Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.

Ni muda sasa kwa wapenda burudani tumesikia bifu lililopo kati ya Joseph Mbilinyi aka Mr II / Sugu na Ruge Mutahaba bila kuwa na suluhisho lenye jitihada za makusudi.

Kwa wafuatiliaji wa burudani n stori za burudani bifu hii haijaanza leo na si ya juzi wakati wa Project ya Malaria kama inavyosemwa la hasha kwani ikumbukwe ni tangu Sugu hajaondoka nchini na aliwahi pia kudisi kimtindo kwenye moja ya nyimbo na video yake.

Inawezekana ukajiuliza mbona nimeandika hivi, ni kwa makusudi mazima nikiangalia mustakabali wa sekta ya burudani na hili lililopo ni wazi kuwa ugomvi unapanuka na kuingia kwenye matawi yao huku Sugu kwa upannde mmoja akitetea kile anachoita Muziki wa ukweli (hip hop) ambapo kwa sasa hamlengi Ruge tuu bali kama umesikiza ule wimbo (gonga hapa) utaona ni kwa umbali gani ugomvi huu umetanuka kwa kwena hata kwa watangazaji na wana THT ambao kwa upande wao watakuwa na chuki binafsi na msaanii husika au hata waliokaribu naye.

Hii ni hatari hasa kwa sekta ya burudani na wasanii kwani kuna kuwa na mgawanyiko na kuwatia uwoga wasanii wale ambao wanahisi wangetaka kumshirikisha Sugu kwenye nyimbo zao ama kwa kuogopa kuingia kwenye malumbano au kwa nyimbo zao kutopigwa redioni kabisa.

Ukisikiliza wimbo unaolalamikiwa (huo hapo juu)  utaona kuwa ni hasira za Mr. II kwenye kwa wahusika, na hii ni muendelezo ya bifu ninayoiongelea mimi.

Si vyema kuuongelea sana ugomvi uliopo sasa kwa kuwa jambo hilo liko kwenye vyombo vya dola lakini kama ilivyo soka ugomvi wa Sanaa na wasanii umalizwe na baraza la Sanaa ambalo hawa wasanii wote wako chini yake.

Hatupendi kufikia mahali kugawa hadi vyombo vya habari na waandishi kutokana na matatizo kati yenu ambayo kiukweli tatizo lililopo linaweza kusuluhishwa na vyombo husika kwa kuhusisha pande zote. Binafsi naimani Baraza la Sanaa ambalo hawa ni wadau wao wanauwezo na migogoro kama hii, hata sio kwa mwamvuli wa BASATA basi mlioko tumieni busara zenu kumaliza mpasuko kama huu.

Ni mtazamo tuu.

Advertisements

7 Responses to Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.

  1. Sugu achana na maswala ya ‘bifu’kilicho baki usikilize matatizo ya Wananchi wa jimbo lako au sio?,

  2. […] jana June 30, 2010 niliandika makala yangu nikisema Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.  Mpaka leo ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili na siku kama mbili tangu makala yangu. […]

  3. Appreciating the time and effort you put into your site and detailed information you present. It’s awesome to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed material. Fantastic read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

  4. I have bookmark your site and in addition include rss.

  5. Admiring the time and energy you put into your site and detailed information you offer. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed material. Excellent read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

  6. We absolutely love your blog and find a lot of your post’s to be what precisely I’m looking for. Does one offer guest writers to write content for yourself? I wouldn’t mind composing a post or elaborating on a number of the subjects you write with regards to here. Again, awesome blog!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: