Waheshimiwa tumieni mitandao kuwafikia wapiga kura wenu.

Mitandao ya social networking ndio inasemwa kuwa njia ya haraka zaidi ya kufikisha mawazo ya mtu huku mitandao kama Facebook, Twitter, Hi5, Friendster, Ning na mingineyo ikiongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi.

Kwa leo naomba niongelee zaidi mtandao wa Facebook na uwezo wa nguvu ulionao kwenye maisha yetu ya kila siku na hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

Nalazimika kuandika na kuyasema haya kwa kuwa facebook kwa sasa ni silaha ambayo hulipiii chochote kuwa nayo na kama itatumika vyema basi we kama mgombea unaweza kuwafikia kirahisi walengwa wako.

Je Vijijini wanasoma facebook?

Asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao hii wako jijini Dar Es Salaam na mikoa mikubwa kama Arusha, Morogoro, Tanga, Mwanza na kwa siku hizi mitandao inafika kote.

Jiji hili la Dar wakazi wengi ni wakuja wanatoka vijijini ambako wabunge wengi hutoka huko. Mathalani mi ni mtu wa Morogoro Kilombero, bila vyombo vya habari siwezi kujua mgombea wa Ubunge wa jimbo langu ana sera gani, lakini kama nitakuwa nasoma mawazo yake kupitia updates za mara kwa mara kwenye mitandao hii naweza nikawa mpiga debe mzuri kwani at least nitakuwa nimepata picha fulani ya mgombea wangu kwa hiyo hata huko kijijini nikibahatika naweza washauri ninawafikia kuwa Bwana Kibonde ni mtu safi na nia ya kutukwamua anayo tumachagueni.

Hakuna kubwa linalofanyayika kwa mtu anapokuwa na ukurasa zake wa Facebook na wala hulipii senti kuwa na kurasa hizi.

Nini unaweza kufanya kwenye ukurasa wako

Kikubwa ni zile information zako ikiwa ni jina, umri, mwaka wa kuzaliwa mahusiano yako, unayopendelea nk.

Unaweza kuweka picha mbali mbali za matukio mbali mbali ambayo wewe umeyafanya ya kijamii na hivyo kushare kirahisi na watu wakaelewa ni jinsi gani una mguso wa kijamii.

Status Updates (sijui kiswahili chake) ila kwa maana rahisi twaweza sema ni pale unapoweza kuwakilisha lililomo kichwani mwako kwa wakati huo na watu kuweza kuchangia hapo unaweza kupata mawazo hata msaada kama utakuwa unahitajika, si wa mali bali hata wa mawazo tuu.

Kutengeneza marafiki maalumu kwa kurasa za ziada kama funpage ambapo unaweza sema Wana Mlimba basi sie wanamlimba tukajiunga na wewe na kubadilishana mawazo humo.

Kiukweli kuna mengi ya kufanya kwenye mtandao huu wa facebook.

image

Ukurasa wa Mh. Rais kikwete kwenye facebook

Nilifurahi nilipoona Mheshimiwa Kikwete yuko kwenye facebook, sina hakika kama ni yeye au ni mtu anafanya kazi ya ku update page yake lakini yupo.

Binfsi sijawahi hata mara moja kwenda kwenye mkutano wowote wa hadhara si kwamba sio mshabiki wa siasa ila naona kama ni kupoteza muda ambao ninaweza kuutumia kwa kitu kingine. wapo wengi kama mimi ambao wana elimu zao ambao si rahizi kuwakuta kwenye mikutano ya hadhara lakini hata nikienda najiona nitakuwa msikilizaji ilihali wakati mwingine ningependa kuuliza japo swali.

Siwezi labda kwa vile nitakuwa nyuma sana au hata kugopa kuzomewa na pengine kutupwa kwa kama mimi ni CCM na nimeenda kwenye mkutano wa Chadema kusikiliza kiongozi ambaye nampenda lakini nataka kujua kwa sisi wananchi wa Mlimba ambao kwetu machungwa yanaharibika kule Masagati au mpunga unaooza melela au ndizi za mofu zinazooza atatufanyia nini wengine wanaweza kuona kama namchallenge mtu wao ikawa taabu.

Kwa nchi za wenzetu hayo yamerahisishwa kupitia technolojia ambapo wagombea wana ma blog, wako kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, hi5, Twitter, na mingineyo ambapo wanawashabiki au wanachama ambao wanawafuatilia na kujibu hoja zao za msingi kirahisi kabisa.

image

Ukurasa wa Facebook wa Mh. Zitto Kabwe.

Nakumbuka siku moja nilimuona Mh. Zitto Kabwe kwenye Facebook nika mu add kama rafiki yangu akanikubali na nikakutana naye siku moja ambayo nilikuwa na kiu ya habari baada ya kuona kwenye moja ya gazeti kichwa “Zitto kuihama Chadema’ nilimuuliza Mheshimiwa Eti muheshimiwa ni kweli unataka kutoka Chadema?, lilikuwa ni swali langu ambalo nilimuuliza mh. Zitto Kabwe kupitia mtandao wa Facebook na yeye kwa kifupi alinijibu “Hapana, hao ni wazushi tuu hehehehehe”. Niliiamini zaidi kwa vile niliyeongea naye ndiye aliyekuwa amepamba vichwa vya habari kwa siku hiyo kwa gazeti moja.

Nimeanza na hii kwa kutaka kuonyesha urahisi wa mawasiliano kwa dunia ya sasa ya mtandao ulivyo rahisishwa kwani siku ya habari hiyo wenda kwa kutokukumbuka nilisahau kuwa ni siku ya wajinga duniani. Utaona hapo ni jinsi gani ilikuwa rahisi ku clear doubt yangu ambayo labda kwa kutokuwa na access ningeamini gazeti lile.

Wengine wanaweza kusema kuwa watu wa chini atawafikiaje lakini ujue wengi wanaokwenda kwenye mikutano ni hao wanaowaita watu wa chini na je watu watu wa ofisini atawafikiaje?. Nasema hivi kwa vile wengi wa wanasiasa wamejaza zaidi ya mashabiki marafiki 5000 ambao wanatakiwa kwenye mtandao kama Facebook.

image

Mh. Barak Obama kama anavyoonekana kwenye ukurasa wake wa facebook

Uzuri wa facebook wanachama wake na washabiki wake wengi ni vijana ambao kwa ulimwengu wa sasa ndio ambao wanamchango mkubwa sana kwenye siasa. Watafiti wa mambo wanasema kuwa Rais Barak Obama alisaidiwa kwa kiasi kikubwa sana na mitandao hii kuwa ilichangia kwa kiasi kikubwa sana mafanikio yake, (gonga hapa).

Obama aliweza kujibu maswali ya wananchi wake ambao wengi wao walikuwa ni vijana ambao awali walikuwa hawapigi kura kwa kisingizio kuwa vijana hawasikilizwi walijitokeza na ni kweli wengi walishawishiwa na utaratibu wa Obama kuwajulisha kila stage kwa kupitia mtandao ama wa twitter ama wa facebook.

Binafsi naona ni wakati muafaka kwa hawa wanasiasa wetu kutumia mitandao hii ambayo mingi ni bure ili waweze kutufikia  sisi ambao hatuendi kwenye mikutano yao huko Mwembe yanga au Kibanda Maiti au Kicheba kwenda kuwasikiliza lakini kama watakuja hapa walao mara moja kwa wiki kam anavyo fanya Mh.. Zitto Kabwe ambaye mara kwa mara tunagongana mtandaoni live na kubadilishana mawili matatu.

Ni kweli huwezi kusema huku bado hatujafikia lakini mjua unapoongelea Sayansi na Teknolojia huwezi pindisha kona na kuviacha vitu kama hivi, kwani nasemwa ugunduzi wa Technolojia ya mtandao wa Internet umeifanya dunia kuwa kama kijiji na kubadili utaratibu za zamani wa kutumia Posta kwa ajili ya mawasiliano.

Si lazima uwe wewe mwenyewe, mathalani Mh. Moe ambaye ana blog yake, ana team yake ya watu wake ambao wana update kila mara, hii inakufanya wewe kuwafikia watu wako kwa maneno yale unayataka wewe, ni njia rahisi na uzuri ni kwamba hailipiwi unataka nini sasa?

Ni mtazamo tuu.

Advertisements

2 Responses to Waheshimiwa tumieni mitandao kuwafikia wapiga kura wenu.

  1. Good details, excellent and valuable layout, as share fantastic things with superior ideas and concepts.

  2. Admiring the time and energy you put into your site and detailed information you offer. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed information. Wonderful read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: