Mali kumkosa Sidi Keita, Angola

image

Baada ya kuumia goti Mali itamkosa mchezaji wake muhiimu Sidi Yaya Keita katika mashindano yajayo ya mataifa ya Afrika nchini Angola mwezi wa Januari.

Keita, anayeichezea klabu ya Hispania ya Xerez, nafasi yake itazibwa na kiungo wa klabu ya Lens Samba Sow katika kikosi cha Mali.

Mali watacheza mashindano ya mataifa manne yatakayofanyika Qatar kuanzia tarehe 27 mwezi wa Disemba, pamoja na wenyeji nchi nyingine zitakazoshiriki mashindano hayo ni Iran na Korea Kaskazini.

Mchezo wa mwisho wa kujipima nguvu kabla kuanza mashindano ya mataifa ya Afrika kwa timu ya taifa ya Mali ni tarehe 4 mwezi wa Januari watakapozipiga na Misri huko Dubai.

Mali baadae watacheza mchezo wa ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika tarehe 10 Januari na wenyeji Angola kabla ya kujitupa uwanjani katika mechi za kundi lao la A na timu za Algeria na Malawi.

2 Responses to Mali kumkosa Sidi Keita, Angola

  1. This is very interesting, You are a very good blogger. I have enjoyed your feed and look forward to seeking more of your magnificent post. Also, I have shared your website in my social networks!

  2. Nikki Sprow says:

    a lot of fantastic info and inspiration, each of which I need to have, thanks to give such a useful data right here.

Leave a comment