Matokeo ya ligi kuu ya England

Manchester United imeiangushia kisago Blackburn Rovers kwa kuitandika mabao 7-1, kwenye uwanja wa Old Trafford. Kati ya hayo Dimitar Berbatov amefunga matano, huku mawili yaliyosalia yakifungwa na Ji Sug Park na Nani. Bao pekee la kufutia machozi la Blackburn limefungwa na Chris Samba.

BerbatovBerbatov alipachika mabao matano peke yake

Bolton imetoka sare ya mabao 2-2 ikicheza na Blackpool. Blackpool ndio ilianza kupata mabao kupitia Ian Evatt dakika ya 28 na bao la pili kufungwa na Luke Varney dakika ya 57. Martin Petrov wa Bolton aliyeingia katika dakika ya 60, aliandika bao la kwanza katika dakika ya 75, huku bao la kusawazisha likifungwa na Kavin Davies dakika ya 89.

KevinKevin Davies

Everton nao wakicheza nyumbani walichabangwa mabao 4-1 na West Brom. kiungo wa West Brom Paul Scharner alianza kwa kuandika bao la kwanza dakika ya 14, Chris Brunt kufunga la pili, Somen Tchoyi bao la tatu, na la nne kufungwa na Sylvain Distin, ambaye alijifunga. Bao pekee la Everton lilifungwa na Tim Cahill dakika ya 42.

West BromWachezaji wa West Brom

Fulham nayo ilitoka sare ya 1-1 na Birmingham City. Goli la Birmingham lilifungwa na Sebastian Larsson, na bao la Fulham kufungwa na Clint Dempsey.

Manchester City nayo imebanwa na Stoke City baada ya kulazimishwa sare ya 1-1. Licha ya Man City kutawala mpira, bao lao lilifungwa katika dakika ya 80 kupitia Micah Richards. Hata hivyo, Stoke wakicheza kufa na kupona waliweza kusawazisha bao hilo katika dakika za majeruhi, kupitia Mathew Ethrington.

ManciniMeneja Roberto Mancini wa Man City

West Ham United ilizinduka ya kuichapa Wigan Athletic kwa mabao 3-1. Valon Berhami ndio aliandika bao la kwanza, Viktor Obinna akifunga la pili na la tatu kupachikwa na Scott Parker. Bao peekee la Wigan limefungwa na Tom Cleverley.

Sunderland ilichapwa mabao 3-2 na Wolves. Mabao ya Sunderland yalifungwa na Darren Bent na Danny Welbeck. Kevin Foley, Stephen Hunt na Sylvan Ebanks-Blake ndio walifunga mabao ya Wolverhampton.

Advertisements

One Response to Matokeo ya ligi kuu ya England

  1. kelvin justin says:

    benfica na chelsea lini?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: