwa sana kuona namna timu yake ilivyocheza katika kiwango cha juu na kuangaliwa na mamilioni ya wapenda soka duniani kupitia televisheni zao wanaokisiwa kufikia milioni 400.

Alijigamba: “Ningependa kuzoa pointi nyingi zaidi dhidi ya Madrid lakini hilo haliwezekani.

 


Full Maubunifu hapa!! Kitenge Collection

December 2, 2010

...

Gladiators za kitenge

...

....

...

...

...

Collection hii pamoja na nyingine kibaaaaao zinapatikana Pinacolada Collection Mitaa ya Namanga karibu kabisa na NMB BANK. Nyoote mnakaribishwa, ukifika hapo sema umeviona kwenye Blog ya Spoti na Starehe.


Jahazi la Gadner ndio kwaheri ama?

December 2, 2010

Gadner Habash

Nimepata email kama tatu hivi wakitaka kujua mustakabali wa mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi kinachorushwa na redio ya Clouds Fm bwana Gadner G. Habash kama ni kweli ameamua kung’atuka utangazaji ama lah.

Ni vigumu kujibu kwa sasa kwani juhudi zangu za kumpata Gadner hazikufanikiwa kuzaa matunda, lakini kwa mujibu wa status ya ukurasa wake wa Facebook Gadner amesema kuwa atatoa tamko rasmi nini kinaendelea kuhusu yeye na kipindi cha JAhazi, “…Jamani friends, ni ngumu kujibu kila mtu ila asanteni kwa kuonyesha upendo…….Sasa Ijumaa hii tar 3 msikilize Jahazi nitatangaza sababu, nia na uwezo wa kufanya ning’atuke Utangazaji CLOUDS na kabla ya hapo nitaizungumza humu humu kwenye Facebook” .

Gadner amejizolea umaarufu mkubwa kwa kipindi chake cha Jahazi na kimenogeshwa baada ya kumuongeza Kibonde ambapo wamekuwa wakiongelea mambo yanayoigusa jamii hasa.

Katika kile kinachoelezwa kuja kivingine Redio hiyo ya Clouds imekuwa ikitaka wasikilizaji wake kupiga kura ili kuchagua wenyewe nani wanamtaka awe kwenye kipindi gani na kwa sababu gani ili kuweza kuwa na vipindi ambavyo wasikilizaji wanavitaka.

Hali hii ya utata si kwa Gadner tuu bali mwanadada machachari wa Kipindi cha African Bambataa bibiye Sophia Kessy naye alitangaza nia ya kung’atuka kazi ya utangazaji na kusema kuwa anataka kujikita zaidi kwenye utangazaji wa luninga.

“Huu ni ubunifu ambao una create ownership kwa wasikilizaji wao nawapongeza sana Clouds …”alisema jamaa yangu tulipokuwa tukiliperuzi hili suala.


%d bloggers like this: