Makirikiri; kuna zaidi ya Ngoma na utamadani?

image

Kundi la Makirikiri chini ya uongozi wa Tshenga wakifanya vitu vyao katika ukumbi wa Ikweta wiki iliyopita.

Ikumbukwe kwamba wanamuziki hawa walikuja nchini kwa ziara ya wiki moja ambayo iliwafanya wakae kwa zaidi ya mwezi jambo lililowafanya waachie mchongo wa kupiga kwenye mechi mbili za kombe la Dunia lakini kutokana na ziara hii walikosa mchongo huo na kuamua kukaa hapa kwa takribani mwezi mmoja.

Jambo ninalojiuliza je hawa wanatofauti gani na vikundi vyetu vya ngoma za asili? Nini kimewafanya wafanikiwe na wawe maarufu, bila shaka ni kujitangaza kwa kuwa na CD na DVD ambazo zimeuzwa kitaifa na kimataifa, umaarufu wao hapa nyumbani ulitokana na kuanza kuonyeshwa kwenye TV zetu hapa nchini. Ndipo watu wakawajua, inawezekana kwa utashi wa mtu mmoja ama kwa ushawishi wa watu mbali mbali hilo likafanikiwa iwe isiwe lazima kuna aliyepelekea video hiz kuonyeshwa.

Tunapoongelea utalii ni pamoja na ngoma hizi za asili, kama picha za ngoma zetu zitatumiwa vyema basi inaweza kuwa ni kitu cha ziada kwenye hiyo sekta ya utalii.

Mathalani Kenya wanapotangaza tangazo lao kuna vitu lazima uvione:-

 • Wanyama
 • Mlima Kilimanjaro
 • Mbuga
 • Wamasai
 • Mahoteli na kadhalika

Ni vitu hivyo hivyo utaviona kwenye matangazo yetu ya utalii, sasa basi nini kinatutofautisha na Kenya?

ni swali ambalo mimi na wewe tunapaswa kujiuliza na kupata majibu, kwangu mimi nafikiria utamaduni kama ukitumiwa vizuri basi tunaweza kuonyesha kwa wenzetu huko mbele kuwa kuna tofauti ya utalii wa Kenya na Utalii wa Tanzania ambao una ziada kama hizo za uchezaji ngoma na kadhalika. Utashangaa naongelea zaidi Ngoma kwa kuwa makala yangu imeanza na hawa Makirikiri.

Ukiangalia vikundi kama Parapanda cha Mgunga mwanyenyelwa utaona walijaribu zaidi kuweka mkazo kwenye utamaduni, nyimbo zetu, ngoma zetu, mavazi yetu.Tuna zaidi ya Wamasai wa kuwaonyesha.

4 Responses to Makirikiri; kuna zaidi ya Ngoma na utamadani?

 1. Baraka says:

  Suala la wanamuziki wetu kutofika mbali ukijaribu kulidadisi unaweza kulia machozi. Samahani kwa kusema kwamba hata yale aliyoyasema MR 2 katika albamu ya Anti-Virus yana ukweli wake japokuwa ujumbe wake aliufikisha kwa hasira pamoja na masuala yake binafsi. Lakini Ibilisi wa wanamuziki wetu kutokufika mbali ni sisi wenyewe, mifumo mibovu ya hati miliki, BASATA kutokuwa na mikakati ya kudhibiti baadhi ya mambo ambayo yanaingia nchini kwetu kila kukicha.

  Amini usiamini kwenye nchi hata ambazo zimeendelea kama CHINA, MAREKANI na kwingineko wanakitu ambayo inaitwa censorship katika zao lolote liwe la kimuziki ama filamu na hii imesaidia sana kuwajenga vijana kimaadili pamoja na kuhifadhi utamaduni.

  Leo ukija Tanzania unawafundisha watoto tena wakiume wacheze KIDUKU. Badala ya kuwajengea tabia zenye maadili kwa kufuata mifano ya viongozi wetu tulio nao watafiti wetu, Maprofesa, Wanamichezo na wengineo wenye tabia zenye maadili leo unamwambia acheze kiduku.

  Jamii ikianza kuteketea ndio tunaanza kuzinduka. Hii kiduku inatakiwa ipigwe marufuku pamoja na masuala mengine. Mamlaka zifungue macho Wizara ya Maendeleo jinsia na watoto iangalie pia na watoto wa mtaani. Na ijue suala la ushoga kushamiri linatokana na wao kuchukua kila wanachokiona bila ya kuchekecha kwa kigezo cha uchumi huria. Na hivyo hivyo muziki wetu utaendelea kuporomoka. Haihitaji mtu mmoja kusema inahitaji watanzania wote kusema kwamba tumechoshwa na tunahitaji kubadilika.

 2. Ahmedy macha says:

  Kiufupi tu kama kunamakundi kama makilikili tz hii mimi nitajiunga nao.tatizo katika makundi yetu ni uchuro mtupu uweke mapenzi na kucheza ngoma wapi na wapi? Ama sanaa yote ile ukichanganya utakoma nimimi ahmedy macha

 3. ROSEMARY says:

  what i want is to cominicate with one of you member who is known as MATHATHANE The choirmaster makirikirione,plse get in touch with me
  Istay Sengerema Mwanza Tanzania
  YOURS ROSEMARY

 4. Reasonably specified he will have a good read. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: