Gloson; Blogger mtoto ashinda tena!

image

niliwahi kuandika kuhusu huyu mtoto Gloson, Blogger mdogo toka Malaysia ambaye kwa kiasi kikubwa amejizolea umaarufu duniani kote kwani pamoja na umri mdogo ameshatunga vitabu viwili vya mashairi akiwa amenyakua zawadi kadhaa kwenye category yake upande ya poetry.

hivi karibuni mtoto huyu alijishindia zawadi kemkem baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la ku Blog kuhusu  Territory ya Malaysia (Blog4FT (Federal Territories) contest!).

Yeye aliandika kuhusu likizo yake kwenye jiji la Kuala Lumpur ikiwa ni hadithi kwa njia ya Picha zaidi(Gonga hapa).

Mara ya kwanza nilipomuona kwa macho yangu ilikuwa wakati wa maadhimisho ya kampeni ya kitalii ya Visit Malaysia katika jengo la KLCC nchini Malaysia, na kipindi hicho alikuwa na miaka 10 tu. nilivutiwa sana naye kwani aliandika poetry nzuri sana kuhusu theme hiyo. Tangu hapo nikawa mfuasi wa Blog yake.

Gloson ameandikwa kwenye vyombo vingi sana vya habari ndani na nje ya Malaysia, Hii yote ni kutambua mchango wake na kipaji chake.

Huu ulikuwa utambulisho wangu miaka miwili iliyopita niliandika kuhusu mtoto huyo kipindi hicho akiwa na miaka 10 tu.

Gloson, 10 Years Old

Gloson, 10 Years Old

Jina Gloson kwa Malaysia limekuwa si geni kwenye vyombo vya habari hasa baada ya kuandikwa sana kw mwaka jana namaanisha nusu ya mwisho ya mwaka jana.

Gloson ni mtoto wa miak 10 lakini ni Blogger anayekuja kwa kasi akiwa na miezi si zaidi ya saba kwenye ulimwengu huu wa magazeti tando, Kipaji chake si tu kwa kublog bali ni uwezo mkubwa alionao wa kujieleza, mara ya kwanza nilisoma kwenye gazeti la The Star haikuniingia hadi nilipoona akihojiwa kwenye Chanel kubwa ya Tv3 na kumuona kwa macho yangu.

Dogo anakipaji kweli kweli na ye anasema ana blog kila kitu anachoona kina manufaa kwa jamii na katika blog yake pia amefundisha jinsi ya kuandika Post yenye mvuto na jinsi ya kuchangia topic bila kwenda nje ya mada, akiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi Gloson anasema alipata wazo la Ku blog toka kwa mama yake ambaye alimshauri ablog naye akaanza.

Mbali na kipaji hicho pia Gloson anakipaji cha kuandika mashairi akiwa meshaandika zaidi ya mashairi 100 ambayo yamechapishwa http://www.poetrytalents.com

Ikiwa na miezi 6 tu tangu ianzishwe blog ya Gloson ambayo inakwenda kwa anuani ya http://www.glosonblog.com/

Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu

"Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu"

“naamini nina mchango kwa jamii mengi waweza kujifunza toka kwangu na kuelimika, kuna mengi yakujifunza kwenye mtandao, napenda Internet naweza kufanya kila kitu kuanzia Homework, games, kununua vitu na kuwasiliana na vitu, alisema Gloson alipohojiwa kwenye Tv3. “kuna vitu siwezi kuwaeleza wazazi wangu moja kwa moja lakini huwa natuma email na naenda kulala nikiamka baba atanijibu ama kwa email au hata akikaa kimya najua anatafakari na amepata ujumbe wangu” aliongeza mtoto huyu anayejua kujieleza kwa lugha ya ufasaha na kufanya wtangazaji wote kucheka.

Pamoja na vipaji hivyo pia Gloson anakipaji cha kutumia Photoshop kwa ajili ya kucheza na picha, na ni mtundu wa mambo ya mtandao pia.

Si mbaya mtembelee hapa utakuta mengi sana ya kujifunza toka kwake. Wana Blog wenzangu mpooo!!!!?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: