Epaka yakwake Soleil Wanga

Soleil Wanga akiwa ni Zao la MWanamuziki Nguli La’ The Grand Zaire Du Rambo, Papa Fololo, Shakespere of Afrika, Quadra Kora Man, Charles Antonio Koffi OLomide, Mukulu Kulu.

Alimpata huyu Wanga na vijana wengine wakiwa choka mbaya baada ya kuwafanyia interview ya muziki kwenye baa baada ya Koffi kukimbiwa na wanamuziki wake, Alipohojiwa na Digital Congo, Koffi alitamba kuwa anauwezo wa kutengeneza timu mpya na ikawa nzuri kama ya mwanzo, na muda si muda ndio akaibuka na hawa vijana na leo ndio unawaona.!

Wanga aling’ara sana kwenye ile Album ya ustaarabu wa waarabu ‘Monde Arab’ ambayo ilikuwa ni jibu la Album ya JB Mpiana iliyojulikana kama Anti Terro, Ambayo kwenye Video ya Wimbo huo alionekana JB na Vijana wake wakiwa wamevalia kanzu na baadaye bomu kulipuka na vijana wanakuja wakizuia ughaidi huo, ndipo Koffi akaja na Monde Arab, akitetea ulimwengu wa Waarabu.

Alikuja na style yake ya uimbaji ambayo Jose Mara wa Wazee wa Mjini aliiga vizuri sana na kumpatia maujiko ya Kichina!

Hii ni Style ya SOUVEREIGN LE GRA LEADER CARITHMATIKE GENERATION DE LA MUSIC CONGOLESE ametamka wazi Kwamba hataki mwanamuziki kutoka bendi yeyote zaidi kukuza vipaji vipya kupitia wenge B aliyoianzisha inayoitwa PPU (PRESIDENTIAL PROTECTION UNIT), Ambao kazi yao ni kulisha kikosi kikubwa baada ya kuiva kule ambapo kazi ya Academy ya PPU ni kufundwa kimuziki hasa.

Utakumbuka kuwa Koffi alliwahi kukimbiwa na wanamuziki wake waliotamba kama AKINA-GERO MPERA, MONTANA KAMENGA, GIPSON BUTUKONDOLO KALAKAMFUMU, DEO BRANDO ambao wameenda kuchakura na kujitafutia riziki huko waendako.

Majuzi mkongwe Didie Kinuani alisikika akimwambia Werasson kuwa ahana haja ya kugombana na vijana wanaoenda kutafuta maisha kwani hata Simba hulea wanawe na baadaye watajigawa na kwenda kuanzisha clan zao kwenye pori hilohilo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: