CAN 2010: Kundi A

January 15, 2010

Wenyeji Angola wameimarika tangu Manuel Jose alipochukua hatamu Juni mwaka jana, baada ya kiwango kushuka na hatimaye kushindwa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2010 Afrika Kusini, huku wakipoteza mechi kadhaa za kirafiki.

Kocha huyo mchangamfu kutoka Ureno, ambaye aliwahi kuiongoza Al Ahly ya Misri kuwika katika soka ya vilabu barani Afrika, amerejesha ithibati kwa timu iliyocheza fainali za kombe la dunia 2006.

Angola yenye jina la utani Palancas Negras, imeshinda mechi mbili na kutoa sare saba kati ya 10 walizocheza kujipima wakiwa chini ya Jose, kipigo pekee walikipata walipotandikwa na Estonia huko Ureno, tarehe 30 Disemba.

Licha ya kuwa mojawapo ya timu zinazopewa nafasi finyu ya kushinda, wanatumai kuiga mfano wa Misri waliokuwa wenyeji wa michuano ya 2006, na Tunisia 2004 kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani kushinda taji lao la kwanza la Afrika.

Hata hivyo, lazima wasonge mbele kutoka mechi za makundi dhidi ya mahasimu wakiwemo Algeria waliowahi kushinda kombe nyumbani kwao – vile vile timu ya mwisho kunyakua nafasi ya kwenda Afrika Kusini, kwa kuichapa Misri katika mechi ya mtoano mwezi Novemba.

Mabingwa hao wa 1990 walishindwa kufuzu kwa mashindano mawili yaliyopita, lakini ushindi wao wa karibuni unaonyesha ni timu inayoweza kuinuka upya na kufanya mambo makubwa.

Kocha wa Algeria, Rabah Saadane amewaongoza Desert Foxes mpaka kiwango cha juu zaidi wakijikuta namba 26 katika orodha ya timu bora ya FIFA. Wanatumai kuendeleza ushindi wao waliopata kwenye hatua ya kufuzu.

Mara ya mwisho Malawi walifuzu kucheza mashindano haya mwaka 1984, wamekuwa wakijiandaa kuwa miongoni mwa timu chache za kusini mwa jangwa la Sahara.

Wakiongozwa na aliyewahi kuwa mchezaji wao nyota, Kinnah Phiri, wameangia mashindanoni wakionekana kama si wenye uwezo wa kubeba kombe, ingawa wamekuwa wakionyesha kiwango cha juu wakati wa mechi za kufuzu, bila kusahau ushindi waliopata dhidi ya Misri.

Pia wamepata mafanikio katika mechi za kujipima nguvu, ikiwemo dhidi ya jirani zao Msumbiji ambao pia wamefuzu, na sare walipocheza na Misri.

Mali, wanaocheza kwa mara ya sita, wamejaliwa vipaji, tatizo kubwa ni kwamba wengi wa wachezaji nyota wanacheza nafasi zinazokaribiana.

Kocha Stephen Keshi atapenda kuwatumia vyema viungo wake hodari lakini wenye mchezo unaoshabihiana, Mahamadou Diarra, Mohamed Sissoko na Seydou Keita, wakati Fredi Kanoute mshambuliaji anayechezea Sevilla, atabakia tegemeo katika ushambuliaji.

Kocha huyo mzaliwa wa Nigeria pia atakuwa na matumaini kuwa timu yake yenye wachezaji wanaosakata kabumbu Ulaya watafaika fainali kwa mara ya kwanza, mafanikio makubwa zaidi waliyowahi kupata ni mwaka 2002 walipofika nusu fainali.

Jumatatu, 18 Januari 2010

Angola v Algeria, Kundi A, 16:00

Mali v Malawi, Kundi A, 16:00


Jumanne, 19 Januari 2010

Burkina Faso v Ghana, Kundi B, 16:00

Ivory Coast v Togo, Kundi B, 16:00


Jumatano, 20 Januari 2010

Misri v Benin, Kundi C, 16:00

Nigeria v Mozambique, Kundi C, 16:00


Alhamisi, 21 Januari 2010

Cameroon v Tunisia, Kundi D, 16:00

Gabon v Zambia, Kundi D, 16:00


Jumapili, 24 Januari 2010

Washindi Kundi A v Wa Pili Kundi B, RF

Washindi Kundi B v Wa Pili Kundi A, RF


Jumatatu, 25 Januari 2010

Washindi Kundi C v Wa Pili Kundi D, RF

Washindi Kundi D v Wa Pili Kundi C, RF


Alhamisi, 28 Januari 2010

Washindi RF1 v Washindi RF4, NUSU FAINALI

Washindi RF2 v Washindi RF3, NUSU FAINALI


Jumamosi, 30 Januari 2010

Waliopoteza NS1 v Waliopoteza NS2, MSHINDI WA TATU


Jumapili, 31 Januari 2010

Washindi NF1 v Washindi NF2, FAINALI


Sporah wa Sporah Show!

January 15, 2010

4719_182065620087_830355087_7134009_2447769_n

Anaitwa Sporah Njau, Kwa wapenzi wa Ben Tv wanamfahamu mwanadada huyu machachari anayetamba na vipindi vyake maridhawa vya mahojiano.

Sporah ni nani alitokea wapi anafanya nini na yuko wapi?

Usikose wiki ijayo kwenye mfululizo wa makala zetu ambapo hupendelea kuongea na watu waliovuma na bado wapo lakini watu hawajui wako wapi ama wanavuma sana katika medani ya Burudani lakini hapa nchini watu wa kawaida hawawajui.

Pata kionjo cha Mahojiano yake ambapo hapa alikuwa akiongelea uhalifu kwa vijana.


Maisha Plus; Washiriki waanza kuonyesha Uhalisia wao!!

January 15, 2010

Wengi wapinga Pendo kulaumiwa!!

IMG_0080

Huku wakiwa na siku 12 katika kijiji cha Maisha Plus. Washiriki wa Reality Show ya Maisha Plus wameanza kuonyesha uhalisia wao na tabia zao. Katika siku za mwanzoni ilikuwa kazi kutambua tabia za watu kwani wengi  walionyesha kuigiza zaidi kuliko kuishi uhalisia wao lakini kwa sasa kila mmoja anaanza kutoa makucha yake” alisema mmoja wa mashabiki waliokuwa wakifatilia kipindi cha jana.

Mada hii ilikuja baada ya mshiriki mmoja kuamua kwa nia ya kufurahisha au kuchangamsha kuwatisha wenzie kwa kuvaa shuka jeupe na kujipaka poda usoni, wengi wa mashabiki walifurahishwa na kitendo kile na walisema kuwa kimeonyesha ubunifu na kuchangamsha kijiji.  Jambo ambalo lilipingwa na washiriki ambapo asilimia kubwa waliangukia kulaumu.

IMG_0102

Washabiki wengi walionyesha kukerwa na kauli ya mshiriki toka Zanzibar ambaye alisema kuwa hatomsamehe Pendo mwanzo wa dunia na hata mwisho wa dunia na haikanushi kauli yake, jambo ambalo lilitafsiriwa vibaya na mashabiki waliokuwa wakifuatilia show hiyo.

Kitendo cha Pendo si kibaya kuwatisha wenzio ndio mambo yanayotokea vijijini na katika maisha ya kila siku kwa umri wake na jinsi alivyo ule ni uhalisia wake, amefanya mchezo umechangamka sioni mbaya kwa kweli alisema shabiki mmoja kwa jina la mwafrika.

Binafsi nilifurahishwa na washiriki wawili tuu katika kijiji ambao walilichukualia suala hili kama kosa la kwanza na kutaka mwenzao apewe nafasi zaidi jambo ambalo lilipingwa zaidi na washiriki wengine na siku ikaisha.

IMG_0088

Likifika sualala kazi ndio utamjua mchapa kazi na mvivu, kwa upande huu jamaa wanajituma


%d bloggers like this: