Sporah wa The Sporah Show

image

Katika mfulilizo wetu wa kuongea na vijana ama waliokatika sekta ya burudani au michezo ambao ama waliwika lakini jamii haijui kwa sasa wako wapi na wanafanya nini au wale ambao wako nje wanafanya mambo makubwa ambapo wengi wetu hatuyajui.

Hivyo basi napenda kutambulisha kwenu Irene Sporah Njau. akiwa ni mtangazaji wa kipindi cha Sporah Show ambacho kinarushwa na Television ya BET huko Uingereza na kuonekana baadhi ya sehemu kadhaa za Nchi za Ulaya.  Yeye ni nani, yuko wapi ana anafanya nini, ni moja ya mambo ambayo atatujulisha mwenyewe katika maswali na majibu yetu leo hii.

Naamini kwamba watu wakijua kuna kazi nzuri nyumbani watakua wanataka kusoma nakumaliza ili warudi nyumbani. Jamani nani anaetaka kuishi nchi za watu? Kazi ngumu, maisha magumu, tamaduni tofauti.”

Swali: Hallo Sporah habari yako?

Salama kabisa.

Swali: Labda kwa kifupi tupe Historia yako.

Jinalangu ni Irene Sporah Njau… Ni mototo wamwisho katika familia yangu, nilimaliza kidato cha sita Kampala–Uganda, nabaada yahapo nilikuja Uingereza kujiendeleza na masomo. Katika purukushani zakutafuta maisha nilijikuta nasomea vitu tofauti..

I hold IT Certificate in Desktop publishing

I hold a BET on Business and Finance

I hold a National Diploma in TV presenting

I have a National Diploma in Accounting and Businesss Management na sasaivi niko mwaka wangu wa mwisho at London Metropolitan University nasomea degree ya International Business Management.

Swali: Wakati unaondoka Nyumbani wazo lako lilikuwa nini, kuja kusoma ama kuja kutafuta maisha nini lilikuwa focus yako?

Kwakweli naweza kusema nilikuwa na mawazo yote pamoja, ila cha muhimu zaidi nilichohitaji ni Elimu. Hata hivi sasa bado naona elimu ni muhimu sana kwangu, na ndio maana bado naenda shule pamoja na kutumia muda wangu kuendesha kipindi cha The Sporah Show.

image Sporah katika pozi tofauti.

Swali: Tumeona vijana wengi wanaokwenda nje wanabadili mwelekeo kutoka kwenye elimu na kutafuta maisha zaidi unaliongeleaje hili?

Ni kweli kwamba vijana wengi wakifika Ulaya hubadili mwelekeo. Lakini mimi naweza kusema yote hii ni kwasababu ya ugumu wa maisha. Maisha ya Ulaya ni magumu sana ukichanganya na shule ndio yanakuwa magumu zaidi nahasa kwa wale ambao hawapati msaada wowote kutoka nyumbani.

Kwa kweli inataka moyo sana maana shule ni ghali, na maisha ni ghali, Ankara za mailipo ya huduma mbalimbali ni nyingi na bado nyumbani hawajakutumia mahitaji mbalimbali, kusaidia ndugu hapa na pale! kwakweli ni ngumu.

Kwa hali hivyo wengi wetu wanaishia kusimamisha masomo kwa muda fulani ili wafanye kazi kidogo wakusanye fedha za kutosha kabla ya kurudi shule.

Hapo ndio wengi wao wanajikuta hawarudi tena shule. Ukishaanza kufanya kazi na kupokea mshahara, kurudi tena shule inakuwa vigumu

Sio hilo tu pia wengi wetu tukiwa ulaya tunaona kama shule sio muhimu wengi usema sasa hata nikisoma ntaishia hapa hapa ulaya kufanya kazi hii hii, kurudi nyumbani siwezi kupata kazi hivyo wanapoteza ramani ya maisha kabisa.

Kwa hili nadhani serikali yetu pia inatakiwa kujaribu kutengeneza mfumo mzuri ambao utasaidia vijana kutapa motisha ya kurudi nyumbani na kuendeleza taifa letu .

Naamini kwamba watu wakijua kuna kazi nzuri nyumbani watakua wanataka kusoma nakumaliza ili warudi nyumbni. Jamani nani anaetaka kuishi nchi za watu? Kazi ngumu, maisha magumu, tamaduni tofauti.

Serikali yetu iliangalie hili kwaundani zaidi.

Swali: Tukirudi kwenye kipindi chako uliwaza nini kuwa na kipindi hiki na wapi hasa ni walengwa wako na kwanini umewalenga wao?

Kwakweli ilikuwa ni ndoto yangu, Ila nilipofika Uingereza nakuona jinsi ambavyo nchi zawenzetu zinamifumo tofauti ya kuelimisha jamii.. hii ilinipa motisha zaidi ya kutaka kutimiza ndoto yangu ndipo nilipoanzisha kipindi cha The sporah Show.

Ukizingatia kwamba hakukuwa na kipindi kingine cha Television kilichokuwa na dhamira kama yangu ya Kuelimisha, Kuburudisha na Kujulisha, haswa katika jamii yetu ya kiafrica huku Ulaya.

Tukiwa kama waanzilishi wa African Talk show hapa Uingereza, na Europe kwa ujumpla. Namshukuru Mungu muitikio ulikuwa mzuri hivyo kunipa morali zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi.

image

Sporah akiwa kazini akiongea na Miss Ugandan Uk.

Swali: Unawezaje kupima mafanikio ya dhamira yako kwa kupiatia Sporah Show, I mean unafikiri ulilotaka limetimia?

Oooh Nooo!!!

Bado kabisa sijafikia lengo langu.

Lakini namshukuru Mungu kwa sasa nimeweza angalua kutimiza ndoto yangu japo bado sijafikia malengo yangu lakini naamini nitafika kwani mwanzo ndio unakuwaga mgumu. Pia namshukuru sana Mungu kwani kwasasa nawenza kusimama nakuongea nakusikilizwa na watu kupitia kipindi changu (The Sporah Show) hapa UK na Europe kwakweli majibu ni mazuri, nafarijika sana kuona hivi.

Safari bado ni ndefu kwani ndoto yangu ni kipindi cha Sporah Show kuonekana Mataifa yote duniani. Dhamira yangu ni kuelimisha, Kuburudisha na kujulisha dunia kwaujumla haswa vijana wa ulimwangu huu wasasa.

Swali: Muitikio wa Vijana ukoje kwa ujumla kuhusu kipindi chako, unapata feedback zozote kama ni negative au positive feedback?

Kwaweli muitikio ni mzuri sana tu.

Namshukuru Mungu tunapata support nzuri kutoka kwa vijana hivyo kuturahisishia kazi kidogo.

The Sporah Show inawapa vijana nafasi yakuja kuonyesha vipaji vyao na pia inatoa nafasi kwa wafanya biashara kuzitangaza biashara zao kupitia kipindi chetu.

Swali: Kumekuwa na malalamiko ya maporomoko ya maadili kwa vijana, hili unalizungumziaje ukiwa kama muelimisha rika katika jamii, nani hasa wa kulaumiwa?

Wow!! Swali zuri

Kwakweli tatizo la maadili kwa vijana ni kilio cha dunia nzima, hata kwenye zile nchi ambazo zilikua zinafuata tamaduni zao.

Vijana wamekuwa wakipata pear pressure kutoka kwenye TV na Magazine, hivyo wanajikuta wanaingia kwenye makundi mabaya

Watoto wengi wanakua wakiiga vitu kutoka kwenye magazeti na television na nakuanza starehe wakiwa na umri mdogo. Kwahiyo nadhani pia wazazi wanatakiwa wawe makini kidogo na wasitupe tamaduni zetu. Ni vizuri sana kuwalea watoto namaadili mazuri mpaka watakapokua wakubwa ndipo wachague maisha yao wenyewe.

Tukirudi kwenye upande wanani wakulaumiwa!

Binafsi nadhani wazazi wana jukumu kubwa katika jambo hili. Wazazi wanatakiwa wawafundishe watoto wao maadili mazuri wakati wakiwa wadogo kama tamaduni zetu, hivyo watoto pia watakuwa wakijua wanatakiwa kufuata maadili mazuri na hivyo wataendeleza turidhisha kizazi hadi kazazi. Kwani wazazi wasipo fanya hivyo watoto hawatakuwa na kitu cha kufundisha watoto wao na hivyo kizazi chote kitateketea na mmomovyoko wa maadili

Pia upendo nikitu cha muhumu sana kwa watoto, wazazi wajaribu kuwaonyesha watoto wao upondo ili wasiende kutafuta upendo nje. Na pia wazazi wanatakiwa kujua kwamba kumuonyesha mtoto upendo haina maana kumpa mtoto uhuru wakufanya chochote anachotaka.

image

Sporah akiwa na mdau

Serikali pia inajukumu kumbwa katika jambo hili ili kushirikiana na wazazi.

Serikali ingejitahidi kuhakikisha kila shule inakua na angalau masaa mawili ya vipindi vya tamaduni na michezo kwa watoto ili kudumisha tamaduni zetu. Bila kusahau serikali inatakiwa kusaidia mashuleni vifaa vya michezo na mambo mengine mbalimbali ili kuwapa watoto vitu ambavyo watakumbuka wakiwa wakumbwa na kuwa nakitu chakujivunia kwa mataifa mengine.

Swali: Katika vipindi vyako ni kipindi gani ambacho ulitengeneza hadi mwenyewe ukakikubali na kwa nini?

Nivingi kwakweli ila naweza nikasema KNIFE & GUN CRIME IN THE UK (Uhalifu wa kutumia visu na silaha)

Hii ni kwasababu, tuliungana na vijana ambao walikua wanabeba silaha na waadhirika wa jambo hilo na wazazi waliopoteza watoto wao kupitia GUN &KNIFE CRIME (Uhalifu wa kutumia visu na silaha)

Kwakusaidiana na Wazazi tulijaribu kuelimishana adhari za jambo hili, watu wengi sana walielimika kuhusu jambo hili na vijana wengi walijitokeza kuelezea jinsi gani walivyo adhika na kwamba wameacha nawameanza maisha mapya. Kwakweli nilijisikia vizuri sana kuona hivyo kumbe na weza kubadisha maisha ya watu kwa kupitia kipindi changu.

Unaweza kuangalia video hiyo na nyingine nyingi kupitia YOUTUBE kwawanaotaka kuangalia video hizo ziko kwenye YOUTUBE.. www.youtube.com/sporahshow (Gonga Player kupata mambo)

10. Kwangu mi nakuona kama umefanikiwa hasa kwa ambacho unakifanya ukizingatia uko nje ya nchi kazi ambazo mara nyingi tumeona vijana wa mataifa mengine wakizifanya, je unaweza kusema ni nini siri ya mafanikio yako kwenye hilo?

Asante sana.

Kwakweli hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi zangu zote na pia kuwa na watu wazuri na wenye upendo wakweli.

Kama unavyojua vitu kama hivi ulaya vinafanywa na watu wamataifa makubwa hivyo mimi Sporah kufanya kitu kikakubalika na watu natakiwa kufanya mara 10 ili kuweza kukubalika na mataifa mbalimbali hapa UK na Europe kwa ujumla.

Nimepoteza marafiki wengi sana, kwasababu nimekuwa busy nafanya kazi wakati wote na kuendesha kipindi sio kazi ndogo. Wakati mwingine najisikia vibaya kupoteza marafiki lakini nakua sina jinsi kwani hii ni ndoto yangu hivyo ni faraja kwangu kuitimiza.

Swali: Uliwahi kuwaza kuwa na kipindi kama hiki kwa Television za nyumbani?

Absolutely yes … Nimeshakuwa approched na TV station tofauti za nchi za Africa.lakini bado sijaamua nianzie wapi, kwasababu bado niko shule hivyo najaribu kuipa shule kipaumbele mpaka hapo ntakapomaliza. Lakini nyumbani muhimu… Hahaaa SPORAH SHOW lazima ije nyumbani.

image

Sporah akiwa na baadhi ya wadau katika jitihada zake za kuongea na watu mbali mbali.

 

Swali: Unalizungumziaje suala la uhuru wa habari kwa sehemu unayoifanyia kazi na nini mipaka yako? Ukilinganisha na hali ilivyo nyumbani unadhani tuko sawa?

Kwakweli sina uhakika sana maana sijawahi kuwa kwenye media nilivyokua nyumbani

Ila nadhani kutakuwa na tofauti kwani huwezi fananisha nchi za ulaya na nyumbani tofauti ni kubwa sana kwenye mambo mengi .

Swali: Katika Production zako kuna mahali uliwahi kukwazwa au kupata matatizo yeyote kutokana na kipindi ulichotengeneza au wakati wa kutengeneza kipindi?

Hapana

Swali: Unaizungumziaje nafasi ya mwanamke wa Kiafrika kwenye Ulimwengu wa habari?

Mimi binafsi naona wanawake wanauhuru katika katika ulimwengu wa habari kama alivyo mtu mwingine. Kama mwanamke anaweza kulea mototo akaja kuwa Raisi, Mbunge, Daktari, mwalimu na Mwanasheria!!! Then kwanini wasipewe uhuru kwenye ulimwengu wa habari?

Swali: Kwa mfano ukapewa nafasi ya kumshauri Raisi kuhusu vijana kwa Tanzania ya leo, yapi utayapa umuhimu?

· The fact are on an annual basic, Tanzania is loosing thousands of young Intelligent, Talented and hard Working into Western world for studying reasons…..

The question is how many of these do come back home? And why don’t they want to come back to home….?

Hinyo ushauri wangu kwa Mheshimiwa Rais ungekua ni kuangalia jambo hili kwa undani zaidi.

image

Sporah akiwa mmoja wa majaji kwenye mashindano ya Miss Central Afrika.

Swali: Who is your role model na kwanini?

Must be… Mama yangu na Dada yangu.

Kwasababu wamenilea viziri nakunipa maadili mazuri ambayo yananiwezesha kuishi nawatu vizuri na hasa kufika hapa nilipo leo hii. Nawapenda sana.

Swali: Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia nje ya nchi kwenda kutafuta maisha huko na wengi wamekuwa wakiondoka kwa gia ya kutafuta shule zaidi lakini kiukweli wengi wao wanaishia kutafuta maisha kwa kufanya kazi za vibarua na si elimu, kwa uzoefu wako wa maisha ya nje hili unalizungumziaje?

Kwakweli, nitarudi tena kwenye serikali nadhani serikali inatakiwa kuliangalia jambo la ajira vizuri.

Watu kungangania ulaya na kufanya kazi zakubeba mabox na elimu zao (Degree, Masters, PHD’s) ni kwasababu ya ukosefu wa ajira nyumbani na hali ngumu ya maisha

“People feel like they cant achieve anything back home other wise you have good connection and people you can trust in the high sector. Otherwise there is no light after the tuner”

Hivyo serikali inatakiwa kutafuta nyenzo rahisi kuwaraisishia vijana kupata kazi bila kuwa na hofu yakwamba natakiwa nimjue fulani ili kupata kazi.

image

Ni vizuri kuzungumza na vijana na hasa wakiongea na kijana mwenzao kwani huondoa uoga na kuwafanya wawe huru zaidi kuongea.

Swali: Nini matarajio yako ya baadaye

Sporah Show kuonekana dunia nzima.

Swali: Mwisho kabisa napenda tu kujua interest zako.

Mimi ni muumini mzuri hivyo na penda kwanda kanisani na pia I like to learn new things.

Swali: Kama una lolote la kuongeza please do,

Ningependa kukushukuru sana kwakunipa nafasi hii.. na pia natanguliza shukurani zangu kwa watanzania wote kwaujumla kwakunipa support katika kazi yangu. Bila kusahau washabiki wangu wa FACEBOOK, TWITTER. Asanteni sana, naningependa kuwakaribisha wengine wote ambao hawajajiunga katika my FACEBOOK ambayo ni THE SPORAH SHOW au SPORAH NJAU.

Namwisho ningependa kuitambulisha The Sporah Show kwa wote na hasa kwa wafanya biashara na Makapuni yanayohitaji kujitangaza Uingereza, Europe Asia, Middle East and Africa, .

The Sporah Show, which is an African Talk show that airs on SKY 184 Every Monday at 10:30pm on BEN Television.

BEN TV is the Europe’s first and biggest black satellite TV channel on Sky 184 which also received in Asia, Middle East and Africa

We are respectfully inviting your Company to use this great opportunity to showcase its services by way of Sponsorship or Advertisements during the programme.

Our Viewership

The Sporah Show is shown weekly slot on SKY TV, Statistically, we have over 900000 weekly viewers

We are respectfully inviting your organization to use this great opportunity to showcase its services/products by way of sponsorships or advertisements during the programme. The estimated TV audience would benefit tremendously from your generosity.

Sponsoring Sporah Show will serve as great benefit to your institution in terms of the following:

· Promoting your corporate expertise.

· Increase your product and services recognition.

· Expand your sales opportunities with new prospects and existing clients.

· Help you in building new and enhance current client relationships.

· Taking  your visibility up a notch considering BEN TV’S large audience base (1.3 million people watching in the UK alone and accessible to over 30 million homes worldwide)

· Associate your name with the most prominent viewers.

Asanteni sana – http://www.sporahshow.com

54 Responses to Sporah wa The Sporah Show

 1. Ndrile says:

  I like the Interview ila mbona hujasema kama ameolewa au lah?

 2. Anonymous says:

  Nampenda sana huyu Dada Kaka angu basi tu, anani inspire sana ningependa kuwa kama yeye.

 3. Anonymous says:

  Nampenda sana huyu Dada, she is my role model

 4. Anonymous says:

  Mbona hakuna maswali ya relationship? Atupe ushauri hasa sisi vijana jinsi yakudili na mapenzi.

 5. Anonymous says:

  Asante sana mjomba, huu ni mfano mzuri sana kwa vijana wetu,nitahakikisha mtoto wangu anasoma hii interviw ili ajifunze. napenda anavojibu maswali, anaonekana anaakili, pia hivo anavoonyesha kwamba ameenda shule, amesomea mambo tofauti, kwakweli am impress because vijana wengi hawapendi kujiendeleza kimasomo hasa wakishajijua kuwa ni wazuri.Huu ni mfano mzuri sana kwa wakinadada wakitanzania.

 6. Anonymous says:

  Aiseee, Nampenda sana huyu dada. Ila mbona hajasema kama yupo kwenye relationship auvipi na atuambie siri yaurembo wake.

 7. Anonymous says:

  Huu udaku wa nguvu ungewekwa kwenye majira bongo li wakina dada wajifunze waache kutembeza uzuri waende shule uyu dada ni mfano mzuri sana

 8. Anonymous says:

  Hii imesimama kaka

 9. Haiwezekani kujibu swali ambalo hujaulizwa,yeye hakuulizwa hilo swali la kama yuko kwenye relationship au bado yuko single,hivyo tunamuomba yeye mwenyewe kwa kauli yake atueleze kuhusu hilo kwani ni vyema tukajua mapema ili nasi tujaribu bahati zetu maana dada mwenyewe naye anatazamika kwa nguvu sana,tafadhali tunahitaji kujua status ya relationship yako,bado uko huru au tayari umeisha tiwa mbaroni?

 10. William says:

  Why not? Nothing is impossible under the sun!!!!!!!!!!!! Keep it up sister!!!!!!!!!!Jah bless!!!!!!!!!!!

 11. tinna says:

  hongera sana dada kazi nzuri

 12. fatma tinna says:

  hongera sana mdada kazi nzuri sana,Mungu akubariki mno pia nakuomba sana achana na hao wanaotaka kujua habari za relationship achana nao kabisa fanya kazi kwa bidii na uangalie mbeleeee wanawake tupo juuuuuuuuu.

 13. Hi dada!
  Umepiga hatua nzuri na mungu akufanikishe zaidi.Tunapomuona mbongo mwenzetu anafanya mambo makubwa na mazuri hatuna budi kumpongeza tusisubiri afariki tumpe zile sifa za marehemu. Hongera sana na ni changamoto kwa vijana wengine wachacharikaji.

 14. Mr Shili says:

  Your doing the right thing Sporah, your interview was beautifully done! good questions were asked and perfect answers were answered.
  I am in a middle of finishing my two TV shows to be aired in one of the education channel in KCEN (Time Warner Cable) , Kansas City , MO(USA) i will probably talk to you sometimes in the future.

 15. Eugene Matemu says:

  Du!!,Mr Sam umeongea la maana sana,wabongo wengi wamezoea kutoa sifa mtu anapokuwa hayupo!!, kweli Dada Sporah unahitaji sifa zote maana kuweza kuwashawishi wazungu au walio nje ya tanzania kuamini kuwa tunaweza si rahisi kabisa.Tukushukuru wewe uliyeamua kuwa na wazo la maana la kuanzisha kipindi cha SPORAH SHOW kuweza kututambulisha wabongo na kutuwekea heshima ulimwenguni.Ila tu hebu jaribu kufanya mpango vipindi vyako hasa unapohojiana na wabongo vionekane na hata baadhi ya TV station za huku Afrika maana si rahisi kwa walio wengi kuweza kukuona pia kupata uwezo wa kununua Satelite Dishes au kusurf kwenye Internet kukuona na vipindi vyako.
  Cheers.

 16. wish all the best in your carrier

 17. Anonymous says:

  KIJANA UNAJITAHIDI

 18. Harrison says:

  DADA HUYU NA VIJANA WENGINE WANA JUHUDI YA MAISHA NA WANAJISOMESHA NA WWENGINE WAMEWEZA KUJISOMESHA ULAYA LICHA YA GHARAMA KUBWA, LAKINI SERIKALI BADO HAIONI HILO.
  KUNA WATOTO WA MAFISADI AMBAO NDIO WANASOMESHWA NA PIA KUANDALIWA KAZI NZURI NYUMBANI. SERIKALI NAOMBA ITAMBUE KUWA VIJANA WENGI NA WENYE VIPAJI NA WALIOWEZA HATA KUONYESHA VIPAJI VYAO KWA KUJISOMESHA ULAYA LICHA YA GHARAMA YA ELIMU, WANAISHIA ULAYA KWA SABABU HAWANA WATU WANAOWAJUA ILI KUPATA KAZI KAMA NCHI YETU ILIVYO, KUWA KAMA HUMJUI MTU HUNA LOLOTE. NA KWA UTARATIBU HUU NCHI YETU INABAKI PALE PALE.

 19. Mwakyusa says:

  Hongera sana mdogo wangu.

  Serkali inapasa iangalie upya sera zake za kusaidia ajira kwa vijana. Iwapo serikali haitalitambua kosa leke basi muda si mrefu nchi za Ulaya zitakuwa na mawaziri na viongozi wengi toka Tanzania. Hivi sasa watanzania wengi wanaporudi nyumbani na kukosa kazi wanageuza na kuja tafuta kazi Ulaya. Watoto wa kizungu hawataki hivyo leading doctors, engineers, universities professors, etc. miaka 10 ijayo kwa hapa UK wengi sana watakuwa ni Africa wakiwemo wa Tanzania. Africa itabakia inapoteza wasomi kwa sera na siasa yao mbovu

 20. Grace S. says:

  MY dear mi nimesoma interview yako kweli imetulia mnooo…. Mdada upo juu unatishaaaaaaa……. sina la zaidi ya kukuombea kwa MUNGU akupe afya njeka na maisha marefu, na yote unayotarajia kuyafanya yafanikiwe, umeweza kuanza mpaka ukafika hapa basi huko mbele sidhani kama kuna kitu kitashindikana. Keep it up sweet!!!!!!!! God bless you, love.

 21. salum says:

  Big up,especial for the course ure undertaken,international bussiness,i like it,im currently studing masters in international trade sister course of Internatinal bussiness,i think u ll be good international marketer and presenter,big up.keep it up

 22. Mbongo says:

  Ninachochukia wabongo wengi akiwemo huyu Sporah ni ile tabia ya kujibu maswali ya kiswahili kwa kuchanganya na kiingereza. Sijui huwa wanadhani kuwa kuchanganya na kiingereza ni fahari. Ninajua kuwa inawezekana kuna mambo ambayo tunayajua kwa kiingereza tu hivyo hatuwezi kujizuia kuyasema kwa kiingereza kwa vile hatujui kiswahili chake au ni rahisi kufanya hivyo, lakini hainiingii kichwani mtu kujibu swali kwa kuchanganya sentensi za kiswahili na kiingereza; inakuwa ni nongwa sana.

  Hebu Angalia:

  Swali: Labda kwa kifupi tupe Historia yako.

  Jinalangu ni Irene Sporah Njau… Ni mototo wamwisho katika familia yangu, nilimaliza kidato cha sita Kampala–Uganda, nabaada yahapo nilikuja Uingereza kujiendeleza na masomo. Katika purukushani zakutafuta maisha nilijikuta nasomea vitu tofauti..

  I hold IT Certificate in Desktop publishing

  I hold a BET on Business and Finance

  I hold a National Diploma in TV presenting

  I have a National Diploma in Accounting and Businesss Management na sasaivi niko mwaka wangu wa mwisho at London Metropolitan University nasomea degree ya International Business Management.

  Swali: Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia nje ya nchi kwenda kutafuta maisha huko na wengi wamekuwa wakiondoka kwa gia ya kutafuta shule zaidi lakini kiukweli wengi wao wanaishia kutafuta maisha kwa kufanya kazi za vibarua na si elimu, kwa uzoefu wako wa maisha ya nje hili unalizungumziaje?

  Kwakweli, nitarudi tena kwenye serikali nadhani serikali inatakiwa kuliangalia jambo la ajira vizuri.

  Watu kungangania ulaya na kufanya kazi zakubeba mabox na elimu zao (Degree, Masters, PHD’s) ni kwasababu ya ukosefu wa ajira nyumbani na hali ngumu ya maisha

  “People feel like they cant achieve anything back home other wise you have good connection and people you can trust in the high sector. Otherwise there is no light after the tuner”

  Hivyo serikali inatakiwa kutafuta nyenzo rahisi kuwaraisishia vijana kupata kazi bila kuwa na hofu yakwamba natakiwa nimjue fulani ili kupata kazi

 23. Anonymous says:

  Acheni nyie huyu dada yuko juuuuuuuuuuu

 24. Tonny says:

  I love what you are doing…keep inspiring other bongoz and Africanz at large. We got your back always…

 25. Joyce says:

  Go Girl
  Nilifurai kujiunga na Sporah kwenye facebook yake, kweli simjui ila nilimtumia meseji kumuomba ushauri kama mwanamke mwenzangu hata sikujua kama ye ni mbongo na akanijibu palepale nakunipa ushauri mzuri sana kitu ambacho mastaa wengi wa bongo hawafanyi hasa kukujibu meseji tena walalahoi kama sisi kwakweli alinifurahisha.. Spora tunakukaribisha bongo njooooooo we love yuuu

 26. Mzee Mjuma says:

  wewe unaesema English Vs Swahili labda hujakaa nchi za wtu, hata ukikaa japani utajikuta unachanganya kijapati na kiswahili, hata kama ukikaa sn mikoani utajikuta unachanganya kiligha chako na kiswahili. Embu jaribuni kuwa waelewa na mkubali pale mu anapofanya mambo mazuri n hiyo ndio njia moja tu ambayo itatusaidia sisi wa Tanzania kuendelea. Wasifieni watu wenye vipaji vyao ili waongeze juhudi jaribuni kuappreciate jamani vinginevyo hatutafika. Huyu dada anafanya mambo mazuri sana ambayo yanaelimisha jamii, ameenda shule, jamani mbona tunatakiwa kujivunia sana tu maana sio rahisi kupata wakina dada kama hawa hivyo tukiwapata tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu.Atawasaidia vijana wengi sana hapa bongo ana Africa as whole.

 27. furaha tagalile says:

  I like this girl!! keep it up u’r carrier!

 28. maya says:

  Go girl,
  you are doing good job, well done.

 29. frozy says:

  nimeipenda kazi yake na nitafurahi sana nikikutana nae siku moja ili niweze kuongea nae mawili matatu au hata awe mmoja wa wasomaji wa blog yangu au hata niwe naandika kuhusu kazi zake

 30. frank says:

  Big up girl kazi nzuri sana, sasa tumia nafasi hiyo kuitangaza bongo land. uwe unatupa ushauri wa kimaisha sisi vijana huku bongo. usisahau nyumbani ok…?

 31. Glory says:

  I Love you so much Spora, i believe utakuja kumake big change hapa bongo kwa kazi unayoifanya.
  Keep it up na tunakukaribisha sana Bongo.

 32. Anonymous says:

  Kwakweli hata mimi huyu dada huwa ananijibu massage zangu, ma nilimuomba ushauri kuhusu mambo ya modeling akanijibu na akanipa ushauri na wala hata hanijui wasanii wengi hapa bongo kuongeanao tu kazi tena hasa kwa sisi wa mikoani.. nampenda Sporah she is very simple.BIG UP

 33. joy says:

  duhu ameimpress sana, amethibitgisha kuwa wabonngo na waafrika tunaweza

 34. julius kanje says:

  ooooh congratz ms njau,u show the way for many tanzanian women

 35. Nipo bongo Tanzania,nina e-mail nyingine ya yahoo,ambayo ni wajn_k@yahoo.com,nimependa historia yako ndugu yangu zaidi na zaidi, MUNGU akujalie kufika mbali zaidi,naomba msaada wako wa ushauri wa maisha tufanyeje tutoke kimaisha?ok

 36. Naima says:

  I love her so much, atakuja lini bongo?

 37. Mama mzumbe. says:

  Kaka hawa ndio mabinti tunaowataka kuwaona kwenye mablog, ili vijana wetu wajifunze.

 38. Anonymous says:

  MMMHH Kazi ipo hapa, kabinti kazuriiii

 39. Baba lindah says:

  Hii ngoma imeend shule DUUUU
  Sasa TV za Tanzania zinaitaji watu kama hawa, Sio Michezo yakijinga ambayo haitufundishi chochote, Watoto wetu hawajifunzi chochote, zaidi yakuwfanya wajinga.. Tunawataka kina dada kama hawa kwenye TV za Bongo ili vijana wajifunze kutoka kwao.
  Keep it up Sporah, we are proud of you.

 40. hussein says:

  sio insh

 41. suleiman says:

  HI sister, Ilike the way you talk and express your feeling, real your vition comes true go on dont give up, congratulation.

  • I will be using this data the next time I am working. Well, I have finished a long list. A ton of details to take into consideration. Write a lot more thank this, that’s all I have to say. I really enjoy this! Right here is some really useful information.

 42. Ernest Dennis says:

  hi sister sporah,natumai u mzima na pole na shughuli zako mimi pia ni mzima,naitwa ernest nipo dsm tanzania,hongera sana kwa hatua uliyofikia na mungu azidi kukuongoza

 43. Anonymous says:

  DUUUUUUU
  Wachaga na nyie ivi ni ndizi zinawafanyaga mnakua hivi.
  Mama Uko Juuuuuuuuuuuuu

 44. Tonny says:

  Hi sister, nimevutiwa sana na habari zako na zimenishawishi nianze kufuatilia vipindi vyako hasa kupitia star tv na hongera pia kwani kuweza kukubalika majuu na kupewa nafasi kwa channel zao si mchezo.Mwenyezi Mungu akutangulie!!!

 45. Nyasani,sam says:

  Hallo sister natamani sana ningekuwa mmoja kati ya team nzima unayoshirikiana nayo dada lakn ili unalolifanya ni kwa muda tu au ndo mwanzo mzuri wenye mwendelezo ‘nice moment’

 46. […] Ukitaka kujua mengi ya mwanadada huyu basi bofya hapa […]

 47. Anonymous says:

  Congrats Dada, Degree ya Uingerera sio mchezo.

 48. hadija wa Ayubu Abdallah says:

  nimependa mambo yako mtoto wa njau, karibu msitu wa mbogo kwa mama happy usisahau kusalimia kwa mzee mwakitubu,,ur my role model 4 sure

 49. Anonymous says:

  Kaza buti dada Sporah, upeo ulionao ni wachache sana wenye nao.

 50. Relatively selected he will have a very good study. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: