Diamond – Kamwambie

January 7, 2010

Hiki ni kizazi cha tatu cha muziki wa kizazi kipya ambapo huimba zaidi na hii style kwa sasa ndio imekamata soko la muziki kwa sasa. Nilibahatika kukutana na Juma NAture akawa anakandia sana hii style na kulaumu baadhi ya  viongozi wa sekta ya Muziki kuwa wanachangia sana kuubadili muziki ambapo mtu kama yeye analazimika kuimba na kutoka kwenye syle yake.

Binafsi nafurahia muziki wote ila mtiririko wa story kwenye style hii ya nyimbo una mguso wa kipekee ingawa hautambulishi upi hasa ni muziki wa kizazi kipya.

Hilo ni suala ambalo nitalijadili siku mbili zijazo hapa hapa.


Eneramo aachwa kikosi cha Nigeria

January 7, 2010

image

Michael Eneramo, ambaye huchezea Esperance, miamba ya Tunisia ameachwa katika kikosi cha Nigeria kinachofunzwa na Shaibu Amodu kabla ya kuelekea Angola kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Awali maafisa walithibitisha kuwa Chinedu Obasi, anayecheza Hoffenheim ndiye angeachwa kwenda Angola.

Lakini kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) Ademola Olajire, kikosi hicho chenye wachezaji 23 kilikamilishwa Jumatatu.

Kocha Shaibu Amodu alichelewesha kutangaza kikosi chake wakati madaktari wakitathmini hali ya Obafemi Martins.


Vieira atakiwa Manchester City

January 7, 2010

image

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, anataka kumsajili Patrick Vieira na kiungo huyo wa Inter Milan ameridhika na wazo hilo, BBC michezo imepata taarifa.

Vieira, 33, anaaminika kufurahishwa na uwezekano wa kurejea kucheza katika ligi ya England, ambako hajacheza tangu alipohama Arsenal kwenda Juventus 2005.

Nahodha huyo wa Ufaransa amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu ya kwanza.

Vilabu vingine pia vimeonyesha nia ya kumchukua, lakini Vieira anaona kuungana tena na meneja wake wa Inter, Mancini kuwa wazo zuri zaidi.


Ulamaa mzigoni!!

January 7, 2010

image

Ukiongelea chimbuko la Bongo Flava kuna vichwa lazima utavitaja, na kwa sasa tupo kwenye kizazi cha tatu kama sio cha nne cha Bongo Flava lakini kuna wakali wamo tuu. Anaitwa Solo Thang Ulamaa, akiwa masomoni huko Uingereza lakini bado anaiendeleza fani. Solo thang ni mmoja kati ya wanamuziki wa kizazi kipya waliokata shule na kuthamini shule, kwangu namuona ni mfano wa kuigwa.

Tuliwahi kufanya mahojiano naye kama yalikupita gonga hapa.

Read the rest of this entry »


Wa sauzi walia na Vuvuzera zao kombe la Dunia!

January 7, 2010

Mbombela Stadium, Nelspruit, South Africa

Chama cha Soka cha Afrika ya Kusini na Shirikisho la Soka wanaendelea kujadilia kuhusu uwepo au usiwepo wa Matarumbeta ya ushangiliaji maarufu kama Vuvuzera.

Baadhi ya mataifa yamewakilisha muswada kwamba uwepo wa Vuvuzera kwenye Fainali za Kombe la dunia mwaka huu kutafanya watu wengine wachanganyikiwe na kuongeza kelele pasi na sababu, Kwa upande wao waafrika kusini wakisema huo ni utamaduni wao, kwa vile hii ni mara ya kwanza mtanange huu kupiganiwa Africa ni vyema basi mataifa mengine yakajifunza utamaduni wa kiafrica ikiwemo ushangiliaji walisema viongozi wa kikundi cha shangiliaji kwa Vuvuzela cha Bafanabafana.

“Hawa watu hawalipwi na  timu ila ni washabiki wanafurahia ni sehemu ya burudani kwa nini wawe na uwoga?” alihoji kiongozi huyo.

Wakati huo huo Rais wa FIFA Blatter amesema kuwa hakuna mji hata mmoja unaweza kusema uko salama hapa duniani hata Uswis kwenyewe, Blatter aliyasema hayo alipokuwa akijibu hija kuwa Afrika ya Kusini sio salama na usalama wake ni mdogo.

Blatter alishauri kuwa ni vyema watu wakachukua tahadhali kama ambavyo wanafanya wawapo popote duniani na kuamini kuwa Serikali ya Afrika ya kusini itakuwa imefanya maandalizi ya kutosha likiwamo suala zima la usalama.

Baadhi ya viwanja vya Africa ya Kusini kwa ajili ya mtanange huo:-

Soccer City, Johannesburg, South Africa

King Senzangakhona Stadium, Durban, South Africa

King Senzangakhona Stadium usiku.

Port Elizabeth Stadium, Port Elizabeth, South Africa

Peter Mokaba Stadium, Polokwane, South Africa


%d bloggers like this: