Mambo ya Titanium – Kuala Lumpur

January 19, 2010

image


Simba, Yanga wapiga “STOP” mechi zao kuonyweshwa luningani.

January 19, 2010

image

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Frederick Mwakalebela, leo alisema wamevipiga ‘stop’ vituo vya luninga kurusha ‘live’ mechi za Simba na Yanga zinazoendelea katika Ligi Kuu kufuatia ombi la vilabu hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Mwakalebela alisema hatua ya kusitisha kurushwa laivu mechi hizo itakuwepo kwa muda usiojulikana.

Majuzi Kiongozi mmoja wa timu ya Simba alipata wakati mgumu alipokwaruzana na maafisa usalama uwanjani akitaka kwenda kuzima Camera za vituo vya Luninga wakati wakirush mechi baina ya Simba na Majimaji.


Soka la Bongo linasikitisha; Machupa

January 19, 2010

machupa

Mchezaji Athuman Machupa “Gaucho” mbaye kwa sasa anacheza soka huko nchini Sweden ligi ya Superettan amesema kuwa anasikitishwa sana na soka la bongo linavyoendeshwa.

Machuma “Gaucho’ ambaye alikuwa hapa nyumbani kwa mapumziko amesema hayo alipokuwa akiongea na Spoti na Starehe.

Machupa amesema kuwa Tanzania inavipaji vingi kwenye soka inasikitisha kuona kuwa wengi wanamaliza muda wao kimpira pasi hata kucheza fainali za Kombe la mataifa ya Afrika, Aidha amesema kuwa kimsingi soka letu linaweza kusaidiwa na kocha wa kigeni endapo tuu TFF watafanya mchakato wa maana wa kuwatafuta makocha tofauti na walivyofanya kuitangaza nafasi hiyo, “mi nadhani tusitafute kocha kwa njia hiyo tujaribu kuangalia makocha kama phillip troussier mfaransa aliyekuwa kocha wa japan…claude leroy aliyekuwa camroun…Jean Tigana ni makocha ambao wanajua soka ya Africa inahitaji nini kaka la kama tunataka kuwa na kocha mradi kocha hatutofanikiwa” alisema Machupa.

Pia Machupa amesema kuwa binafsi yake haoni kama Maximo ameleta mageuzi kwenye soka la Bongo kwani bado Tanzania iko kwenye ranki ile ile, “mimi kwangu sidhani kama maximo alikuwa ana msaada kwetu wanaompigia debe ni kwamba alikuwa ana manufaa kwao ukizingatia hakuna la maana alilotufanyia angalia kwenye rank anazotuambia yeye hatujapanda ni renki zilezile za chini ya mia ndio alitukuta nazio na ndio katuacha nazo au uongo kaka? alihoji Machupa.

Shirikisho la Soka hapa nchini TFF kwa sasa liko kwenye mchakato wa kumtafuta kocha na kwa mujibu wa TFF nafasi iko wazi.

Nini wazoo lako?


%d bloggers like this: