Mwanza wavunja rekodi kampeni ya Miss Tanzania 2009

2 Mbiringe mbiringe za mtanange wa ulimbwende wa Miss Tanzania unazidi kunoga baada ya mikoa na kanda kujiimarisha kila mmoja akikusudia kunyakua taji hilo kubwa la Ulimbwende nchini, Mkoa wa Mwanza uko mbioni kukamilisha ratiba yao na mwaka huu wamo warembo waliotimia idara zote akiwemo Grace Bani (23), Binti albino ambaye kwa mujibu wa waandaaji Flora Entertainment wanasema ametimia idara zote ana ataleta upinzani. Hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya urembo kwa watu wa kundi hili kushindania taji hili.

Ama kwa hakika hili ni jambo linalotakiwa kupongezwa na kila mpenda amani kwa ukizingatia mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji na ukatili dhidi ya jamii ya watu wenye ulemavu wa Ngozi (albino) kwa visingizio vya kutumia viungo vyao katika imani za kishirikina.

Hii ni changamoto kwa jamii na italeta muamko kwa jamii nzima, kwani inaonyesha baada ya kupigiwa kelele sasa jamii imeamka na kuwatambua wenzetu hawa, kwani ni hivi karibuni katika shindano la ulimbwende la Miss Universal kundi maalum la Ngoma la Albino lilipewa nafasi kutumbuiza katika mashindano yale yanayoheshimika kwani kwenye historia ya Urembo warembo wa kundi lile toka Tanzania walifika mbali. Taji la Miss Tanzania linashikiliwa na Nasreem Karim ambaye anatokea mkoa wa Mwanza.

picha na Jiachie, Pius Grafix

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: