Iveta – Wimbo wa Sajna wenye kisa cha ukweli

Albamu yake iko tayri kwenda Sokoni.

Albamu ya Sajna inatoka sasa, kilichonifurahisha ni kisa cha ukweli katika wimbo ambao umemtambulisha Sajna wa Iveta wimbo ambao umebeba Album kwa kiasi kikubwa, na kupendwa sana.

Katika Wimbo huo ambao unazungumzia mapenzi ya kijana ambaye alimuacha mpenzi wake kijijini na yeye kuja mjini kuhangaika. Inasemekana kuwa huko kitaani kwake Sajna kuna kijana ambaye alikuwa akifahamu kwamba mchizi ni mwanamuziki hivyo siku moja walipokutana akampa kisa chake ambapo jamaa anatokea Kanda ya ziwa na alikuwa jijini katika harakati za kutafuta harakati ambazo zimemuingiza kwenye biashara ndogo ndogo. 

Lakini taarifa anazopata kuwa mpenzi wake kijijini analalamika kama mchizi kamtosa kidizaini baada ya kufika mjini, Kwa mujibu wa XXL ya Clouds FM Sajna pale pale alidondoka na Chorus ya wimbo huo wa Iveta na hatimaye kudondoka na Verse tatu zilizoelezea kisa hiki cha ukweli ikiwa ni ujumbe kwenda kwake Iveta huko Kijijini.

Rafiki yangu Robert Mwafrika anaupenda sana huu wimbo sijui labda unamgusa kwa namna moja ama nyingine, lakini unaujumbe wa ukweli ambao hata kama unausikia leo kwa mara ya kwanza ni wazi kuwa utaupenda.

Record Label ya Tetemesha Records ndio waliofanya mambo kwenye albamu ya IVETA, chini ya KID BWOY, AB RECORDS chini ya AMBA, A2P chini ya SAM TIMBER, IMMORTAL MUSIC chini ya TRIS na M LAB chini ya DUKE.

Single ya pili kutoka bado haijaamuliwa ila ni kati ya SITAKI KUUMIZWA na MBALAMWEZI, moja kati ya hizo itakayopendekezwa na wadau wengi ndio itakayofuata baada ya IVETA.

Album ya IVETA ya msanii SAJNA ina jumla ya nyimbo 10, ambayo ilianza kutengenezwa Mwezi January 2010 na kukamilika mwezi July 2010. Wasanii waliopata nafasi ya kushirikishwa katika album hii ni Belle 9, Linah wa THT, Josefly kutoka Musoma Mara pamoja na Pipi. Lengo la kutoshirikisha wasanii wengi sana ni kutaka kuonesha uwezo wake na kuthibitisha kwamba msanii mchanga si lazima atoke kwa kupitia mgongo wa wasanii wakubwa.

A2090 - HUSSEIN JUMBE - SUBIRI KIDOGO

Gonga picha kuikuza.

 

ALBUM TITLE: IVETA

ARTIST: SAJNA

RELEASE DATE: 19TH AUGUST 2010

EXECUTIVE PRODUCER: KID BWOY

DISTRIBUTOR: GMC & UMOJA AUDIO VISUAL

Gonga hapo chini kujua nyimbo ndani ya Albamu hii ya Sajna

Song list as appeared on Cd cover

1. IVETA

2. Sitaki Kuumizwa ft. Linah

3. Binadamu

4. Mbalamwezi

5. Udehule

6. Mganga ft. Josefly

7. Nadhifa

8. Roho Mbaya ft. Belle 9 & Pipi

9. Subira

10.Ishara ya Msalaba

2 Responses to Iveta – Wimbo wa Sajna wenye kisa cha ukweli

  1. Anonymous says:

    Miito ya simu/nyimbo zote zidownload za SAJNA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: