Kuimbwa kuna gharama zake!

January 28, 2010

m53

Pichani ni Zadio Congole ambaye ni rafiki binafsi na shabiki mkubwa sana wa JB Mpiana akiwa katika moja ya shoo za Wenge BCBG huko Shengeni mwaka jana.

Ni jambo la kawaida kusikia majina ya watu fulani yakitajwa kwenye nyimbo, kuna watu wengi waliwahi kuniuliza majina hayo ni akina nani hasa na kwa nini yanatajwa?, Kimsingi ni mbwembwe na kujenga jina ambako kunatokana na umaarufu kwenye jamii ama kisiasa ama kibiashara.

Mara nyingi watu hawa wanakuwa ni watu maarufu ama kwenye sekta ya burudani ama mtu fulani ambao ni wafanyabiashara lakini wengi wao unakuwa wanamguso katika sekta nzima ya burudani, Mfano majina kama Sadam Hussein ilikuwa likiitajwa sana kwenye nyimbo za lingala, huyu ni mtoto wa Marehemu Mabutu Seseseko Rais wa zamani wa Zaire ambaye yeye alipendelea sana maisha ya anasana kama mtoto wa Rais wa Zamani wa Iraq Uday na Kusay, na alisaidia sana wanamuziki katika kutengneza Albamu zao. Pia kuna watu kama Zadio Congole, huyu pia ni ‘mpigaji” ambaye alifaikiwa kupata pesa anaishi huko Ubelgiji (shengheni kwa ujumla) na ni mshabiki mkubwa wa JB Mpiana ambaye kwa kiasi kikubwa amejitolea pesa na muda katika bendi hii,

Pia kuna watu kama Tabou Fatou Top Model ambaye ni “mfanyabiashara” na mdau mkubwa wa sekta nzima ya burudani naye yuko huko huko Paris na Ubegiji.

Boris Bondo, Bebee Ramadhani, Papito Mbala, Zamalenga, Cedric Okitundu ni baadhi ya majina ambayo unaweza kuyasikia sana kwenye nyimbo nyingi za Congo, wengi wao kama nilivyosema ni watu wenye nafasi zao kwenye jamii na hasa ulimwengu wa burudani.

Marehemu Mama Mere Malou “madame ya poto“ kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa, Pia Mere Malou ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mwanamuziki

Sio watu tuu bali nyingine ni kampuni zinazojishughulisha na masuala ya burudani kama Kin Service Express ambayo kwa wakati fulani ilikuwa ikifanya kazi na mwanamuziki Koffi Olomide, Manuru Vaka Productions ambao kwa sasa wamejizolea umaarufu kwa Video za Live za Wenge BCBG kwa ubora wa hali ya juu.

Kwa hapa nyumbani utasikia majina kama PDG Ndama aka mutoto ya Ngombe, Papaa Musofe na wengineo ambao wote hao wanawajibika ipasavyo na ni wadau wakubwa kwenye sekta nzima ya burudani.

Wengi wa waimbwaji hawa wamekuwa wakijitoa sana kwenye shughuli nzima ya burudani na kuzigharamia bendi husika au mwanamuziki husika kwa mavazi au huduma nyingine ikiwa ni pamoja na usafiri nakadhalika.

Angalia kipande hiki uone jamaa wanavyotunza, ikiwa ni gharama ya kuimbwa.

Kwa nchini Kongo jina lako likitajwa kwenye wimbo na bahati nzuri wimbo huo ukawa maarufu basi jina la mtu huyo hutokea kuwa maarufu na wengi walitumia nafasi hizo kisiasa na kupata ushawishi wa kisiasa, jambo lililopelekee Serikali kuingilia kati.

Hivi karibuni Serikali ya Kongo imepiga marufuku kutajwa kwa majina ya wanasiasa na viongozi wa makampuni ya umma kwenye nyimbo za wanamuziki.
Vilevile kurushwa kwa miziki ya aina hiyo katika vituo vya redio na televisheni nchini humo.Kulingana na serikali ya Kongo hatua hiyo ina azma ya kuimarisha utendaji kazi .

Ni jambo la kawaida kusikia majina ya watu maarufu yakitajwa na wakati mwingine kutumika kama Kampeni kwenye uchaguzi na kuwafanya kujizolea mashabiki na wapiga kura kirahisi kwani kwa serikali za Congo wanamuziki wanachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mtazamo wa kisiasa.

Inagharimu sana kwa mtu kuimbwa kwani wengi wamekuwa wadhamini wakubwa wa wanamuziki hawa kimavazi, kugharamia kutoa albamu au mengineyo.


Kolabo inanogesha Mziki bwana!!

January 28, 2010

Sikiliza Huu wimbo wa Mzee wa Busara toka kwa Nature na Inspekta enzi hizo (Si video Rasmi)

Kuna vitu ambavyo huwa kila siku naombea kitokee tena kwenye burudani ya muziki wa Bongo Flava:-

1. Kuwaona Hard Blasters wanafanya kazi pamoja tena.

2. Kuwaona Nature na Inspector wakifanya kazi pamoja tena

3. Kuendelea kumsikia Mr. Paul akizirudia nyimbo za zamani

4. Niwasikie Mandojo na Domokaya

5. Kuwasikia GWM wakiimba tena

Oamoja na wengineo lakini ningependa kuwatolea mfano Nature na Inspekta au Hard Blasterz (Terry, Jay na Willy).

Kwa kiasi kikubwa collabo ya hawa watu wawili ilileta muamko kwenye sekta nzima ya burudani ya Bongo Flava kwani ilikuwa inatoa hadhi hasa ya Flava za Bongo, Namkumbuka mmoja wa watangazaji wa wakati huo Mike Mhagama akiwa Radio One aliitaja hii Collable kama hazina ambayo wangeendelea basi wangeleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta nzima ya Muziki wa kizazi kipya.

Wakati huo haikuwa rahisi kupenya kwenye uzio wa nyimbo kama Bongo Dance ambapo Bendi za Dance nazo zilikuwa zimeleta mageuzi kwa kutumia Mirindimo ya Ki Congo na Muziki wa Dance ndipo zikazaliwa Bendi kama African Revolution, Twanga Pepepta, TOT, Diamond sound na muendelezo wa bendi jizo.

Hivyo basi vijana wakawa wameachwa nyumba na kujiliwaza kwa muziki toka Magharibi na ndipo huu muziki wa kizazi kipya ulipoaanza na kupitia mageuzi na vikwazo kadha wa kadha kwani wakati huo ulikuwa ukijulikana kama mziki wa kihuni.

Picha ya Maktaba ikiwaonyesha The Hard Blasters, Terry kushoto,   Prof Jay (kati) na Biggie Willy (Kulia)

Nakubaliana na kila  mmoja wao kwenda solo kwani inampa uwanja mpana zaidi lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye makundi siku zote kila mmoja ana nafasi yake, kuna wengine wanajua sana kupanga sauti wengine kupanga vina na wengine kupanga mpokezano. Mfano kwenye bendi ya Wenge Muzika wakati huo kulikuwa na mtu anaitwa Blaise Bulla kwenye wimbo utamsikia Verse moja tuu ila kazi yake kubwa alikuwa kupanga sauti na wakati mwingine hata kushauri kuwa beti hii haifai kuimbwa na wewe ikiimbwa na fulani italeta mguso zaidi.

Muziki wa Bongo Flava unatofautiana na Genge (wa KEnya) kwani wao ni Commercial zaidi wakilenga kuchezesha watu na wakati mwingine hupati maana kwenye wimbo mzima hata wakihojiwa wanashindwa kusema mziki ulilenga nini. Tofauti na muziki wetu ambao unalenga kutoa ujumbe na kuburudisha na ndio maana utaona kila mtu anajitahidi kumshirikisha mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti ambayo pia inapatikana kwenye makundi, na utao nyimbo nyingi ambazo mtu ameshirikisha mwingine zimewatoa sana.

Hivyo basi ni muhimu kwa makundi ya muziki kuthamini mchango wa kila mmoja tumeshuhudia makundi kama HArd Blasters baada ya kupanguka mmoja tuu amefanikiwa kutoka na wengine wamebaki waki piga kwata kwenye sekta ya burudani. Kuna ladha ambayo tunaikosa kama wapenzi napenda kumsikia Pro. Jay lakini naikosa ladha ya Loon T (Terry), naikosa ladha ya Biggie Willy (Baba Walter).  Hivyo usia wangu ni kwamba mnatutia kilema mashabiki wenu ambacho mkipanguka mnatupa kazi kuikubali hali halisi.


Wanamuziki wengi wa Bongo Flava wako “Facebook”

January 28, 2010

ay

Ukurasa wa AY kwenye Face Book

Wasanii kadhaa wa Bongo Flava kwa sasa wanapatikana kwenye mtandao wa Facebook na kuweza kuwasiliana moja kwa moja na wapenzi wao ambao wengine hawapati nafasi ya kukutana nao ama hata kuweza kubadilishana mawazo mawili matatu.

Ambwene Yessaya aka AY, Prof Jay, Chid Benz, Fid Q, Mr Paul, Mr II ni baadhi ya wasaniia ambao kwa kiasi kikubwa haipiti siku lazima utakutana nao kwenye mtandao huu maarufu kuliko zote katika ulimwengu wa Social Networking.

fid

Ukurasa wa Fid Q Facebook

Wengine ni Mwana FA, Albino Fulani, Judith Wambura, na wengineo kibao. Mamia kwa maelfu ya vijana ni wanachama wa mtandao huu ambao hata Rais wa Marekani Barak Obama alikiri kutumia muda wake kwa wakati fulani kwenye mtandao huu.

Hii ni njia nzuri ya kuweza kuwasiliana moja kwa moja na funs wao ambapo kama mtu ana swali, hoja, ushauri anaweza kuuliza moja kwa moja pasi na kutegemea radio na magazeti pekee ambapo washabiki wa wanamuziki hawa walioko nje hawapati nafasi ya kukutana nao.

mrpaul

Paul Mbena akiupamba ukurasa wake na Picha yake na Mwanaye mpya!!! Hongera kaka.

Facebook ni mtandao ambao unajipatia umaarufu na kuwa na watumiaji wapya zaidi ya 10,000 kila siku huku ikikisiwa kuwa asilimia zaidi ya 30% ya vijana wa mijini kwenye nchi zinazoendelea na 85% kwa nchi zilizoendelea wamejiunga na mtandao huu.

Facebook kwa sasa inatumika kama sehemu ya kufanyia kampeni, kutangaza biashara, na hata kujuika na marafiki toka pande mbalimbali za dunia.

Mwaka jana Waziri wa Elimu ya Juu wa Malaysia DATOO TAN SRI MUHYIDDIN MOHD YASSIN alitangaza kuwa kila alhamisi hutumia masaa manne kujibu maswali ya wanafunzi kupitia mtandao huu.


%d bloggers like this: