Athmani Machupa: Tuache maneno tucheze mpira!

image

Soka la Tanzania limekuwa likikuwa kwa kususasua na miaka ya karibuni tumeshuhudia wachezaji wengi wakienda nje ya nchi kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulikwa wengi wao wamekuwa wakirudi na ahadi za matumaini na wachache kufanikiwa.

Mmoja wa wachezaji chipukizi aliyefanikiwa ni Mchezaji Athuman Idd Machupa aka Gaucho ambaye kwa sasa anacheza soka huko nchini Sweden ambapo anachezea ligi ya Superettan baada ya Premier League ya Sweden, Nimepata bahati ya kuzungumza naye machache ingawa muda ulikuwa hautoshi kwni kumpata huyu bwana si kazi ndogo. Tumeongelea maisha binafsi na maendeleo ya soka la bongo kwa ujumla,

Fuatana nami kwenye maswali na amajibu kati ya SS na Gaucho.

SS: Ebwana Mkuu salama? karibu kwenye kijiji cha Spoti na Starehe tubadilishane mawili matatu ya soka.

Gaucho: Shukrani mzee

SS: Kwanza wapenzi wa soka wangependa kujua uko wapi kwa sasa na unafanya nini kama hutajali kujibu hilo.

Gaucho: kwa sasa nipo stockholm ,sweden nakocheza mpira katika timu ya VASALUND IF iko superettan kwa hapa baada ya premier league ya hapa ndio inafuatia

SS: Vipi mipango yako imefikia wapi ya kupata timu ya kulipwa huko ulaya?

Gaucho: Kama nilivyosema nachezea VASALUND IF hapa Sweden

SS: Bado ni kijana mdogo na bado kiwango chako kiko juu ukiitwa timu ya Taifa na uko nje ya nchi je bado unaweza kulitumikia taifa na kujiunga nao?

Gaucho: bila wasiwasi ni fahari kwa kila mchezaji kuchezea timu yako ya taifa niko tayari muda wowote endapo nitaitwa. Kwani hata nchi nyingine zinawatumia wachezaji walioko nje.

SS:Ni yapi majaliwa ya soka la bongo ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo udhamini ulikuwa haba leo hii kuna wadhamini kibao na bado mafanikio yanakuja ingawa sio kwa kiwango mashabiki wanategemea unadhani shida iko wapi?

Gaucho: tuache ubabaishaji katika kila idara ili kuweka majaaliwa ya soka letu lifike mbali..wadhamini waungwe mkono na ubabaishaji usiwepo. Watu wajitolee na viongozi wapunguze migogoro haitupeleki popote.

image

SS:Kwa mtazamo wako unamzungumziaje kocha Marcio Maximo kwa muda ambao amekaa na timu ya Taifa ambapo baadhi ya Makocha wazalendo wamekuwa wakimponda kama Mziray ambapo anasema ye anaweza kufanya makubwa tuu zaidi ya Maximo hili unalisemaje?

Gaucho: ukiangalia tulipokuwa na tulipo sasa amefanya kazi kubwa sana katika kutuweka hapa tulipo..kwani makocha wazalendo nao walishindwa kutuwezesha japo kusonga hatua kumi mbele, tumpe ushirikiano yapo ya kujifunza kutoka kwake.

SS: Unapozungumzia soka la bongo unazungumzia Simba na Yanga, kwa miaka ya karibuni tumeona wanabadilika leo hii klabu inatoa Million 30 kumnunua mchezaji je unadhani tukibadili mfumo wa soka ya Tanzania na kuufanya wa kulipwa unaweza kuleta tija na mabadiliko kwa kiwango chetu cha mpira?

Gaucho: sidhani kama itawezekana kwani ubabaishaji utakuwa palepale.
image

SS: Tanzania ina vipaji vingi sana vya wanasoka lakini hatuna wanasoka wa kutosha kwenye medani ya soka kimataifa je unadhani tatizo liko wapi kwa wachezaji wa Tanzania kupenya kwenye soka la kimataifa?

Gaucho: kwetu sisi tunangangania mchezaji lazima aende Yanga au Simba badala ya kupandikiza mbegu ndogo zitusaidie baadae tuwekeze katika vijana.

SS: Je una wazo lolote kwa kocha wa Taifa Stars ukilinganisha na uliyoyaona nje ya nchi yetu?

Gaucho: tumpe ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa tunahitaji kusonga mbele na kuiangalia kwa ukaribu timu zetu za taifa za vijana.

image

Machupa Kulia akiwa na washkaji huko  Sweden


SS: Swali la mwmwisho la kizushi, Je umeoa a una mchumba Mzeiya?

Gaucho: nimeoa na nimemuoa amina bakari.

SS: Nashukuru sana kwa muda wako mkuu Siku njema kila la heri.

Gaucho: nashukuru kwa ushirikiano wako….

image

Akiandaa maakuli

Advertisements

8 Responses to Athmani Machupa: Tuache maneno tucheze mpira!

 1. Ndambo says:

  Maswali mazuri sana nakupongeza muuliza maswal dogo umejibu kihuni ndio tatizo la Watanzania, Namshukluru aliyemkosoa Hasheem mwanzo alokuwa hivyo siku hizi anaongea Vizuri mnatabia ya kudharau vyombo vya nyumbani nyambafu, ila poa tu nakupa Big up kwa mafanikio hayo

 2. Anonymous says:

  Safi sana mpwa heko kila la heri
  Mdau Kinondoni Biafra

 3. Anonymous says:

  Hongera kaka kwa kupata timu ila usianze starehe huko utapoteza mpira wako nakuaminia mdau wa Msimbazi hapa.

 4. Anonymous says:

  Mkuu Saluti kamanda nakukubali kutoka Chandimu hadi Maulaya baaabu kubwa ila kweli kaka maswali umejibu kimagomeni sana bwana.

 5. Jordan says:

  Machupa,babu kubwa na umejibu maswali vizuri kwa sababu hapo naamini umejitahidi sana kuongea lugha laini kwa maana wasokasoka wa nyumbani hapo akawii kujibu kimaskani,msijali wadau mshikaji atabadilika na atakuwa mfano wa kuigwa,mdau uk

 6. husna says:

  muddy chella wapi kaka kitambo

 7. I want you to thank for your time of this excellent read through!

 8. Good data, exceptional and useful design, as share great stuff with good thoughts and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: