DJ Q Mzigoni

September 24, 2010

Anaitwa Mohammed Chande AKA DJ Q akiwa mitamboni, kwa sasa DJ Q yuko na Times FM akikamua vitu vyake pande zile.


Mpela Brothers – Mortel Combat

September 24, 2010

Wanaitwa Mpela Brothers wakiwa ni makaka wawili Allain Mpela na Geco Bouro Mpela, Hawa vijana wote ni matunda ya makundi mawili makubwa ambapo Allain Mpela alikuwa na kundi la Wenge Musica BCBG chini ya nguli JB Mpiana huku Geco Bouro Mpela ye akiwa anatokea kundi cha Koffi Charls Olomide.

Alain Mpela aling’aa sana alipokuwa na Wenge Musica BCBG hasa kwenye albamu yao ya Titanic ambapo aliimba sana na beti zake kuvutia wengi nyimbo kama Liberation, Serge Palmi na nyinginezo. wakati Geco Mpela yeye aling’ara zaidi kwenye Ultimatum ya Koffi Olomide.

Allain Mpela aliamua kutoka solo na mpaka sasa ana Album moja sokoni inaitwa INTIFADA huku Geco Mpela naye alitoka kivyake na album yake inaitwa ICE DE PROCEDURE, lakini wawili hao huwa wanafanya show ya pamoja na walitoa album moja wote wawili ikiitwa Mortel Combat ambayo ilitengenezwa na Professionally Solorist Allain Prince Makaba huko Bruxells Belgium.

Iliwahi kutamkwa kuwa Allain Mpella alikuwa tayari kurejea kundini juhudi ambazo zilifanywa na ZK Zadio Congolo akishirikiana na tajiri mwingine lakini mpela alisema kuwa kwa sasa hawezi kwa kuwa anamipango yake ambayo bado hajaikamilisha pindi ikikamilika basi ataufikiria huo mpango.

Alain Mpela ni moja ya mapigo makubwa sana kwa JB Mpiana kwani alikuwa ana wapenzi wengi sana lichaya ukweli kuwa ana sauti nzuri na tamu.

Weekend njema waungwana.


Titus Bramble atuhumiwa kumbaka mwanamke

September 24, 2010

Mlinzi wa Sunderland Titus Bramble, amekamatwa baada ya mwanamke kubakwa kwenye hoteli moja mjini Newcastle.

Mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya England amekamatwa pamoja na mtu mwengine katika hoteli ya Vermont mapema siku ya Jumatano na wanahojiwa na polisi.

Bramble mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa kwa kushukiwa amebaka baada ya polisi kupigiwa simu na mwanamke mmoja.

Klabu ya Sunderland hadi sasa haijazungumza lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Bramble alijiunga na klabu hiyo akitokea Wigan msimu huu.

Msemaji wa kituo cha polisi cha Northumbria, amesema wanaume wawili, wakiwa na umri wa miaka 29 na 30 wamekamatwa wakituhumiwa kubaka mwanamke.

Bramble pia aliwahi kuichezea New Castle na Ipswich.


Walemavu wapanda mlima Kilimanjaro, Ni Askari wa zamani wa Marekani

September 24, 2010

Kirk Bauer, Neil Duncan na Dan Nevins

Na BBC

Maaskari watatu wa zamani raia wa Marekani waliokatwa viungo vyao vya mwili wamepanda mlima Kilimanjaro, wakistahamili maporomoko na majeraha kufikia kilele cha mlima mrefu barani Afrika kila mmoja akiwa na mguu mmoja tu ambao ni imara.

Watu hao kutoka Vietnam, Afghanistan na Iraq, walikwea hadi kufikia juu ya mlima huo wenye urefu wa mita 5,891 uliopo nchini Tanzania.

Iliwachukua siku sita kufikia kileleni kwa nia ya kuonyesha kuwa ulemavu haumaanishi huna uwezo wa kufanya lolote.

Safari hiyo huchukua siku tano hadi sita, na ilibidi watu hao kusimama mara kwa mara ili kurekebisha miguu yao ya bandia, baada ya kuteleza sana.

Wakweaji hao wa mlima ni Dan Nevins, mwenye umri wa miaka 37, ambaye alipoteza miguu yake nchini Iraq, Neil Duncan, wa miaka 26, alipoteza miguu yote miwili katika shambulio la bomu lililotegwa barabarani Afghanistan mwaka 2005; na Kirk Bauer, mwenye miaka 62, aliyepoteza mguu mmoja huko Vietnam mwaka 1969.

Bw Bauer aliliambia shirika la habari la AP, ” Ikiwa watu watatu waliokatwa viungo kutoka vita vitatu tofauti na kutoka vizazi tofauti na wana mguu mmoja tu wanaweza kupanda mlima Kilimanjaro, marafiki zetu wengine walemavu wanaweza kutoka na kupanda mlima au kuendesha basikeli au kuogelea, na wanaweza kuwa na maisha yenye afya njema.”

Bw Nevis alipata jeraha katika kigutu ya moja ya miguu yake hiyo ya bandia na baada ya kufika kileleni aliondoshwa kwa kutumia machela.

Bw Bauer ni mkurugenzi mtendaji wa michezo ya walemavu wa Marekani, shirika lililopo mjini Wasington DC linaloshughulika na uzima wa afya na ushiriki wa michezo kwa walio na ulemavu.


CAF yapata Katibu Mkuu mpya

September 24, 2010

Hicham el Amrani wa Morocco ameteuliwa katibu mkuu wa muda wa shirikisho la soka barani Afrika, Caf.

Uteuzi huo ulithibitishwa baada ya mkutano wa kamati ya utendaji ya Caf mjini Cairo, Misri, siku ya Alhamis.

Kijana huyo mwenye miaka 31 anachukua nafasi ya Mustapha Fahmy anayeondoka Caf kujiunga na Fifa kama mkurugenzi wa mashindano.

Uteuzi wa Amrani unaanza rasmi tarehe 1 Oktoba, na kupanda haraka kwa mtu huyo aliyejiunga na Caf mwaka 2009.

Aliacha kazi yake kama meneja masoko wa shirikisho la soka barani Asia ili kuwa katibu mkuu msaidizi wa Caf, ambaye alifanya kazi kwa ukaribu na Fahmy.

Rais wa Caf Issa Hayatou alimsifia Fahmy aliyekaa kwenye nafasi hiyo kama mkurugenzi mkuu wa chombo hicho.

Hayatou alimwambia Fahmy ambaye ni raia wa Misri, “Hapa ni kwako daima.”

Fahmy amabye alikuwa katika hisia kali alimwaga machozi na kuzungumzia jinsi ilivyo “vigumu” kwake kuondoka kwenye shirikisho hilo.

Alisema “ataendelea kuwa mfanyakazi mwaminifu wa soka ya Afrika” wakati akifanya kazi na Fifa.


Yanga yailamba Kagera 2-0

September 24, 2010

Mchezaji wa Yanga , Nsa Job akitoa pasi ya mpira kwa kutumia kichwa , huku akilindwa na beki wa Kagera Sugar, Said Mourad ( jezi 15) wakati wa mchezo wao uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa. Yanga ilishinda bao 2-0.


Formula 1

September 24, 2010

Britain’s Lewis Hamilton of McLaren Mercedes arrives at the Marina Bay racing circuit ahead of Formula One’s Singapore Grand Prix night race in Singapore on September 23, 2010. The race to the Formula One drivers’ title is on a knife-edge going into the Singapore Grand Prix, and picking up points will be crucial for the five men in serious contention.